This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Friday, October 28, 2011
Thursday, October 27, 2011
Gaddafi is NO MORE!!
Pichani juu ni Mwili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, kabla ya kuzikwa.
Luqman Maloto na Intaneti
MAZISHI ya aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, yalitawaliwa na maajabu ya aina yake, kubwa zaidi likiwa ni kaburi alilozikwa kuwa na kina kirefu kupita kawaida.
Hata hivyo, haikuelezwa ni muda gani mwili wa Gaddafi ulizikwa lakini vyanzo mbalimbali vinaeleza maajabu ya mazishi hayo.
MOSI: Kaburi hilo lilichimbwa urefu wa futi 12. Baraza la Mpito la Libya (NTC) lilifanya makusudi ili kuwakomoa watu watakaotaka kuutafuta mwili wa kiongozi huyo.
PILI: Alizikwa wakati wa giza. Walifanya hivyo ili watu wasione. Lengo ni sehemu aliyozikwa ibaki kuwa siri.
TATU: Inadaiwa hakuoshwa kama sheria ya dini yake ya Kiislam inavyotaka, wala hakuhifadhiwa kwenye sanda.
NNE: Hakuna ndugu yeyote aliyehudhuria.
TANO: Hakukuwa na kiongozi wa kidini aliyeongoza mazishi. Wapiganaji wa NTC kwa muongozo wa mabosi wao, waliuchukua mwili wake na kuufukia.
AZIKWA JANGWANI
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kama lilivyopokea taarifa kutoka kwa maofisa wa NTC, jirani na Gaddafi alizikwa mwanaye aliyeuawa naye wakati wa mapambano, Mutassim.
BBC liliandika kuwa NTC ilieleza kwamba Gaddafi alizikwa jangwani kwa siri mno na hakuna alama yoyote ambayo imeachwa.
Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa serikali ya Gaddafi, Libya, Abu Bakr Younis Jabr, ambaye aliuawa siku moja na bosi wake, alizikwa pia sehemu hiyo.
MWISHO MBAYA
Ulikuwa mwisho mbaya wa Kanali Gaddafi, kwani kabla hajazikwa, mwili wake ulikuwa umeshaharibika na kutoa wadudu.
Habari zinasema kuwa wananchi wa Libya, waliokuwa wanakwenda kuushuhudia mwili huo walilazimika kufunika pua zao kutokana na harufu kali.
Awali, kulikuwa na danadana kuhusu mazishi ya Gaddafi, ingawa mwishoni, Serikali ya Baraza la Mpito (NTC) ilitangaza kuukabidhi mwili wa mwanaharakati huyo wa Umoja wa Afrika kwa familia yake.
Watu wa kabila la kiongozi huyo wa zamani wa Libya, walidai wakabidhiwe mwili wa ndugu yao ili wauzike kwa heshima, lakini NTC, iliweka ngumu kwa madai kuwa ni lazima azikwe kwa siri kubwa.
NTC ilidai kwamba ni busara Gaddafi azikwe eneo la siri kwa sababu kaburi lake likijulikana, kuna watu watakuwa wanakwenda kumuabudu.
Waziri wa Mkuu wa Serikali ya NTC, Libya, Mahmoud Jibril alisema: “Ni jambo hatari sana kuuzika mwili wa Gaddafi sehemu inayojulikana. Kuna watu watakuwa wanakwenda kwenye kaburi lake kuabudu.
“Ni vema na salama mwili wake uzikwe eneo la siri. Jukumu la kuzika mwili wake lipo ndani ya NTC na tutauzika kwa siri kubwa.”
Hata hivyo, baada ya jumuiya za kimataifa kuingilia kati kwa kuilaani NTC na Nato kutokana na udhalilishaji walioufanya kwa mwili wa Gaddafi, baadaye Jibril alitangaza kuukabidhi mwili wa mfadhili mkuu huyo wa AU kwa familia yake.
Jumatatu jioni ya wiki hii, Jibril alisema: “Taratibu zinaandaliwa, mwili wa Gaddafi utakabidhiwa kwa familia yake ambayo ndiyo itasimamia mazishi, lakini hakutakuwa na maadhimisho kitaifa.”
