Monday, December 28, 2009

Website ya African Lyon Sports Club

http://www.africanlyonfc.com/

Yanga ndio mabingwa wa Tusker 2009


wachezaji wa Yanga pamoja na baadhi ya viongozi wao wakishangilia kombe hilo jana baada ya kuifunga timu ya Sofapaka tokaKenya bao 2-1 katika uwanja wa Taifa

Kwa Hisani ya Micuzi blog

Thursday, December 24, 2009

Heri ya Krismas wadau wote msomao blog hii!



Mimi Mlaule DJ na familia yangu tunapenda kuwapa heri ya Krismas, muwe na sikukuu yenye amani, utulivu na barka tele.
Mungu muumba mbingu na nchi na vitu vyote awabariki sana!

Viongozi wapya wa Basketball Tanzania


Kwa hisani ya Michuzi Blog!
TBF Patron Chief Justice Augustino Ramadhani (centre, front row) in a souvenir photo with the newly elected Executive Commitee of the federation soon after their General Meeting held at the Courtyard hotel in Dar es salaam. To his right is the new TBF President Mussa Mziya and to his left is Vice President Phares Magesa


Tanzania Basketball Federation held their elections on 19th December, 2009, Dar Es Salaam. The New Committee will be in Power for the period of 4 years. The following were elected to take the office as of 19th December, 2009

1.PRESIDENT- MUSSA MZIYA
CELL +255 754 261 600, +255 715 261 600
EMAIL: mkmziya@yahoo.com, mkmziya@hq-tz.org

2.VICE PRESIDENT- PHARES MAGESA
CELL: +255 713 618 320
EMAIL: magesa@hotmail.com

3. SECRETARY GENERAL-ALEXANDER MSOFFE
CELL: +255 755 008 966
EMAIL: kadeghealex@yahoo.com


4.UNDER-SECRETARY – MICHAEL MALUWE
CELL: +255 717 053 876, +255 786 242 484
EMAIL: maluwe@yahoo.com

5.TREASURER – MARY MMBAGA
CELL: +255 754 307 075, +255 715 307 075
EMAIL: marymmbaga@hotmail.com

Thanking you in Advance
Lawrence Cheyo
Former Secretary – Tanzania Basketball Federation

Wednesday, December 23, 2009

Sakata zito la Kakobe na Tanesco!


Na Leon Bahati wa gazeti la Mwananchi

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe ameligomea Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitisha mbele ya kanisa lake njia ya umeme ya msongo mkubwa wa kilovolti 132.

Akofu huyo pamoja na mamia ya waumini wake, jana walikusanyika mbele ya kanisa hilo lililo kando ya Barabara ya Sam Nujoma karibu na Mwenge, jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kupambana baada ya kupata taarifa kwamba mafundi wa Tanesco wangewasili kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kupitisha njia hiyo ya umeme.

"Mimi nimejiandaa kuongoza waumini wangu katika kukabiliana na yeyote. Mimi nipo tayari kufa na nitahakikisha hawapitishi njia hiyo labda wawe wameniua," alilalamika.

Alilalamika kuwa iwapo umeme wa msongo huo utapitishwa eneo hilo utaathiri mitambo inayosaidia kunasa, kupaza na kurekodi sauti kwenye ibada zinazofanyika kanisani hapo pamoja na mpango wake wa kuanzisha kituo cha televisheni cha kanisa.

Isitoshe, alisema kwamba tayari Tanesco wamemuarifu kuwa itabidi wayang'oe mabango mawili ambayo yaligharimu Sh120 milioni ili kupisha mradi huo.

"Kama Watanzania haijatokea vita ya dini, basi ndiyo hii. Ni kubwa kuliko ile ya Wabarbeig," alisema Askofu Kakobe na kuitaka serikali iingilie kati suala hilo ili kuepusha dhahama inayoweza kutokea.

"Mimi na waumini wangu tumekubaliana tutakesha hapa usiku na mchana. Maana nasikia huwa wanaweza kuja usiku kubomoa mabango haya," alisema Askofu huyo mwenye maelfu ya waumini jijini Dar es Salaam.

