Wednesday, October 27, 2010

Tariq Aziz ahukumiwa kunyongwa

ALIYEKUWA msaidizi mkuu wa kimataifa wa utawala wa Saddam Hussein nchini Iraq, Tariq Aziz, leo amehukumiwa kunyongwa kwa ajili ya kuendesha manyanyaso dhidi ya waumini wa madhehebu ya Shia nchini humo Tukio hilo limekuja baada ya miezi mitatu tu baada ya Wamarekani kumsalimisha mtu huyo kwa serikali ya Iraq.

Msemaji wa Mahakama Kuu ya Iraq, Mohammed Abdul-Sahib, hakutaja ni wapi mtu huyo mwenye umri wa miaka 74 ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje angenyongewa. Hata hivyo, Aziz amepewa siku 30 za kukata rufaa.

Aziz, ambaye alikuwa Mkristo pekee miongoni mwa washirika wakuu wa Saddam ambaye alikuwa mfuasi wa madhehebu ya Sunni, alikuwa amevaa suti ya bluu wakati akiwa amekaa peke yake mahakamani akiwa ameinama.

Mwanasheria wake kutoka Jordan, Badee Izzat Aref, aliishutumu serikali kwa kumbambikia tuhuma hizo ili kupotosha nadhari ya umma kuhusu kufichuliwa hivi karibuni kwa manyanyaso wanayofanyiwa wafungwa na majeshi ya Iraq kwa mujibu wa hati za jeshi la Marekani zilizotolewa wiki iliyopita na taasisi ya WikiLeaks.

“Tunalijadili suala hili na hatua za kuchukua,” Aref aliliambia shirika la habari la The Associated Press mjini Amman, nji mkuu wa Jordanian na kuongeza kwamba "hukumu hii si ya haki na ilikuwa na madhumuni ya kisiasa."

Azizi alifahamika kimataifa kama mtetezi wa utawala wa Saddam nchini humo na mpinzani mkuu wa Marekani hususani alipokuwa waziri wa mambo ya nje baada ya uvamizi wa Iraq nchini Kuwait mwaka 1990 na baadaye kuwa makamu wa waziri mkuu. Mkutano wake na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, James A. Baker, mjini Geneva, Januari 1991 ulishindwa kuzuia kuzuka kwa Vita vya Ghuba.

Azizi pia alikutana na Papa John Paul wa Pili huko Vatican wiki kadhaa kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani mnamo Machi 2003, katika juhudi zake za kuepusha vita hivyo.Habari kwa hisan ya GPL

Wednesday, October 13, 2010

Klabu ya Manchester United yadaiwa paundi milioni 80


Klabu ya Manchester United imearifiwa inadaiwa paundi milioni 79.6 za Uingereza hii ni kabla ya kukatwa kodi, ikiwa ni mzozo mkubwa wa kifedha kuikumba klabu, hiyo hali iliyosababisha kupungukiwa na fedha za mauzo ya wachezaji.

Deni hili ni la miezi 12 hadi mwezi wa Juni, ikilinganishwa na faida ya paundi milioni 48 kwa mwaka uliopita, ambapo mapato yaliongezeka baada ya kumuuza mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo kwa paundi milioni 80.

Madeni yote kwa ujumla ya klabu hiyo kwa mwaka uliopita yalifikia dola milioni 67. Pia klabu hiyo ililipa riba ya paundi milioni 40.

Wakati watu nao walipungua kuingia uwanjani kwa mechi, hali iliyozidisha kuporomosha mapato ya kibiashara ya klabu.

Kwa ujumla mapato halisi ya Manchester United kwa mwaka yaliongezeka kwa paundi milioni 286.4.

Malipo ya riba ya paundi milioni 40 yaliyofanywa yalikuwa sawa na malipo ya mwaka uliopita.

Faida itokanayo na uendeshaji, ambayo haijumuishi gharama za madeni yaliyotokana na huduma, pia imepanda, na kufikia paundi milioni 100.8, ikilinganishwa na paundi milioni 92 kwa mwaka uliotangulia.

Manchester United ilinunuliwa na familia ya akina Glazer ya Marekani kwa dola milioni 800 mwaka 2005.

Mashabiki wanaoipinga wanadai familia hiyo imeitumbukiza klabu hiyo katika deni kubwa, hali iliyosababisha kuwepo na maandamano.