Jumanne wiki hii (juzi), Waziri wa Habari wa Libya katika Serikali ya NTC, Mahmoud Shammam, alikwenda kwenye chumba ambacho kimetumika kuuhifadhi mwili wa Gaddafi lakini baada ya kuzidiwa na harufu, aliziba pua.
Shammam alikiri kuwa mwili umeharibika na kwamba ili kuepusha athari zaidi, inabidi uzikwe haraka.
Baadaye, NTC ilibadili uamuzi na kumzika kwa siri bila familia wala kiongozi yeyote wa kidini kuhusishwa.
Katibu Mkuu wa zamani wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) sasa Umoja wa Afrika (AU), Dk. Salim Ahmed Salim, alizungumza kupitia redio ya watu, Clouds FM na kulaani kila kitu alichotendewa Gaddafi.
Dk. Salim alisema, ni bora Gaddafi angeuawa kwenye mapambano lakini inasikitisha kwa sababu alikamatwa mzima kisha kuuawa kwa risasi.
Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Tanzania, alilaani hata kitendo cha mwili wa kiongozi huyo kuachwa wazi kwa sababu kinapingana hata na sheria za Kiislam.
Wednesday, October 26, 2011
THREE LEADERSHIP SKILLS
1.Productive Paranoia.
Bill Gates was hyper-vigilant about what could hit and damage Microsoft.
“Fear should guide you,” he said in 1994. “I consider failure on a regular
basis.” Herb Kelleher predicted eleven of the last three recessions. Andy
Grove ran around “looking for the black cloud in the silver lining.”
Productive paranoia is the ability to be hyper-vigilant about potentially
bad events that can hit your company and then turn that fear into
preparation and clearheaded action. You can’t sit around being fearful;
you must act, like Herb Kelleher, who insisted on cutting costs and
running lean operations in good times, so that they would be prepared for
the next storm, imagined or real.
2.Empirical Creativity.
Well, just staying alive does not produce greatness. You must also create.
So we should expect these leaders to be highly creative—to create new,
wonderful products. Yes, but here’s the rub. The leaders of the average
industry peers also displayed lots of creativity. We found that the
differentiating leadership principle was a certain approach to creativity,
what we call empirical creativity—the ability to empirically validate your
creative instincts. This means using direct observation, conducting
practical experiments, and engaging directly with evidence, rather than
relying on opinion, whim, and analysis alone (and, as a prior management
consultant, I would include pure market analysis void of testing in this
category). When Peter Lewis of Progressive, the car insurance company, had
the idea of expanding into the safe-driver market, he did not move in one
big swoop. Rather, he started with trials in Texas and Florida, then added
more experiments in other states, and finally, three years later, when the
concept was validated, he bet big on the new business. His idea was rooted
in empiricism, not analysis alone.
3.Fanatic Discipline.
Discipline can mean many things—working hard, following rules, being
obedient, and so on. We mean something else: The best-performing leaders
in our study exhibited discipline as consistency of action—consistency
with values, long-term goals, and performance standards; consistency of
method; and consistency over time. It involves rejecting conventional
wisdom, hype, and the madness of crowds—essentially being a
nonconformist. When John Brown of Stryker set the long-term goal of 20%
annual net income growth, year in and year out (he hit it in more than
90% during 21 years), he was so committed to this quest that it could
only be described as, well, fanatical. Markets down? Competition severe?
Recession? Market hype? He did not care. He built a system of fanatic
discipline to achieve the quest, no matter what. He was highly
disciplined by showing consistency between his words (the goal) and his
behaviors (everything he did to make it happen).
You need all three leadership skills in an uncertain world: Fanatic
discipline keeps you on track; empirical creativity keeps you vibrant; and
productive paranoia keeps you alive.
When I speak to leaders, I find it helpful to ask: When you consider these
three leadership skills, which do you perceive as your weakest one, and
how can you turn that into a strength?

AJALI YA BASI LA DELUX-Jana Jumanne October 25, 2011 Saa 8 mchana
Basi lilikua likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, likapasuka tairi la mbele, likapinduka na likawaka moto maeneo ya Kongowe km 10 kabla kufika Mlandizi. Wengine wamepaita eneo la ajali eti ni Kibaha Misugusugu. Abiria zaidi ya saba wamefariki tena baadhi yao hawatambuliki kwa jinsi walivyoteketea kwa moto.