Mwananchi lilipowasili jana eneo hilo ilikuta mamia ya waumini hao pamoja na Askofu Kakobe wakionekana kutokuwa na silaha yoyote lakini wakisisitiza kuwa wako tayari kwa vita dhidi ya mtu yeyote atakayefika eneo hilo kwa lengo la kung'oa mabango yao.

"Walifikiri kwa kuwa sisi ni walokole tutakaa kimya, lakini sisi tunasema katika hili hakuna cha kusema tutamwachia Mungu. Mungu yuko 'busy' (anakabiliwa na majukumu mengi) ana kazi nyingi, hili ni jukumu letu," alisema Askofu Kakobe.

Alilalamika kwamba utawala wa Rais Kikwete unalikandamiza kanisa lake huku akidai kuwa kama ingekuwa madhehebu mengine ya dini, kitendo kama hicho kisingetokea.

"Wanachokifanya hakina adabu! Kwa (askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp) Pengo isingekuwa rahisi. Wanamuonea Kakobe kwa kuwa ni mnyonge," alilalamika Kakobe akisema yuko tayari kufa ili mradi ahakikishe njia hiyo ya umeme haiwekwi karibu na kanisa lake.

Alibainisha kuwa awali njia hiyo ilikuwa ipite upande wa pili wa barabara mkabala na kanisa hilo, lakini wakazi wengi wa eneo hilo walipinga kitendo hicho hata pale walipoahidiwa kufidiwa.

"Hawa waliokataa, hata pale walipoahidiwa kufidiwa, wengi ni wasomi wa chuo kikuu. Eneo hilo ndilo lenye nafasi kubwa. Lakini wakaona upande huu hauna wasomi wanaweza kukubali kirahisirahisi tu.

Mimi katika hili nasema hapana," alisema Kakobe.

Kakobe alisisitiza kuwa yeye na waumini wake wameamua kuwa watakuwa wakikesha eneo hilo kuhakikisha watapambana na yeyote atakayefika kung'oa mabango yao.

Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alisema asingeweza kuwasiliana moja kwa moja na mwandishi wa Mwananchi lakini akaahidi kutuma taarifa ambayo hata hivyo haikujibu maswali ya msingi ambayo yanalalamikiwa na Askofu Kakobe.

Ingawa taarifa hiyo haikugusia sababu za Tanesco kutotumia upande wa barabara ambao una nafasi kubwa na badala yake kubanana na makazi ya watu upande ambao kanisa hilo lipo, alisema Tanesco imefanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kwamba njia hiyo ya umeme haiwezi kumuathiri binadamu wala mazingira yake.

Alieleza kuwa njia hiyo inapita kwenye eneo la hifadhi ya barabara na tayari wamepata kibali cha Wakala wa Barabara (Tanroads) kujenga njia hiyo ya umeme inayolenga kukidhi mahitaji ya umeme jijini ambayo yameongezeka kutokana na wingi wa shughuli za kibinadamu jijini.

Alisema mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Japani na unahusisha ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo 132kV kutoka Ubungo mpaka Makumbusho na kituo cha kupozea umeme Makumbusho.

"Shirika lingependa kuwataarifu wakazi wa maeneo hayo na wananchi kwa ujumla kuelewa kuwa hakuna madhara yoyote watakayopata wananchi wanaoishi na kupita maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme," alisema Badra na kuongeza:

"Shirika la umeme lilifanya utafiti wa kina na wa kitaalamu pamoja na wa kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa mradi huo na Baraza la Taifa za Mazingira (NEMC) lilijiridhisha na kuridhia kuwa ujenzi huo hautakuwa na matatizo au madhara yoyote kwa wakazi au wapita njia wa maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme."

Katika kufafanua namna njia hiyo itakavyojengwa ili wananchi wasidhurike, alisema nguzo zinazobeba umeme huo zinajengwa kwa urefu unaofuata viwango vya ujenzi wa msongo wa 132kV mijini ambavyo ni mita 23, akisema ndivyo vinavyokubalika kimataifa, na kuhakikisha usalama wa wakazi na wananchi katika maeneo hayo.