Mashabiki wengi wanaendelea kususia kuvaa fulana za klabu hiyo za rangi nyekundu pamoja skafu na badala yake wameamua kuvaa fulana za rangi ya kijani na dhahabu, ambazo ndio rangi za asili za Newton Heath, klabu iliyoanzishwa mwaka 1878 iliyokuwa an wachezaji wasio wa kulipwa ambayo baadae iligeuka na kuwa Manchester United

Mkuu wa waasi Rwanda akamatwa nchini Ufaransa




Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ilisema kiongozi wa kundi la FDLR la Rwanda alikamatwa nchini Ufaransa kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Katika hati ambayo ni siri, Callixte Mbarushimana (Pichani juu) anashutumiwa kwa makosa 11 ya mauaji, ubakaji na uhalifu mwengine uliofanywa wakati wa ghasia za muda mrefu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwaka jana aliiambia BBC kwamba alikana kuhusika na uhalifu wa kivita na wapiganaji wa FDLR hawakuwashambulia raia.

Wapiganaji wa FDLR hivi karibuni walishutumiwa kuwabaka mamia ya watu huko Congo.

Wakati huo huo, walio wengi Wahutu wa FDLR (Democratic Forces for the Liberation of Rwanda) walikana kuhusika na mashambulio katika mji wa Luvungi mashariki mwa Congo.

Baadhi ya viongozi wa FDLR wameshutumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa kati Rwanda.

Baada ya kundi la Watutsi walio wengi kuidhibiti Rwanda, walikimbilia kwa ambapo kwa sasa kunajulikana kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusababisha ghasia kwa miaka mingi eneo hilo.

Jela ni mbaya, Mzee Mandela asimulia manyanyaso!


Barua zilizoandikwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela wakati alipokuwa miaka 27 gerezani zinaeleza maumivu makali aliyokuwa akiyasikia alipotenganishwa na familia yake.

Dondoo za barua hizo, zitakozoanza kuuzwa siku ya Jumanne, zinaonyesha jinsi alivyokuwa tafrani wakati mke na watoto wake walipokuwa wakisumbuliwa na serikali ya ubaguzi wa rangi.

Alimwambia Winnie Mandela alipotumikia kifungo cha miezi 18 alipotengwa na kufungiwa katika chumba cha peke yake, " Najihisi nimelowanishwa kwenye kidonda."

Katika barua kwa watoto wake aliandika, "Kwa muda mrefu mnaweza kuishi kama yatima."

Nelson Mandela

Nakala za barua nyingi zilikuwa zikiandikwa katika madafatri ambayo yalitaifishwa na serikali.

Hatimaye zilirejeshwa kwake na aliyekuwa askari wa usalama mwaka 2004.

Mwandishi wa kujitegemea anaelezea namna mume na mke, wanavyojaribu kushikilia familia yao pamoja huku kukiwa na mtikisiko mkubwa wa kisiasa na hisia.

Mwaka 1969, aliwaandikia mabinti zake wawili, Zeni na Zindzi wenye umri wa miaka tisa na 10, wakati wote wawili yeye na mkewe wakiwa gerezani.

Aliwaambia, " Sasa hamtosherehekea siku za kuzaliwa wala Krismasi, hamna zawadi au magauni mapya hamna viatu wala vidude vya kuchezea watoto."

Katika mwaka huo huo, alizuiwa kuhudhuria mazishi ya Thembi, mtoto mkubwa wa kiume miongoni mwa watoto wake wawili katika ndoa ya mwanzo, aliyefariki dunia kwenye ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 24.

Aliandika, " Nilipoambiwa kwa mara ya kwanza kuhusu kifo cha mwanangu nilitikisika tangu juu mpaka chini."

Barua kwa Winnie Mandela mwezi Agosti 1970 inaonyesya hasira kutokana na misukosuko inayoikumba familia yake.
Uhusiano uliojaa wasiwasi

Barua hizo pia zinaonyesha uhusiano wake na Winnie Mandela. Mwaka 1976 aliandika kwamba tatizo lake kubwa ni "kulala bila wewe kuwa pembeni mwangu na kuamka bila wewe kuwa karibu yangu, kupita siku bila mimi kukuona wewe."

