This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Thursday, December 29, 2011
Upepo mkali wapeperusha vitu na watu huko Blackpool Uingereza
![]() |
| Muone huyu mdada utadhani kaweka style ya Nwele kumbe ni kazi upepo hadi anaonekana hivyo, uso wote umefichwa na nywele wima, Duh si mchezo ati! |
Ndege yaanguka na kushika moto wakati ikitua
Wednesday, December 28, 2011
Tuesday, December 27, 2011
Ngazi za umeme zaboresha usafiri katika jiji nchini Colombia
Natamani zingekuja na hapa Tanzania haswa maeneo ya Usambaani na Upareni kwenye milima
![]() |
| Mama huyu naye anazitama ngazi hizo kwa mbele chini, zinapamba mji pia kusema ukweli |
![]() |
| Luis Holguin (Kushoto) na binti yake Refsa wakipandishwa na ngazi hizo. Ni raha sana |
![]() |
| Watoto nao wakijinafasi katika ngazi hizo |
![]() |
| Muonekano mpana zaidi wa ngazi hizo. Jueni kwamba huduma hii ni BURE. Hulipii chochote. |
Thursday, December 22, 2011
Wednesday, December 21, 2011
Tuesday, December 20, 2011
CHAKULA NDIYO CHANZO CHA MARADHI YANAYOTUSUMBUA
CHAKULA ni dawa, lakini chaweza kuwa sumu pia. Katika makala yetu ya leo tunazungumzia namna ambavyo chakula kimekuwa chanzo cha maradhi mengi sugu yanayotusumbua binadamu hivi sasa.
Vijana wengi wanapoteza uhai wakiwa bado vijana, maradhi kama shinikizo la damu (presha), saratani, kiharusi, kisukari, magonjwa ya miguu na migongo, yamekuwa sawa na ni wimbo wa taifa.
Asilimia kubwa ya magonjwa yanayotusumbua, kama vile shinikizo la damu (Low and High Blood Pressure), Magonjwa ya moyo (Cardiovascular diseases), saratani (cancer), ambayo ndiyo mengi, yanatokana na vyakula tunavyokula kila siku au tunavyoacha kula kama inayotakiwa.
Ukiangalia katika muongozo wa vyakula (Food Guide Pyramid) ambao unatuonesha kundi lipi la vyakula tunatakiwa kula kwa wingi na kundi lipi tunatakiwa kula kidogo, katika maisha halisi tuliyonayo, utaona muongozo huo umegeuzwa, miguu juu, kichwa chini.
Hii ina maana kwamba vyakula ambavyo tunapaswa kula kwa wingi tunakula kidogo au kwa nadra sana na vyakula ambavyo tunapaswa kula kidogo na kwa nadra ndiyo tunakula kwa wingi na karibu kila siku.
VYAKULA TUNAVYOTAKIWA KUVILA KWA WINGI
Katika muongozo huo wa vyakula, ambao unatambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), unaorodhesha vyakula vitokanavyo na nafaka kama vile mchele, ngano, mahindi, uwele, mtama, n.k, kama vyakula tunavyotakiwa kuvipa kipaumbele katika milo yetu ya kila siku kwa kuvila kwa wingi.
Tukizungumzia maisha ya Kitanzania, vyakula maarufu vitokanavyo na nafaka hizo, ambavyo vinatumiwa na familia nyingi ni ugali, wali, mikate, tambi, makande, uji, n.k. Uzoefu unaonesha kuwa familia nyingi za Kitanzania zinatumia ugali, wali na mikate, uji karibu kila siku katika milo yao, lakini tambi, kande na vingine vya jamii hiyo, huliwa mara moja moja.
TATIZO LIKO WAPI?
Ikiwa familia nyingi zinakula ugali, wali, mikate na maharage kila siku kama muongozo wa vyakula unavyotukata, tatizo liko wapi? Tatizo lipo, tena kubwa na familia nyingi zinaathirika nalo kwa kukosa elimu ya kutosha kuhusu vyakula wanavyokula. Kweli wanakula ugali, mikate, lakini VIMECHAKACHULIWA!
UGALI
Familia nyingi zinapopika ugali zinatumia unga mweupe, wenyewe wanaita sembe safi nyeupe, wakiamini kwamba huo ndiyo unga bora wakati siyo kweli.