Vile vile alisema mikono inayoshika vikombe vya waya za umeme katika nguzo hizo vitaelekezwa upande wa barabarani kwa umbali wa mita tatu kutoka kwenye nguzo.

"œShirika lingependa wananchi waelewe kuwa ujenzi wa njia hiyo ya umeme wa namna hiyo katika maeneo ya mijini ni teknolojia inayoendelea kutumika sehemu nyingine duniani mfano, Japani," alisema.

Kijana mTanzania auawa na mwenzake-kisa Facebook!



KIJANA Mtanzania, Salum Kombo (18) ameuawa kwa kuchomwa kisu nchini Uingereza.

Rafiki wa kijana huyo ndiye aliyemchoma kisu baada ya malumbano waliyofanya kupitia mtandao wa kompyuta kwenye tovuti ya Facebook.

Kijana huyo alikuwa akisoma Sanaa katika chuo cha Tower Hamlets kilichopo London ya Mashariki.

Kombo aliaga dunia baada ya kuchomwa kisu mara kadhaa kifuani na shingoni akiwa karibu na nyumbani kwao.

Imedaiwa kuwa mtu aliyemchoma kisu ni rafiki yake mkubwa na amefanya hivyo baada ya Salum kumtumia taarifa iliyomkera wakati akijibu hoja yake baada ya kukataliwa kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na akina Kombo.

Kombo alichomwa kisu hicho Jumapili kiasi cha yadi 400 kutoka makazi ya shangazi yake ambaye ndiye alikuwa akimlea.

Imedaiwa kuwa, kijana mwingine baada ya kukasirishwa na ujumbe huo alimfuata Salum akijifanya hakuna tatizo kati yao na kabla ya kumchoma kisu huku akiwa anamkumbatia.

Kombo aliwasili nchini Uingereza akitokea Tanzania miaka saba iliyopita na alikuwa akiishi na shangazi yake huko Bow, London ya Mashariki.

Majirani wa akina Kombo wamedai kuwa, kabla ya kijana huyo kuchomwa kisu alikuwa akiimba nyimbo za Krismasi na wenzake.

Imeelezwa kuwa hali ya shangazi yake Salum si nzuri baada ya taarifa za kifo cha kijana wake.

Gary Byrne, 46, alisema alikuwa anaona jinsi uhai unavyomtoka kijana huyo taratibu dakika chache kabla ya watu wa huduma ya kwanza kufika na kumsaidia.

Kijana huyo alipoteza maisha dakika 20 tu baada ya kuanza kupewa huduma ya kwanza.

Kijana huyo alipata majeraha makubwa katika kifua na shingoni. Haya ni mauaji ya 13 kutokea kwa vijana katika jiji la London mwaka huu.

Polisi wanamshikilia kijana aliyehusika na mauaji hayo na walikuwa wanatarajia kumfikisha mahakama ya Thames jana

Kwa maelezo ya Kiingereza kopi hii link hapa chini ui paste ktk address bar then gonga enter key.

http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/2781029/Facebook-insult-led-to-killing-in-the-street.html#ixzz0aP7d8QHr

Tuesday, December 15, 2009

Du hii kali-Ukikwama kuelewa omba msaada wa tafsiri!

Two couples were playing cards. Jeff accidentally
dropped some cards on the floor. When he bent down under the
table to pick them up, he noticed that Dave's wife,
Sandy, was not wearing any underwear! Shocked by this, Jeff
hit his head on the table and emerged red-faced.

Later when Jeff went to the kitchen to get some refreshments, Sandy followed him and asked,
"Did you see anything under the table that you liked?" Jeff admitted, "Well, yes I did."
She said "you can have it, but it will cost you $100." After a minute or two, Jeff indicates that he is interested.

She told him that since Dave goes to work on Friday afternoons and Jeff doesn't, then Jeff should come to their house
around 2:00 PM on Friday.

Friday came and Jeff went to her house at 2:00 PM. After paying her the
$100, they went to the bedroom, and had strong and enjoyable sex for a few hours and
then Jeff left.