Wakati huo, alipandishwa cheo na chama cha African National Congress kama ishara ya ya kupambana kwake na ubaguzi wa rangi. Lakini katika miaka ya kati ya 80 matendo yake yaliongezeka kuwa na utata na uhusiano wao ulianza kuleta wasiwasi.

Nelson na Winnie Mandela

Mwaka 1987, aliandika kwa rafiki yake kuhusu hasira aliyoonyesha Winnie Mandela alipomwambia namna watoto wake wawili wa kike walivyokuwa wakubwa: "Alinikumbusha:Mimi, si wewe, ndiye niliyewakuza hawa watoto ambao sasa unanileza mimi. Nilishtushwa."

Japokuwa alitembea naye sambamba alipoachiwa huru mwaka 1990, walitengana mwaka 1992 na kuachana miaka minne ijayo.

Aya kutoka barua hizo zimetolewa kwenye gazeti la Uingereza, The Sunday Times, na katika magazeti ya Afrika Kusini.

Zimechapishwa kwenye kitabu, Mazungumzo na Nafsi yangu, inayojumuisha hifadhi za nyaraka za kumbukumbu na vitu alivyorekodi mwenyewe pamoja na barua.

Kutoka dondoo moja kwenye kitabu hicho, ni wazi kuwa Bw Mandela alianza kuwa mwangalifu kutokana na kuongezeka kwa heshima yake katika nyanja za kimataifa wakati alipokuwa gerezani katika kisiwa cha Robben.

"Jambo moja ambalo lilikuwa likinitia wasiwasi mno ni sura isiyo sahihi nilioiweka bila kujua kwa ulimwengu wa nje; wa kuonekana kama mtakatifu.

Monday, October 11, 2010

HEBU MSIKILIZE HUYU DADA, ILA USIMHUKUMU YEYOTE!!


Na Musa Mateja wa GPL
Mwanadada anayetisha kunako tasnia ya filmu Bongo, Shamsa Ford (pICHANI jUU)ametoa kali baada ya kuweka wazi kuwa katika maisha yake hajawahi kulala na mwanaume katika nyumba ya kulala wageni ‘gesti’, Amani haliachi kitu.

Shamsa ambaye ametunuku penzi lake kwa jamaa mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Dick wa Mikocheni Dar na kumwacha njia panda mchumba wake mjamaika, aliyasema hayo alipokuwa akigonga ‘spesho intavyu’ na Amani ndani ya Bilicanas Club, Posta, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Huwezi amini, katika safari yangu ya mapenzi sijawahi kulala gesti na mwanaume, mara nyingi jamaa niliowahi ‘kutoka’ nao walikuwa wakinimpeleka kwenye ‘mageto’ yao,” alisema Shamsa.

Shamsa aliendelea kutambaa na mistari kwa kudai kwamba, amekuwa akijitahidi kumshawishi mwanaume anayemtaka kwenda naye sehemu yoyote kuvunja amri ya sita kwa sharti moja tu, siyo gesti.

Alisema: “Katika vitu ninavyochukia ni pamoja na kuona mtu akinishauri kuminya naye gesti.”

Thursday, October 7, 2010

TANZANIA YASEMA-TUNAUWEZO WA KUHIFADHI NYARAKA ZA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA RWANDA


(Pichani juu)NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, BALOZI SEIF IDDI, AKIZUNGUMZA WAKATI WA MKUTANO WA BARAZA KUU LA 65 LA UMOJA WA MATAIFA ULIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI, MKUTANO HUO ULIPOKEA NA KUJADILI TAARIFA ZA MAHAKAMA ZA KIMATAIFA ZA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA(ICTR) NA MAUAJI YA HALAIKI YA ILIYOKUWA YUGOSLAVIA YA ZAMANI (ICTY). KATIKA MKUTANO HUO PAMOJA NA MAMBO MENGINE NAIBU WAZIRI ALISISITIZA NIA NA UTAYARI WA TANZANIA WA KUHIFADHI NYARAKA NA KUMBUKMBUKU MUHIMU ZA MAHAKAMA HIYO BAADA YA KUMALIZA KAZI ZAKE.


NA MWANDISHI MAALUM

NEW YORK-Wakati Marais wa Mahakama za Kimataifa za Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda(ICTR) na ile ya mauaji ya halaiki ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani (ICTY0, wakilalalamikia uhaba wa fedha na wataalamu. Tanzania imeiambia tena Umoja wa Mataifa kwamba inayo nia na uwezo wa kuhifadhi nyaraka na kumbumbuku za Mahakama ya kimataifa ya Rwanda.