Ili upate faida ya nafaka kwa kula ugali, ni lazima iwe nafaka ambayo haijaondolewa viini lishe vyake na ili vipatikane viini lishe hivyo, mahindi hayatakiwi kukobolewa bali yanatakiwa kusafishwa na kusagwa hivyohivyo.
Halikadhalika mtama na uwele.
Mahindi yaliyosagwa bila kukobolewa ndiyo yanayotoa unga safi na bora kiafya, unga huo ndiyo unaojulikana kama dona.
Mahindi yaliyosagwa bila kukobolewa ndiyo yanayotoa unga safi na bora kiafya, unga huo ndiyo unaojulikana kama dona.
Kwa kutumia unga huo, iwe kwa kupika ugali au uji, utakuwa umepata faida ya kula vyakula vitokanavyo na nafaka kama inavyoagizwa kwenye muongozo wa vyakula. Ulaji wa ugali ama uji uliotokana na sembe nyeupe ni sawa na kula chakula kilichochakachuliwa!
MIKATE
Kama ilivyo kwenye ugali, tatizo hilo lipo pia kwenye mikate inayotumiwa na familia nyingi mijini karibu kila siku. Mikate inayoliwa na watu wengi ni hii inayotengenezwa kutokana na nafaka ya ngano, lakini kwa bahati mbaya nayo huwa imechakachuliwa na kukosa faida ya ngano kiafya.
Mkate unaopendwa na kuliwa sana ni mkate mweupe, huu hutengenezawa kutokana na ngano iliyokobolewa na kwa maana hiyo kiafya hauna ubora, kwa sababu viini lishe vyake vimeondolewa na mbaya zaidi hutiwa sukari kunogesha ladha.

Licha ya kasoro hiyo, mkate mweupe umeendelea kuwa chaguo la kwanza na mlo wa kwanza katika familia nyingi duniani.
Ingawa kuna aina mbili ya mikate, lakini aina moja ndiyo inayopendwa na watu wengi zaidi kuliko aina nyingine ambayo hutengenezwa kutokana na ngano isiyokobolewa, aina hii huitwa mkate mweusi au ‘brown bread’

Waranti kumkamata makamu wa rais wa Iraq
![]() |
| Makamu wa rais wa Iraq, Tareq al-Hashemi |
Iraq imetoa waranti ya kumkamata makamu wa rais wa nchi hiyo Tareq al-Hashemi, kwa madai ya kuhusika na ugaidi.
Kwa mujibu wa duru za usalama na sheria, waranti hiyo imetolewa na kamati ya mahakama kuambatana na sheria za kupiga vita ugaidi. Wakati huo huo, wizara ya mambo ya ndani mjini Baghdad imesema, walinzi wa Hashemi wamekiri kupanga na kufanya mashambulio. Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya Iraq, watu hao walipewa fedha na walihakikishiwa kuungwa mkono na al-Hashemi. Makamu huyo wa rais wa madhehebu ya Kisunni, ni mpinzani na mkosoaji mkali wa Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ambae ni wa madhehebu ya Kishia.
Monday, December 19, 2011
BARCELONA YATWAA KOMBE LA KLABU BINGWA DUNIANI
![]() |
| Cesc Fabregas akiifungia Barcelona bao la tatu dhidi ya Santos katika fainali ya Klabu Bingwa Duniani iliyopigwa Yokohama, Japan leo. Barcelona imeshinda bao 4-0. |
Kwanini FUNGATE/HONEY-MOON ukafanyie kitanda cha GEST badala ya CHAKO nyumbani kwenu????
![]() |
WAUMINI wa Kikristo wametakiwa kulala kwenye vitanda vya nyumbani kwao na si vya nyumba za wageni (gesti) wakati wa FUNGATE/HONEY MOON, mara baada ya sherehe za harusi ili kuepuka tabia ya kufanya ngono hovyo hovyo na kuzizoea Gesti kupaona pa kawaida sana.
Haya yalisemwa na Mchungaji Elieza Masoud kutoka Mbeya ambaye alihudhuria harusi ya rafiki yake Mchungaji Thomas Paul wa Usharika wa Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) Mji Mpya katika Manispaa ya Morogoro ambaye amefunga pingu leo (Jumapili).