Dave came home about 6:00 PM and asked his wife, "Did Jeff come by
this afternoon?" Totally shocked, Sandy replied,
"Yes, he did stopby for a few minutes." Next, Dave
asked, "Did Jeff give you $100?" Sandy thought,
'Oh hell, he knows!' Reluctantly she said,
"Yes, he did give me $100.."

"Good" Dave says. "Jeff came by the office this morning and
borrowed the $100 from me and said that he'd stopby our
house on his way home and pay me back.
My friend It's so good to have a friend you can
trust!!
Niambie mke wa Dave alijisikiaje?

Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex msama akizungumza na mchungaji
Mama Getrude Lwakatare kwenye moja ya tamasha la Msama Promotions hivi karibuni

KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, imeandaa tamasha la kimataifa la nyimbo za injili, litakalofanyika Desemba 25, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama,amesema kuwa tamasha hilo ni tamasha litakalowaunganisha waimbaji kutoka nchi za Kenya, Malawi, Uganda, Burundi Zambia na Afrika Kusini. Alisema, lengo la tamasha hilo ni kusaidia watu wenye ulemavu na yatima na wengine wenye mahitaji ambao wanapaswa kusaidiwa katika jamii.

“Ujue kuna baadhi ya watu wenye ulemavu ambao wanahitaji misaada mbalimbali, kwa mfano baiskeli, hivyo kampuni yangu imeliona hilo, hivyo tumepanga kuelekeza nguvu kwa walemavu wa mikoani,” alisema Msama na kuongeza. Fikiria kuna wengine wanatamani kusoma, lakini kwa kukosa usafiri na huduma nyingine muhimu, wanashindwa, hivyo tumeona ni vizuri kama tutawakumbuka,” alisema Msama.

Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili akiwa mwasisi wa matamasha ya injili, alisema katika tamasha hilo, pia kutakuwa na waimbaji wapya walioingia katika albamu ya Haleluya Collections Volume 5, wakiwamo kutoka Tanzania. Msama alisema kamati hiyo imeamua kufanya matamasha mara mbili kwa mwaka ikiwa ni kufanyia kazi maoni ya wapenzi na mashabiki wa muziki huo.

Kuhusu misaada kwa makundi mbalimbali ya kijamii, Msama alisema kamati yake imekuwa ikifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kusaidia wenye mahitaji katika jamii. Alisema, kamati hiyo imekuwa ikimuomba Mungu azidi kuijalia uwezo kwani lengo ni kugawa baiskeli 100 kila mwaka badala ya 70, ilizowahi kugawa na kusomesha yatima. Mbali ya baiskeli, kamati hiyo imewahi kutoa vitanda vya wagonjwa katika hospitali mbalimbali nchini ingawa kwa kipindi hicho hawakuwa wakitangaza hadi pale waliposhauriwa kufanya hivyo.

Alisema kuanzia sasa, watakuwa wakitangaza hata mapato katika matamasha mbalimbali ili kuwa wazi zaidi, kwani hiyo pia itawajengea imani zaidi kwa jamii. Aidha, Msama ametoa wito kwa watu mbalimbali katika jamii kuguswa na suala hilo, kwani linalenga kusaidia makundi maalumu katika jamii. Sambamba na hilo, Msama ametoa wito pia kwa jamii kuunga mkono juhudi za kamati hiyo kwa kununua albamu ya Haleluya Volume 5 iliyoko madukani.

Tuesday, December 8, 2009

Miaka 48 ya Uhuru wa TANGANYIKA sio Tanzania


Kikosi cha askari wa kutuliza ghasia-Field Force Unit a.k.a Fanya Fujo Uone kikipita mbele ya Amiri Jeshi mkuu kwa heshima katika mwendo wa haraka.

Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya Tanzania, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride katika sherehe ya miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika zilizofanyika jana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

Mama na wanawe!


Arusha baridi,bila kuvaa mtindo huu utakimbia mji hasa kuanzia mwezi wa tano (May) mwishoni hadi wa nane (August) hivi.

