Washiriki kumi na sita wamejitokeza kushiriki katika Shindano la mwaka huu la Kimwana wa Twanga Pepeta. Washiriki hao wote wanatokea Dar es salaam katika Wilaya zote yaani Ilala, Temeke na Kinondoni.
ASET na MANYWELE inatoa wito kwa kina dada kujitokeza kwa wingi kwa kuwa nafasi bado zipo nyingi za wao kushiriki katika shindano la mwaka huu la Manywele Kimwana wa Twanga Pepeta 2011.
Zawadi ya Mshindi wa Kwanza anataraji kupatiwa Duka la vipodozi lenye thamani ya Shilingi Milioni Tano za Kitanzania.
Washiriki hao baadae wiki hii wanataraji kuanza kambi rasmi ili kujifua kwa ajili ya utambulisho unaotarajiwa kufanyika tarehe 06-05-2011 katika Klabu ya San Siro ambapo kundi zima la African Stars "TWANGA PEPETA" na Msanii aliyefanikiwa kuzoa tuzo tano za Kili za Mwaka huu 20% na baadae shoo kali kutoka kwa akina dada watakaoshiriki Manywele Kimwana wa Twanga Pepeta 2011.
Wadhamini wa shindano la Manywele Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 ni pamoja na EAST AFRICA TV/RADIO, GLOBAL PUBLISHER, CLUB SAN SIRO SINZA, BM BARBER SHOP na MICHUZI BLOG.
This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Tuesday, April 19, 2011
Anti Lulu ametukalia uchi, jambo ambalo si zuri
Presenta wa Kipindi cha Nyumbani ni Nyumbani katika Kituo cha Runinga cha C2C cha jijini Dar es Salaam, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt Lulu’ (pichani) amewashangaza watu baada ya kukaa vibaya huku akiacha wazi maungo yake nyeti.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Paparazi wetu lilijiri ndani ya ‘kiwanja’ cha starehe cha Billicanas kilichopo Posta, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika tukio hilo, kachero wetu alimshuhudia Aunt Lulu akiwa hana tone la aibu usoni huku baadhi ya watu wakiponda kivazi alichotinga ambacho mbali na kumwacha uchi kwa asilimia kubwa lakini pia kilimchora akiwa hana hata ‘kufuli’ yaani Chupi.
“Hiyo Mei 21, naamini kabisa ni mwisho wa dunia kwa staili hii, wewe angalia msichana kama yule anatembea uchi na mbaya zaidi hana nguo ya ndani,” alisikika mrembo mmoja aliyemwona Aunt Lulu ukumbini humo.
Kama kawa kama dawa, Risasi Mchanganyiko ‘lilimtaiti’ Aunt Lulu na kumhoji kulikoni kukaa uchi ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Siko hapa kwa ajili ya kujibu maswali, niko kistarehe zaidi.”

Friday, April 15, 2011
Kasheshe la VISA za KIchina
Na Issa Mnally
Baada ya mateso ya muda mrefu ya Watanzania kulala nje ya Ubalozi wa China uliopo jijini Dar es Salaam wakifuatilia vibali vya kuingilia nchini humo ‘Viza’, suala hilo sasa limechukua sura mpya baada ya wananchi kufanya vurugu kwenye ubalozi huo wakishinikiza kulegezwa kwa masharti.
Tukio hili lililovuta hisia za watu wengi lilijiri Aprili 10, mwaka huu na kusababisha afisa mmoja wa ubalozi huo kutekwa na wananchi hao akishinikizwa amwite Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng ili aongee nao.
“Huondoki hapa mpaka umwite balozi mwenyewe. Hii ni nchi yetu, tumechoka na manyanyaso yenu. Nyiye mnaingia kila siku hapa kwetu kufanya biashara, lakini sisi tukitaka kwenda kwenu mnatutenda kama mbwa kwa kutukeshesha hapa nje ya ubalozi wenu,” walisema Watanzania hao huku wakionekana kupandwa na hasira.
Kufuatia shinikizo hilo, afisa huyo alilazimika kupiga simu kwa bosi wake huyo ili kumwita.
Hata hivyo, badala ya balozi huyo kutoka yeye, alimtuma afisa mwingine, jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ambaye alipofika ndipo wananchi hao wakamwachia afisa waliyekuwa wamemteka na kuanza kuongea na mtu huyo.
