Siku za hivi karibuni pamekuwa na minong'ono kwamba kuna mcheza mpira mmoja pale Uingereza anasadikika kuibanjua amri ya sita na mmoja wa aliyekuwa mshiriki katika kipindi cha televisheni cha Big Brother, Imogen Thomas.
Haraka haraka pakapitishwa sheria ya kulinda jina la mchezaji huyo wa mpira kutotolewa hadharani kwa sababu wanazozifahamu wao wenyewe. Leo, ghafla bin vuu, mbunge kwa tiketi ya chama cha Demokrasia ya Kiliberali, John Hemming, akatelezesha ulimi na kumtaja mchezaji huyo anayelindwa na sheria hiyo kuwa ni Ryan Giggs wa Man United. Bwana Hemming amekuwa mmoja wa wanaharakati ambaye amekuwa akipinga kwa mchezaji huyu kulindwa na sheria hiyo.
Sheria hii ilipitishwa mahsusi kuwabana watumiaji wa mtandao wa Twitter ambao walikuwa wameshalinyaka jina hilo na kuanza kumegeana ndogo ndogo kwa kasi ya sawa na moto wa nyika kwenye nyasi kavu. Hemming alipopewa nafasi ya kuuliza swali juu ya sheria hiyo, anayoamini imetungwa mahususi kuwafunga mdomo raia karibu 75,000 waliotumia Twitter kuhabarishana habari hiyo, alisema hakuna maana kuendelea kumlinda mchezaji huyo maadam jina lake limeshavuja kwa raia wa Twitter.
Akitumia nafasi ya kipekee katika ukumbi wa bunge, na bila shaka kujilinda kwa kanuni za bunge hilohilo, Hemming akajikuta akilianika jina Giggs dakika chache baada ya Mahakama Kuu ya Uingereza kutupilia mbali kesi iliyokuwa ikitaka sheria hiyo iliyokuwa mahsusi kumlinda Giggs ifutwe.
Hazikupita sekunde kadhaa kabla ya Hemming kuvutwa shati na spika wa Bunge hilo la Uingereza, John Bercow, ambaye ni spika kupitia chama cha Kihafidhina (Conservative). Bercow alisema, "Nafasi kama hii tuliyompa mbunge ni ya kujadili uhalali wa sheria hii na si kusimama na kusema chochote tu. Iwapo mbunge anataka kuendelea na hoja yake ya msingi na aendelee."
Duh! Unadhani ni kwa nini tumekuwa na mfululizo wa kesi za masuala ya uzinzi kwa watu maarufu, kwa kiasi kikubwa siku za hivi karibuni?
This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Tuesday, May 24, 2011
Ngeleja akabwa koo
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba amemshutumu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa amekuwa mtu wa kukimbia, kujificha na kutosema ukweli kuhusu tatizo la umeme nchini.
Ngeleja anatupiwa shutuma kuwa kauli ya Serikali aliyoitoa bungeni juu ya hali ya umeme nchini ikiwemo kukodishwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 260 ifikapo Juni na Julai mwaka huu imeshindikana lakini Waziri yuko kimya.
“Waziri alisema bungeni na akamwambia Rais (Jakaya Kikwete) naye akalitangazia Taifa kuwepo kwa umeme ifikapo Julai, lakini kwa taarifa nilizonazo biashara hiyo imekwama na Waziri yuko kimya anakimbia kusema ukweli,” alidai Makamba.
January alidai kitendo cha Waziri kukimbia na kujificha, kinaonesha kuna ombwe la uongozi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na akaahidi kuwa Kamati yake itambana Waziri huyo aeleze utekelezaji wa mipango yote aliyoiainisha kwenye kauli ya Serikali.