Mshiriki wa Miss Utalii kinondoni atimuliwa baada ya kubainika kuwa na mtoto


Mshiriki wa Miss Utalii Kinondoni 2009- Christina Masandeko (pichani juu), amefukuzwa katika kambi ya Washiriki kutokana na kuwa na Mtoto ikiwa ni pamoja na kuwa Ameolewa na hadi sasa anakaa na mume wake katika maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imefuatia kutoakana na Kanuni za Mashindano hayo kutoruhusu Mshiriki kuwa na Mtoto ama kuwa na Ujauzito,

kutokana na Uchunguzi uliopatikana kutoka kwenye Vyanzo vya Washiriki, Mrembo huyo alikuwa akishiriki kwa kificho lakini hata hivyo hakuna siri Duniani na hivyo aliweza kubainika wakati washiriki wenzake walipokuwa wakifanya Utafiti baada ya kuwepo na fununu kuhusiana na suala hilo.

Kambi ya Washiriki Miss Utalii Kinondoni inaendelea katika Ukumbi wa New Msasani Klabu, chini ya Mwalimu wao Miss Utalii Iringa 2005 Ester Kinyunyi, ambapo jumla ya washiriki KUMI TANO wapo katika Ushindani Mkali kutokama na wote kuwa na sifa za kuwa washindi.

Fainala Miss Utalii Kinondoni zimepangwa kufanyika Tarehe 11 katika Ukumbi wa New Msasani Klabu, ambapo Wasanii wa kizazi kipya kwa kushirikiana na Vikundi vya Ngoma za Asili watasindikiza Onyesho hilo sambamba na Kundi la Vaibration Sound, ikiwa ni pamoja na TID, Abubakari Msasu(KIBOOT), Diamond,

kwa Upande wa Vikundi vya Ngoma watakaosindikiza Onyesho hilo ni Irene Sanga na kundi lake, Mandela Theatre chini ya Mzee Jangala, Mfalme Band chini ya Costa Siboka, Black Wariours, Makumbusho Dancing, ambapo onyesho limepangwa kuanza majira ya saa tatu na nusu Usiku.

Wadhamini waliojitokeza kusaidia shindano hilo ni pamoja na Mine De Copper, Fom Com International, Empire Furniture, A-one Tours & Safaris, Aucland Tours & Safaris, Aurora Security, Mashujaa Pub & Intertainment, Mamaa Sakina Trans, Ele-Tech & Lighting Agency, Regency Hotel, The Grand Villa Hotel, Clouds Fm, Prime Time Promotions, Kitangoma Magazine, Michuzi Bloggs, Mlonge By Makai Interprisess, Cm Motors, Mh.Idd Azan Mbunge, Billionea Club, Dage Saloon, Al Water Well Drilers,Rose Gaden Restaurant, B-kule Records, Tom Diamond,Ambiance Club,Varry Spring, Ngorongoro Crater,Tanga Beach Resort na Tanapa.

Jinsi ya kuhakikisha juhudi zako zinatambulika kazini


KAMA wewe ni kijana mdogo na ndio kwanza umeajiriwa, kwa vyovyote vile utapata ugumu unapotaka kujenga jina lako kazini kwako na kutambuliwa kwa mchango wako. Pengine
changamoto kubwa ni kujitambulisha bila kuonekana kama vile unajidai au una mmajvuno.

Iwapo mara kwa mara utasikika ukijisema jinsi ulivyo maridadi, jinsi unavyoiweza kazi yako na jinsi shirika au kampuni yako ilivyo na bahati kwa kuwa na wewe
utachukuliwa kuwa mtu wa majigambo na kujiinua. Namna hii utapuuzwa.

Lakini pia ukikaa kimya kabisa unaweza kujikosesha fursa ya kupewa majukumu fulani ya kukujengea jina. Hushauriwi kujipigia debe kwa maneno na kwa kujipendekeza kwa
mabosi, lakini angalau uchukue jitihada za kuwaonesha watu wanaokuzunguka kuwa unao mchango muhimu katika eneo lako la kazi. Zipo mbinu ambazo ukizitumia vema zitakusaidia.