"Nashangaa sana, utaona mkazi wa maeneo ya Mji Mpya anaacha kitanda chake kizuri anakwenda kulala kwenye nyumba ya wageni inayopaswa kulala mimi mgeni kutoka Mbeya. Hii yote ni watu kukosa uelewa katika somo hili la harusi. Wanalichukulia kama maigizo ya Kanumba (mcheza sinema Steven)," alisema mchugaji huyo ambaye baada ya kumtaja Kanumba waumini wote waliofurika kwenye ibada hiyo waliangua vicheko
Akifafanua zaidi, mtumishi huyo wa Mungu alisema hali hiyo inatokana na watu kushindwa kuzidhibiti nafsi zao zilijojaa tamaa nyingi na kukosa hofu ya
Mungu.
Maoni ya Mhariri/Mwenye Blogu:
Hii ni kweli tena ni muhimu sana. Ndoa yangu niliyofunga Juni 14, 2003 nilifanyia FUNGATE/HONEY-MOON kwenye kitanda changu nyumbani. Sikuona HESHIMA kumpeleka mke wangu mpendwa na kufanya nae TENDO LA NDOA katika KITANDA CHA WOTE huko Gesti, Hoteli, Lodge au vyovyote utakavyoita.
Kuanzia Maigizo ya ITV hadi Degree Marekani
![]() |
| Mpiganaji Ligongo baada ya kuchukua cheti chake |
![]() |
| Mdau akiwa na mai waifu wake Mary-Mzubwa Ndaro, hii inakuwa kama vile mdau karudisha bao baada ya mai-waifu wake kula nondo toka chuo hicho hicho hivi karibuni |
Thursday, December 15, 2011
MGOMO WA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM
Wanafunzi hao waliokuwa wanaendeleza mgomo wao ulioanza Jumatatu wiki hii wakidai taarifa za kwa nini pesa zao zinachelewa wakati bodi ya mikopo, ilishasema wamezileta chuoni hapo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu na uvunjifu wa amani chuoni hapo tangu mwanzo wa juma hili.

Tuesday, December 13, 2011
WASHINDI WA AIRTEL MZUKA WAENDELEA KUJIZOLEA ZAWADI ZAO
Thursday, December 8, 2011
Mafuriko huko Bogota-Colombia
![]() |
| Firefighters evacuate residents from a flooded neighborhood in Patio Bonito, southwest of Bogota on Dec. 7. |
Miti ya X-Mass yaanzisha maandalizi ya sikukuu hiyo huko Marekani
![]() |
| Askari wa jeshi la Marekani Sgt Evan Kirouak ambaye amerejea hivi karibuni toka Iraq akipoea zawadi ya mti wa X-Mass jana Jumatano huko Fort Carson Colorado Spring-Marekani |
![]() |
| Hapa Sgt Evan Kirouak akisimama na mchumba wake Aeryn Dahl mara baada ya kuchagua mti wa X-Mass |
![]() |
| Sgt Patricia Foust wa jeshi la Marekani nae akiwa na mti wake wa X-Mass |
![]() |
| Mke wa askari wa jeshi la Marekani Candace Jones akiwa amembeba binti yake Abighail (mwenye miaka 2) huku akielekea kwenye gari mara baada ya naye kupata mti wake |
Subscribe to:
Posts (Atom)