“Kama tulijitolea kuikaribisha mahakama hiyo katika ardhi yetu, kama tulitoa ushirikiano wa hali na mali kwa mahakama hiyo, kama tulitimiza wajibu wetu wa kimataifa na kitaifa katika kufanikisha utendaji kazi wa mahakama hiyo, hapana shaka kwamba hata uwezo na raslimali za kuzihifadhi kumbukumbu hizo tunao”.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Iddi, katika mkutano wa Baraza Kuu la 65 la Umoja wa Mataifa, lilipokutana mwishoni mwa wiki, kupokea na kujadili taarifa kuhusu utendaji kazi wa mahakama hizo mbili.

Naibu Waziri Seif Iddi, akaueleza mkutano huo, kwamba, wakati utendaji kazi wa mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, ikikaribia ukingoni mwa kukamilisha kazi zake, Tanzania imekuwa ikifuatilia kwa karibu sana maamuzi ya kikao cha kazi cha Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuhusu uhifadhi wa nyaraka na kumbukumbu muhimu za makahama hiyo.

“Na kwa sababu hiyo serikali ya Tanzania inaamini kuwa nyaraka nyeti zinazoihusu mahakama hiyo, lazima zitunzwe mahali salama, penye amani na mazingira ambayo yataruhusu na kutoa fursa kwa UN, mamlaka au mtu atakayeruhusiwa kuzipata nayaraka hizo bila ya vikwazo au pingamizi, wasi wasi wa usalama au tatizo la kisiasa” akasisitiza Naibu Waziri

Akaongeza “ Tanzania iko tayari kuendelea kuzihifadhi nyaraka hizo na kumbukumbu zote kwa moyo mmoja kama ambavyo tumekuwa katika kipindi chote tangu kuanza kazi kwa mahakama hiyo. Tunaamini kwa nguvu zote kwamba miundombinu imara ya kutunzia nyaraka na kumbumbu hizo muhimu kwa vizazi vijavyo tayari ipo”.

Akizungumzia utendaji kazi wa Mahakama hizo mbili, Naibu Waziri, amesema hapana shaka kwamba mahakama hizo zimefanya kazi nzuri na iliyotukuka nakwamba zinapaswa kupongezwa na kila mtu.

“ Ningepeda kutoa shukrani zangu kwa mahakama hizo kwa kuweza kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria watuhumiwa wote. Lakini ninapenda kuunga mkono ombi lililotolewa na marais wa Mahakama hizo la kutaka nchi wanachama waendelee kutoa ushirikiano wa kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria watuhumiwa walioko bado mafichoni”. akasema Balozi Seif Iddi

Na kuongeza “ Nikiizungumzia Tanzania, ninapenda niwahakikishie, waheshimiwa marais, kwamba serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano siyo tu kwa ICTR bali hata kwa mahakama ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani (ICTY)pale itakapo bidi.

Akatumia fursa hiyo kuzitaka nchi nyingine kutoa ushirikiano kwa mahakama hizo na kuhakikisha kwamba watuhumiwa ambao wanasadikiwa kuwa wamo ndani ya nchi zao wanafikishwa kwenye mkono wa sheria.

Awali Marais wa Mahakama hizo wakiwasilisha taarifa zao wameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba licha ya kazi kubwa na nzuri ambayo mahakama zao zimekuwa zikitekeleza hadi sasa, ukwasi wa fedha na wafanyakazi wenye uzoefu unarudisha nyuma utendaji kazi wa Mahakam hizo.

Jaji Dennis Byron, Rais wa Mahakama ya Rwanda akiwasilisha taarifa yake, amesema kuwa Mahakama hiyo imeendelea kupoteza wafanyakazi wenye uwezo na uzoefu mzuri ambao wamekuwa wakiondoa na kwenda kutafuta kazi zenye maslahi mazuri zaidi.

Akasema hadi sasa ICTR imekwisha kupotea wafanyakazi 167 kati ya Julai 2009 na Juni 2010. Na kuongeza kuwa licha cha changamoto zote hizo, mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha Tanzania inaendelea na mchakato wa kukamilisha kesi zinazotakiwa kumalizika kabla ya mwaka 2011.