Fahamu lengo lako

Kabla ya kuanza kujipigia tarumbeta na kuimba sifa zako mwenyewe kazini, jiulize lengo lako la kufanya kazi kwa bidii ni nini hasa. Je, kuna mtu unataka kuchukua nafasi yake? Je, unataka mtu fulani akuone unavyowajibika? Je, unataka kuwafurahisha wakubwa wa kampuni?

Kama hujui hatimaye unataka jitihada zako zikufikishe wapi, haitakuwa rahisi kufahamu kama uko katika njia sahihi au kama umefika. Lakini ili ufanikiwe, hakikisha kuwa lengo lako la kujiboresha linakwenda sanjari na malengo ya shirika
lako, pamoja na malengo maalumu ya idara au kitengo chako.

Hakikisha una mafanikio yanayopimika

Ili uweze kuwa na ujasiri wa kujisifia – kama ni lazima kufanya hivyo – hakikisha kwanza unalo jambo la kujisifia kwalo, maana huwezi kujisifu bila sababu. Hakikisha unacho kitu maalumu ulichofanikiwa kukifanya na kiwe kinapimika.

Katika kazi, kama kitu unachokiita mafanikio huwezi kukipima basi hoji uhalali wa kukiita kitu hicho mafanikio. Kadiri itakavyowezekana, hakikisha unapojisifia uwe na jambo maalumu ambalo mtu akikuuliza unajisifu kwa lipi uweze kumwonesha, na liwe linapimika.

Lenga zaidi mambo makubwa

Unapokuwa na mawazo mafupi utajikita zaidi katika mambo madogo madogo. Kama utakuwa mtu wa kujitapa kwa mambo madogo madogo utakuwa kichekesho na kila mmoja atajua
unayoyaweza ni hayo madogo. Zaidi ya hapo, hakuna mtu atakayeona jipya kwako.

Mafanikio madogo yaweke moyoni mwako – watu watayaona tu hata usiposema. Badala yake, weka msisitizo katika mambo makubwa, mathalani mambo ambayo kila mtu anayafikiria na yanamtia hofu. Kuna jambo ambalo ukilifanya kila mtu atakuona shujaa, jitahidi kulifanya hilo.

Sifa zako zifanye za kampuni

Unapofanikisha jambo, lazima tu utajisikia vema na unaweza hata kujivuna. Hata hivyo, iwapo utajaribu kuonesha kuwa mafanikio ya kampuni/shirika umeyaleta wewe utalitia tembo maji, maana watu wengine wote hawatakuunga mkono, kwani yamkini nao watajiona wanafanya kazi, si kucheza.

Kwa hiyo, badala ya kutembea ukijitangaza kuwa wewe ndiwe kinara wa kampuni/shirika, ashiria tu kwamba mafanikio yaliyopatikana ni ya shirika zima na yameletwa kwa
ushirikiano wa wadau wote.

Kwa kufanya hivi, mbali na kwamba watu watatambua kuwa ni wewe uliyefanikisha jambo husika, lakini pia watakuona jinsi ulivyo muungwana kwa kutopenda kujisifia.

Usikubali kukatishwa tamaa

Kuna wakati ambapo utajiona kana kwamba huna maana, mathalani bosi wako anapokupuuza au kukataa pendekezo lako. Lakini wakati mwingine bosi wako anaweza kuwa tu ametingwa na hakumaanisha kukupuuza.

Kumbuka hata kama bosi wako ni mkubwa kiasi gani na yeye anao watu anaowajibika kwao, huku pia akiwa na kazi zake, halafu pia akitakiwa kukusikiliza wewe na wengine
walio chini yake. Siku moja ukifika ngazi ya menejimenti utaelewa.

Kwa hiyo, usijisikie vibaya iwapo bosi ataonekana kutokusikiliza vizuri. Badala ya kuvunjika moyo, endelea kushirikiana na bosi wako na hakika mchango wako utabainika siku muafaka ikifika.

Watu husema raha mtu hujipa mwenyewe. Kazini kwako wewe ndiwe mtu wa kwanza kujitakia heri na mafanikio na kwa hiyo lazima ufanye jitihada za kulitangaza jina lako kwa mustakabali mwema wa maisha yako. Isipokuwa tu utapaswa kuwa makini, maana ukijiinua mwenyewe utashushwa.