Katika kujibu malalamiko ya wananchi hao, afisa huyo alisema hata wao wanaelewa hali ni mbaya lakini ni kwa sababu hawana wafanyabiashara wengi ndiyo maana wanachukua jumla ya watu 20 tu kwa siku ingawa wanapokea maombi kati ya 200 hadi 300 kwa siku moja.
Baada ya majibu hayo afisa huyo aliondoka kwa dharau akiwa amesusa kuongea zaidi na wananchi hao.
“Mnaona mnaona, hawa Wachina wanadharau sana. Sasa ngoja, muda si mrefu tutaanza chuki dhidi yao kama ilivyotokea kule Afrika Kusini. Tutawaondoa wote warejee kwao,” alisema mwananchi mmoja.
Tukio la Afrika Kusini alilomaanisha ni lile lililoitwa ‘Xenophobic’ ambapo wazawa waliwachinja wageni kwa chuki wakidai kwamba, waliingia nchini mwao kuchukua nafasi zao za ajira na kufanikiwa.
Aidha, kitendo cha dharau kilichofanywa na afisa huyo wa ubalozi kilisababisha wananchi waamue kutumia nguvu kuingia ndani ili waonane na Balozi Xinsheng, uamuzi uliosababisha vurugu kubwa kwenye lango la ubalozini hapo.
Hata hivyo, ghafla Askari wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walifika kujaribu kutuliza vurugu hizo.
Ndipo uongozi wa ubalozi ukaruhusu wawakilishi kadhaa wa wananchi hao kuingia ndani kuonana na maafisa wengine wa ubalozi huo.
Ndani ya ubalozi huo yalitolewa masharti kwamba, mwandishi wa gazeti hili, Issa Mnally asiingie na kamera kitendo ambacho hakikukubaliwa na wawakilishi hao hivyo kufanya mazungumzo hayo kushindikana.
Nje nako, hali ilizidi kuwa mbaya kwani wananchi walijiandaa kufanya fujo zaidi, ndipo askari wa FFU walipoamua kuingia ndani na kuomba kuonana na balozi ili kutafuta suluhu ya tatizo hilo.
Baada ya majadiliano yaliyochukua takribani dakika ishirini, uongozi wa ubalozi ulitoa tamko kuwa, umekubali kuongeza idadi ya maombi kutoka 20 ya zamani hadi 50 ili kupunguza jazba za wananchi.
Hata hivyo, bado wananchi hao walionesha kutoridhishwa na majibu hayo wakitaka Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuingilia kati suala hilo ili utaratibu wa Viza ubadilishwe na kuwa kama balozi nyingine ambazo hazina matatizo kama ya China yaliyotafsiriwa kama unyanyasaji wa raia.
“Kwa nini wasifanye kama ubalozi wa Marekani. Kule tunajaza fomu kupitia mtandao, hakuna usumbufu kabisa?” Alisema mwananchi mmoja.
Madai hayo yaliyotolewa na wananchi na kurekodiwa na gazeti hili yamesema kuwa, kinachofanywa na Serikali ya China ni utekelezaji wa mpango kabambe wa kuwaendeleza raia wake walioko nchi za nje.
Madai hayo yakaendelea kusema kuwa, Serikali hiyo inawabana wageni kwenda kwao kununua bidhaa ili Wachina walioko katika nchi hizo waliochukua uajenti wa viwanda vya kwao waweze kufanya biashara vizuri na kutajirika huku wazawa wakizidi kufa kiuchumi.
“Tumeshaufahamu mpango wao na sisi hatukubali, kama hivyo ndivyo basi Wachina wasiingie kabisa hapa nchini kwetu,” alisema mwananchi mmoja.
Aidha, wananchi hao wamepeleka kilio chao kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, asaidie kuwaondolea kero hii ya Viza katika ubalozi huo, wanaamini anaweza kuwasaidia.

Mabinti wa Twiga Stars wakiwa mazoezini
Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya wanawake 'Twiga Stars' wakifanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya michuano ya awali ya kusaka tiketi ya kucheza fainalio za kombe la mataifa ya Afrika. Picha na Chachandu Daily
Saturday, April 9, 2011
Kampeni ya malaria jijini Arusha
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa,Jan Poulsen akiwa na baadhi ya watoto wa shule katika viwanja vya sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo.Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya malaria imefanyika jijini Arusha jana katika kiwanja Sheikh Amri Abeid na kuhuduriwa na kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania pamoja na mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni.