Monday, October 24, 2011
By Luquman Maloto na Mitandao wa GPL
KUNA mvutano kuhusu mazishi ya marehemu Kanali Muammar Gaddafi, watu wa kabila la kiongozi huyo wa zamani wa Libya, wanadai mwili wa ndugu yao ili wauzike kwa heshima, wakati Baraza la Mpito linaweka ngumu na kusisitiza kwamba atazikwa kwa siri kubwa.
Ijumaa Wikienda, limenasa maisha ya Gaddafi saa 18 kabla ya kifo chake pamoja na danadana za mwili…
Luquman Maloto na Mitandao
KUNA mvutano kuhusu mazishi ya marehemu Kanali Muammar Gaddafi, watu wa kabila la kiongozi huyo wa zamani wa Libya, wanadai mwili wa ndugu yao ili wauzike kwa heshima, wakati Baraza la Mpito linaweka ngumu na kusisitiza kwamba atazikwa kwa siri kubwa.
Ijumaa Wikienda, limenasa maisha ya Gaddafi saa 18 kabla ya kifo chake pamoja na danadana za mwili wa kiongozi huyo ambaye neno lake, harakati zake na fedha alizomwaga katika ufadhili, ndivyo viliwezesha kuundwa kwa Umoja wa Afrika.
Jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Baraza la Mpito (NTC), Mustafa Mohammed Abdul Jalil alitarajiwa kwenda jijini Misrata kutoa tamko kuhusu mazishi hayo.
Kwa mujibu wa mtu anayedaiwa alikuwa mlinzi wa Gaddafi kabla ya kumgeuka dakika za mwisho, saa 18 kabla kiongozi huyo wa zamani wa Libya kufariki dunia, alizitumia kusali na kuweka mikakati ya kuhama Jiji la Sirte.
Mlinzi huyo (jina limehifadhiwa) alisema kuwa katika saa hizo 18, Gaddafi alizungumza na wanajeshi wachache waliokuwa wamebaki wanamlinda na kuwaambia kwamba hategemei kurudi kutawala Libya na hadhani kama ana maisha marefu.
Hata hivyo, jina la mlinzi huyo limefichwa ili kukwepa hasira za watu wanaompenda Gaddafi kulipa kisasi.
Aliongeza kusema: “Aliwaambia wapigaji kwamba wakipata nafasi warudi kuitetea Libya na wasikubali vibaraka wa Marekani na Uingereza wafilisi mali za Walibya.”
Alisema kuwa saa tatu kabla Gaddafi na timu yake, hawajaanza kutoroka, alizungumza na wanaye kwa muda mrefu lakini akawasisitiza: “Msiumie wala msifedheheke, wakati mwingine Shetani hutumia nguvu na kufunika haki dhidi ya batili.”
NENO LA MWISHO
Mlinzi huyo alisema, Gaddafi alijitetea kwa maneno mengi ili asiuawe lakini kauli maarufu aliitoa kwa njia ya kuuliza, “je, ninyi wanangu, mnaifahamu haki kwenye uongo?”
SAFARI YA KIFO
Alhamisi iliyopita (Oktoba 20, 2011), Gaddafi na timu yake, wakiwa kwenye magari ya kifahari, walikuwa wanahama kutoka Jiji la Sirte kuelekea mpakani. Inadaiwa walitaka kutorokea nje ya nchi, ingawa taarifa nyingine zinadai kiongozi huyo aligoma kuondoka na kusisitiza anangoja kufa kwenye ardhi aliyozaliwa.
Saa 2:30 asubuhi (saa za Libya), vikosi vya Nato na Ufaransa viliyashambulia kwa mabomu magari ya msafara wa Gaddafi. Magari 15 yaliharibiwa kwenye mashambulizi hayo, Gaddafi na timu yake walikwenda kujificha kwenye daraja la mtaro.
5:05 asubuhi, NTC ilitangaza kuwa ngome ya Gaddafi imekwisha na kilichobaki ni kutafuta masalia.