Isipokuwa tu kwa kuendelea kuwa mwaminifu kwa wakubwa
zako, huku ukiyachukulia mafanikio yako kuwa mafanikio ya kampuni, utaonekana na kutambuliwa zaidi.

Mtuhumiwa mauaji abambwa kavaa baibui

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

MWANAFUNZI mmoja wa Shule ya Sekondari anayetuhumiwa kufanya mauaji mkoani Mwanza na kutorokea Shinyanga
amekamatwa na akiwa amevaa mavazi ya kike aina ya baibui akiwa katika harakati za kutoroka.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Daudi Siasi amemtaja mwanafunzi aliyekamatwa kuwa ni Daudi Rashidi (18) ambaye pia hutumia jina la Athumani Rashidi
anayetuhumiwa kumuua mwanafunzi mwenzake jijini Mwanza wiki iliyopita.

Kamanda Siasi alisema mbali ya mwanafunzi huyo ambaye alikamatwa juzi katika kituo kikuu cha mabasi mjini Shinyanga, polisi iliwakamata watu wengine watatu
wanaodaiwa kushiriki katika mauaji hayo.

Wengine waliokamatwa ni Nixon Robert (18), pia mwanafunzi wa sekondari anayetuhumiwa kushiriki kumpiga mwanafunzi aliyekufa, Bw. Ally Rashid (40) mfanyabiashara wa Mtaa wa Rufiji mjini Mwanza ambaye anadaiwa kuwatorosha wanafunzi hao na Bi. Margaret George (25) mkazi wa Ndembezi, Shinyanga aliyekuwa awapatie hifadhi.

Mtuhumiwa Daudi alishtukiwa na abiria wenzake aliokuwa nao katika basi hilo kutokana na sauti yake kuwa ya kiume
wakati mavazi aliyokuwa amevaa ni ya kike ikiwa ni baibui nyeusi iliyokuwa imeficha uso wake wote na kuachia uwazi kidogo katika sehemu ya macho na hivyo kutoa taarifa polisi.

"Baada ya kuwakamata tuliwasiliana na wenzetu wa Mwanza ambao baada ya kuwatajia majina ya Daud na Nixon waliwatambua kuwa ndiyo wanaowatafuta kuhusiana na kesi ya
mwanafunzi wa sekondari aliyeuawa kwa kipigo na sasa
tunaandaa mipango ili kuwarejesha Mwanza kujibu shtaka la mauaji," alieleza Kamanda Siasi.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema kuwa polisi walikuwa na taarifa za siri zilizotolewa na raia wema mkoani Mwanza, kwamba wanafunzi hao na mtu anayewasaidia kuwaficha wametorokea Shinyanga.

Kutokana na taarifa hizo na raia walimshtukia mmoja wa watuhumiwa polisi walifanikiwa kuwanasa wakati wakiteremka kwenye basi la Kampuni ya Mohamed Trans mjini Shinyanga.

Jamani Didier Drogba na timu yake ya Taifa wanatua Bongo Laiv bila chenga!


Timu ya taifa ya Ivory Coast ina mpango wa kuweka kambi jijini Dar kwa maandalizi ya kombe la mataifa ya afrika huko Angola mwakani. hivyo wadau tukae mkao wa kula wa kumuona Didier Drogba na wenzie.

Rais wa TFF Leodegar Chilla Tenga kawaambia waandishi wa habari sasa hivi kwamba Ivory Coast watatua Dar January 2, 2010 na kucheza mechi mbili. ya kwanza kasema itakuwa January 4 na ya pili January 7, na timu ya taifa - Taifa Stars.

tayari ujumbe mzito wa toka nchi hiyo upo Dar kwa maandalizi ya awali na hivi sasa upo hoteli ya New Africa kuongea na waandishi wa habari.

ujumbe huo ambao ni makamu wa kwanza wa rais wa chama chama cha soka cha huko, Idris Diallo, katibu mkuu wake pamoja na kocha wao, Vahid Halilhodzic, wameshatembelea hoteli kadhaa na pia uwanja mpya wa neshno na wameonesha kuridhika. ila wametoa rai kwamba uwanja wa gymkhana ambao watafanya mazoezi mepesi urekebishwe..