Ambapo shule zaidi ya nane zimeshiriki mashindan hayo ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi za kuhakikihsha kuwa Malaria haikubaliki miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
Shindano hilo limeandaliwa na taasisi ya John Hopkins University ya marekani tawi la tanzania.
Awali akifungua michezo hiyo katibu tawala wa jiji la Arusha, bibi. Emmy Lyimo alisema serikali imefurahishwa sana na juhudi za taasisi hiyo katika kuhakikisha jamii inapiga vita ugonjwa wa malaria na kusema huu ni mchango mkubwa sana uliowahi kupatikana katika juhudi za kupambana na malaria nchini Tanzania.
Alisema kilele cha siku ya malaria ulimwenguni kitafanyika katika jiji la Arusha tarehe 25/04/2011, hivyo kutafunguliwa kliiki ya kusaidia kukumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia Vyandarua vyenye dawa ya kuuwa mbu na pia kutumia dawa kwa usahihi pale mtu anapokutwa na wadudu wa malaria.
Aliwataka wanajamii kote nchini kuungana kwa pamoja katika kuupinga ugonjwa huo na pia kuzingatia kauli mbiu ya serikali ya MALARIA HAIKUBALIKI NA TUUNGANE KUITOKOMEZA.
Kwa upande wake mkurugenzi wa ufundi wa TFF Bw. Sunday Kayuni alisema wameamua kufanya michezo hiyo kwa watoto kutokana na ukweli watoto ndio tabaka linaloongoza kwa vifo vya maaria kote ulimwenguni ambapo barani Afrika pekee kila baada ya sekunde thelathini mtoto mmoja hupoteza maisha.
Jumla ya zaidi ya watoto mia tano wameshiriki katika michezo hiyo ambapo licha ya kupata mafunzo lakini wanapatiwa vyeti na vyandarua kwa kila mshiriki kwaajili ya kuwasaidia kwenda kuwa mabalozi wa kudumu wa malaria kote ulimwenguni
Wednesday, April 6, 2011
Mambo ya Davina
Na Imelda Mtema
Msanii wa filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ (pichani) aliye zao la Kaole Sanaa Group, ameruka kimanga skendo inayomtafuna ya kuzaa na mume wa mtu ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Davina alisema kuwa, kumekuwa na uvumi wa yeye kuzaa na mwanaume huyo ambaye anadai hamjui ambao umekuwa ukienezwa na wabaya wake kwa lengo la kumchafua.
“Unajua wasichana wa mjini wamekalia umbeya tu, kazi kufuatilia maisha ya watu na kuwatafutia skendo zisizokuwa na miguu wala kichwa.
“Sijazaa na mume wa mtu na wala simjui, sema tu mtu anaweza kukupakazia chochote anachojisikia kwa sababu ameona hawezi kupimana ubavu na wewe hivyo anaamua kukuchafua. Ukweli sijui faida anayopata mtu wa aina hiyo,” alisema Davina na kuongeza:
“Kuna baadhi ya watu huwa hawapendi kuona maendeleo ya mwenzake hivyo binadamu wanapaswa kuwa makini kupita maelezo.”
Davina ni msanii wa ‘long time’ ambaye yupo mbioni kutoa kitu chake kipya kinachokwenda kwa jina la She is Mine akishirikiana na msanii mwenzake, Mwasiti Mohamed ‘Sishi’.

Friday, April 1, 2011
CHEKA KUZICHAPA NA BONDIA BORA DUNIANI KUTOKA MAREKANI!!
Kimbau akielezea mpambano huo, Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam.
AFISA Uhusiano wa Kampuni ya Aurora Group Companies, Shomari Kimbau, leo ametangaza mpambano wa ngumi unaotambuliwa kimataifa na IBF kati ya bondia Francis Cheka wa hapa nchini anayeshikilia nafasi ya 134 kwa ubora duniani, na Marcus Upshaw wa Marekani ambaye anashika nafasi ya 36 kwa ubora duniani na nafasi ya 6 nchini Marekani.
Mwanamasumbwi Francis Cheka wa Tanzania.
Kimbau amesema mpambano huo utafanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Mei 1 mwaka huu ambapo refarii na wasimamizi wengine watatoka nchi mbalimbali. Kimbau aliongeza kwamba endapo Cheka atashinda pambano hilo linalotambulika kimataifa atapanda kutoka nafasi ya 134 duniani aliyopo sasa.Bondia Marcus Upshaw wa Marekani.

Subscribe to:
Posts (Atom)