8:00 mchana, baada ya mapambano ya risasi kwisha, Gaddafi aligundulika yupo kwenye daraja la mtaro wa maji machafu amejificha.
8:45 mchana mwanaume mmoja mkazi wa Sirte aliliambia Shirika la Utangazaji la Reuters kuwa alimuona Gaddafi akipigwa risasi tumboni kwa bastola yenye ukumwa wa 9mm.
8:56 mchana, Reuters ilitangaza kuwa Gaddafi alifariki dunia kutokana na majeraha baada ya mapigano ya risasi.
9:00 mchana, wapiganaji wa NTC walianza kuzunguka mitaani wanashangilia kukamatwa na kuuawa kwa Gaddafi.
10:31 alasiri, AFP ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Muttasim amekutwa ameuawa jijini Sirte.
11:52 jioni, mwili wa Gaddafi ulifikishwa Misrata.
1:50 jioni, Aljazeera ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Saif al Islam naye ameuawa kwenye mashambulizi hayo. Ingawa taarifa za baadaye zinasema kuwa Saif mikono yake ilikatika katika mashambulizi.
Saturday, October 22, 2011
Harusi ya Micky na Monicah ndo imemalizika hivi punde
Ni katika kanisa la Katoliki pale Njiro
Fuatana nami katika picha hizi
Hapa Bibi harusi akiingizwa
Anaingia Kanisani
Ndani ya Kanisa-Mambo na taratibu mbalimbali
Monicah akila kiapo kumkubali Micky kwa hiari yake wala hajalazimishwa
Waumini waliohudhuria wakiwabariki maharusi
Baraka toka kwa Padre
Na waliporuhusiwa kukumbatiana hawakufanya ajizi, hebu muone Monicah anavyolisikilizia kumbatio la mumewe Micky!
Na ndipo Micky akaanza kumvisha pete mkewe
Monicah nae akamalizia
Wakaanza kutoka na safari ya ukumbini ikaanza
Wanapongezana ndani ya gari
Kwaya hii ilihudumu kwa nyimbo tamu

Friday, October 21, 2011
Dada Monicah ameremeta katika Send Off party yake
Sherehe ilifanyika huko Shambalai, wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara
Hapa chini ni Bwana Harusi mtarajiwa Micky Thambikeni akipokelewa ukweni yeye na msafara wake.
Makao ya muagwa-Monicah kabla mwenyewe hajafika
Yeye mwenyewe ndio huyu hapa chini kushoto.
Shangazi wa Bwana Harusi mtarajiwa-Micky akipokelewa
Msafara wa Bwana harusi mtarajiwa-Micky wakiwa katika pozi wakishuhudia kinachoendelea
Mpiga picha wetu nae alikua bize haswa
Wawakilishi wa wazazi wa Bwana harusi mtarajiwa wakipeleka zawadi kwa wazazi wa Binti
Hapa pia
Baba mzazi na Mama mzazi wa Monicah wakiwa tayari kupokea zawadi
Sasa zoezi la kupokea zawadi limeanza rasmi
Picha ya pamoja na wazawadiwa
Bibi harusi mtarajiwa nae alienda mbele ili kuzawadiwa
Mara safari ya kumtafuta mchumba akiaanza, haya twende pamoja
Alipomkosa nje ya ukumbi akarudi ndani
Hata katikati ya watazamaji alipita kumsaka barafu wa moyo wake. Duh si mchezo ati!
Mara akamwona na safari ya kwenda nae ikaanza
Akala tunda yeye kisha akampa Micky nae akale
Pozi hili ni zuri sana
Kaka mtu akimtoa dada yake kwa mshenga
Hapa ni wao
Na hawa ni wasimamizi wao
Lishanaji keki ukaanza-Huyu ni Mchungaji wake
Wakafuata wazazi baba na mama
Mdogo wake hakusahaulika
Best wake nae alipongezwa kimtindo
Hapa anawakabidhi keki wakwe zake
Wazazi wa pande zote wakielekea katika chakula
Maharusi watarajiwa naowakichukua chakula
Hapa wanakula

Subscribe to:
Posts (Atom)