Ikumbukwe Ivory Coast imefuzu kucheza kombe loa dunia sauzi na mechi yao ya kwanza wanapiga na Ureno June 20, 2010 kabla ya kuivaa Brazil Juni 25 na kumalizia na Korea Kaskazini katika mzunguko wa kwanza.

Haya mnaotaka kazi kwenye NDEGE mchongo huu hapa, msilaze damu!!


INTERNATIONAL FLIGHT ATTENDENT/CABIN CREW JOB.

MT GlobalExperts is an international online Recruitment Agency in collaboration of emott solutions ltd of Tanzania are specializing in supporting airlines and organizing Cabin Crew Recruiting Days world-wide.

We work with a wide variety of airlines and aim to offer Cabin Crew a simple method of finding good employment in the aviation industry.

Our Cabin Crew Recruiting Days also offer Cabin Crew the opportunity to meet airline personnel and ask as many questions as they want.

If your initial application is accepted, our local agent will invite you for a Pre-selection days in our chosen venue. Please note that if you are not from the country where we organize pre-selection we will not provide any visa assistance for you to enter the country!
Recruiting Campaign in Tanzania will be:
23 december.2009 - Pre-selection Day (hotel blue pearl ubungo)
27 december. 2009 - Screening day
28-29 december.2009 - Individual Interviews

Please contact below address for more details;-

Emott solutions ltd
P.o.box 504
Dar es Salaam,
Tanzania

Mob; 0754663399/ 0713687539/0713154900
Email; info.emott@gmail.com

Deadline for submission;- 21st December 2009.
MT GlobalExperts also organize together with local partner emott solutions ltd in-house selection days so that we can highlight the most outstanding candidates and pass on your details to our various airline clients.
We have numerous candidates and thus each is expected to arrange and pay their own expenses. We will not be able to provide any compensation for these expenses

Friday, December 4, 2009

Wanafunzi wa Cisco Networking (CCNA) komaeni msiache kozi


Hosea Lotashu (kushoto) na Frank Mdoe (kulia) nao nawakubali sana katika hii fani

Hawa ni Clara Mwakyoma (kushoto) na Chrstina Thadey (mwenye pozi la kuinama)

Hawa nao ni Amne (Mtaalam wa mahela), katikati ni Hosea Lotashu na kulia ni Oscar Lusako, mambo si mchezo

Hapa wanaonekana wanafunzi hao wa session 5 saa 11 jioni. Kushoto ni Njikalia Mrema, kulia ni Hamisi Majaliwa na nyuma ni Christian Kavishe.

Thursday, December 3, 2009

Tujikumbushe!




Ni mambo gani mazuri unayokumbuka ambayo mtu huyo hapo juu kakufanyia wewe na nchi yako?

JK ndani ya Cuba

Rais Jakaya Kikwete akiwa ziarani Cuba. Hapa yupo na Rais Raul Castro mdogo wake na Rais aliyepita Fidel Castro.
Wadau mtindo wa kupeana madaraka uliotokea Cuba nyie mwauonaje?
Ndio mzuri kwa ajili ya kuimarisha amani na utulivu katika nchi au ni utawala wa kuikoo zaidi?

Sky Scrapper-Arusha


Hata Arusha tunavyo vikwangua anga kama hicho hapo juu, tatizo ni kusimama kwa ujenzi sijui pesa zimeisha au ....
Wadau jengo hili likiisha mji wetu (sio jiji) utapendeza sana.

Nawatakia Likizo Njema


Enyi wanafunzi wetu wa Certificate in Computing and Information Technology, najua mnafurahia likizo yenu. Sisis tunaendeleza kazi tukiwasubiri kwa semester ya pili.
Nawatakia Likizo Njema, Karibuni tena!!!!!

Katika picha wanaonekana baadhi ya wanafunzi hao wakati wakijiandaa na mitihani ya Semester November 2009.