Kwa upande wake Jaji Patrick Robinson, Rais wa Mahakama ya Yugoslavia wa Zamani ( ICTY) naye amesema kuwa tatizo la kuondoka kwa wafanyakazi wenye uzoefu limeathiri pia mahakama yake. Na akauomba Umoja wa Mataifa kuzisaidia Mahakama hizo ili ziweze kukamilisha kazi zake.

Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) ilianzishwa mwaka 1994 wakati ile ya Yugoslavia iliyoko The Hauge Uholanzi,ilianzishwa katika miaka ya 1990 baada vita vya Balkan

TANZANIA IMEFANIKIWA KATIKA TEKNOHAMA KUTOKANA NA SERA NA MFUMO WA LESENI ULIOPO

Na Innocent P. M. Mungy
Guadalajara Mexico,

Tanzania imefanikisha kukua kwa sekta ya TEKNOHAMA (Teknolojia ya habari na Mawasiliano (ICT) kutokana na sera yake ya TEKNOHAMA ya mwaka 2003 pamoja na Mfumo wa Leseni wa Muingiliano wa Teknologia (Convergence Licsensing Framework) inayoutekeleza.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla alipokuwa anahutubia Mkutano Mkuu wa ITU 2010 (ITU Plenipotentiary unaofanyika hapa Guadalajara Mexico.
Prof. msolla alisema sera hiyo iliyopelekea kuundwa kwa mfumo huo, vimewezesha sekta ya mawasiliano kukua kwa kasi nchini na kuleta maendeleo kwa kipindi kifupi.

Alitaja maeneo yanayoonesha kukua kwa sekta hio kuwa ni pamoja na kuwepo kwa makampuni saba ya simu za mkononi yanayofanya kazi nchini na mengine manne yanayojenga mitandao tayari kuanza kazi.
Hali kadhalika alisema matumizi ya simu za mkononi yamekuwa kutoka watumiaji karibu laki mbili hadi kufikia takkribani milioni 18 hivi sasa.
Watumiaji wa intenet pia wameongezeka kutoka asilimia 0.06 mwaka 1994 hadi asilimia 12 hivi sasa.

Mkutano huo unaendelea jijini Guadalajara na masuala muhimu ya maendeleo ya sekta ya habari na mawasiliano yatajadiliwa na kufikia maamuzi muhimu kwa maendeleo ya baadae.

Mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Mexico Felipe Calderón Hinojosa aliyewataka wajumbe wa mkutano huo kuwa makini katika majadiliano na kufikia maamuzi yatakayoleta maendeleo ya TEKNOHAMA kwa watu wote duniani.

Tuesday, October 5, 2010

Ndugu yetu Makulilo atoa msaa katika Green Card U.S.A.

Entries for the DV-2012 DV lottery must be submitted electronically between noon, Eastern Daylight Time (EDT) (GMT-4), Tuesday, October 5, 2010, and noon, Eastern Daylight Time (EDT) (GMT-4), Wednesday, November 3, 2010. Applicants may access the electronic DV Entry Form (E-DV) at www.dvlottery.state.gov
during the registration period. Paper entries will not be accepted. Applicants are strongly encouraged not to wait until the last week of the registration period to enter. Heavy demand may result in website delays. No entries will be accepted after noon, EDT, on November 3, 2010.

Electronic lottery entry in the annual DV program is free (there is no fee). The U.S. Government employs no outside consultants or private services to operate the DV program. Any intermediaries or others who offer assistance to prepare DV entries do so without the authority or consent of the U.S. Government. Use of any outside intermediary or assistance to prepare a DV entry is entirely at the entrant’s discretion.

Instructions for the DV 2012 Lottery:
READ before applying please

http://travel.state.gov/pdf/1318-DV2012Instructions-ENGL.pdf

-------------------------------------------------------------------------------

NOTE:
Watch the Video on Green Card Lottery specific procedures and requirements at youtube.com/watch?v=5NtBFBQSBsg

If you have problem on Green Card photo requirements, write me at makulilo@makulilofoundation.org

and I will help to edit your digital photo for FREE.

For more videos on scholarships and other opportunities, visit www.youtube.com/makulilofoundation

MAKULILO, Jr.
makulilo@makulilofoundation.org