Tuesday, May 10, 2011
Wafah Dufour Bin Laden, Mtoto wa kaka yake Osama Bin Laden anayeng’ara kwenye Ulimbwende
Huku Dunia ikiwa inatawaliwa na habari pamoja na matukio yaliyoambatana na kupatikana na hatimaye kuuwawa kwa gaidi nambari moja Dunianiani (kwa mujibu wa CIA), Basi sisi Spoti na Starehe tunajaribu kuiangalia familia hii ya Osama Bin Laden katika kona nyingine ya kiburudani zaidi.
Pichani juu anaitwa Wafah Dufour ila jina lake kamili ni Wafah Dufour Binladin akiwa ni binti wa kaka yake Osama Bin Laden ambaye yeye na wazazi wake walikuwa wakiishi huko Calfornia-Marekani ambako walilowea.
Wafah ni mtoto wa kaka yake Osama anayeitwa Yeslam bin Ladin, Osama na Yeslam ni baadhi ya watoto 54 wa Mohammed bin Laden raia wa Yemen aliyeamia Saudi Arabia na kulowea huko ambapo alijiendeleza na kufikia kuwa ni mmoja wa makandarasi wakubwa. Mama yake anaitwa Carmen bin Ladin ambaye ni raia wa Iran amechanganyika na Mswiss.
Wafah Dufour aliishi Los Angeles Calfornia katika utoto wake na baadaye Jeddah, Saud Arabia lakini baadaye alihamia Geneve Switzerland akiambatana na wazazi wake na wadogo zake wawili wa kike Nadjia na Noor. Mnamo mwaka 1988, wazazi wake walitengana na baadaye waliachana (divorced) mwaka 2006. Inasemwa kuwa Wafah hajawahi kuongea na baba yake wala wadogo zake tangu akiwa na miaka 15.
Kabla ya September 11 alikuwa ni mtoto wa kawaida na ambaye alitumia jina lake bila ya wasiwasi kama mtu mwingine, hali ilibadilika ghafla baada ya Sep 11 ambapo jina la Bin Laden likawa ni kama nuksi kwake ndipo alipoamua kubadili jina na kutumia ubini wa mama yake na kujiita Wafah Dufour. “Siwezi kubadili ukweli kuwa ni hawa ni ndugu zangu na yule ni ndugu wa baba yangu, lakini pale inapokuja jina linahusishwa na ugaidi tena ambao umeua Wamarekani wenzangu, hapo ndio naliona jina mzigo” Alisema Wafah alipofanya mahojiano na jarida la GQ.
Kama watoto wengine Wafah naye alijifunza kutunza Koran akiwa na miaka 10 hukohuko CAlfornia Marekani, Wazazi wake walihamia Switzerland yeye akiwa binti mdogo.
Alipokuwa akaanza kuwa na mapenzi ya kufanya uanamitindo na muziki jambo ambalo alilifanikisha, mwenyewe anasema zamani aliishi vizuri sana na kwa uhuru ila baada ya tukio la September 11 la kigaidi jina la baba yake liliona chungu kwani alinyoshewa kidole kila anapopita.
“Nimezaliwa Amerika, nataka watu wajue mimi ni mmarekani, pia wajue mimi ni kama raia wengine wa Marekani, kwangu mimi Amerika ndio nyumbani” alisema Wafah alipoongea na jarida la GQ.
Baada ya tukio lile la Word Trade Centre kupigwa mabomu Wafah alikuwa America na anasema ilibidi ajifungie ndani kwa miezi 6 bila kuongea na watu, “nilipatwa na msongo wa mawazo (depression} na wakati mwingine kutamani hata nipotee kabisa”. Wakati wa tukio la September 11 Wafah alikuwa na mkataba mzuri wa kazi lakini kila kitu kilifutika, pamoja na kuwa na MAster Degree ya Sheria lakini bado kwa ubini wa BinLAden asingeweza kuajirika, ingawa bado alikuwa ni mwanafunzi wa New York’s Columbia Law School.
HApo ndipo idea ya kubadili jina ilipokuja na kuamua kubadili fani na kujikita kwenye Ulimbwende na Muziki ndipo alipokutana na jarida la GQ ambalo anasema lilimtoa.
Picha zile zilileta mtafaruku na kufanya aandamwe sana na vyombo vya habari kwani kwa kuzingatia anatoka kwenye familia yenye msimamo mkali wa kidini na yeye kupiga picha za nusu utupu. Kwa upande mmoja hii ilimbeba na kumpandisha chati sana kwenye fani yake.
Binafsi anasema anapenda kufanya kitu ambacho moyo wake unapenda na kamwe kisihusishwe na dini yake, bado imani yake ipo pale pale ila ni yeye anajua anachokifanya.
Kwa sasa Wafah ni mwanamitindo na mwanamuziki ambaye tayari amesharekodi nyimbo zake kadhaa zilizo kwenye mahadhi ya Pop!. Amejizolea umaarufu huku akifananishwa na Angeline Jolie kwa midomo yake. Kwa sasa Wafah anaishi London Uingereza na yuko kwenye mipango ya kujiunga na Bendi maarufu ya Rock Black Lips.

Thursday, May 5, 2011
Obama alishuhudia 'live' kifo cha Osama Bin Laden
Habari na Exuper Kachenje, Andrew Msechu na Mashirika ya Kimataifa
Rais wa Marekani Obama akifuatilia kwa karibu kifo cha jaidi Osama Bin Laden

RAIS Barrack Obama wa Marekani alishuhudia moja kwa moja (live) jinsi makomandoo 100 wa jeshi lake wakitekeleza shambulizi na hatimaye ‘mazishi’ ya kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda, Osama Bin Laden.
Operesheni hiyo ilishuhudiwa pia na Makamu wa Rais Joe Biden, Waziri wa Mambo ya Nje, Hillary Clinton, Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), Leon Panetta na viongozi wengine wa ngazi ya juu. Makomandoo hao walifanya kazi hiyo usiku wa giza nene wakiwa wamevaa miwani maalumu iliyowawezesha kuona.
Ilikuwa kama sinema wakati walipokuwa wakiendesha operesheni hiyo. Obama aliangalia tukio hilo zima akiwa Ikulu ya Marekani ya Washington-DC. Kazi hiyo ilitumia dakika 40 na kuhitimisha miaka 10 ya kujificha na kuwa tishio la mashambulizi ya kigaidi.
Kushuhudiwa huko moja kwa moja kwa operesheni hiyo, kuliwezeshwa na makomandoo hao kwani walivaa kamera maalumu zilizorekodi matukio yote yaliyokuwa yakifanyika na kuyarusha moja kwa moja hadi Ikulu ya Marekani na Makao Makuu ya CIA.
Kwa mujibu wa mtandao wa Gazeti la Daily Mail la Uingereza, shambulizi hilo lilifanyika huku kukiwa na wingu zito lililotanda katika Mji wa Abbottabad, Pakistan hali ambayo ilielezwa kwamba ilikuwa mwafaka kutekeleza kazi hiyo baada ya kuiahirisha usiku wa siku iliyotangulia.
Taarifa zinasema wachambuzi wa taarifa wa CIA walitumia mwezi mmoja wakifuatilia mtambo wa 'satellite' kujua kilichomo ndani ya nyumba alimouawa Osama kisha kuandaa ramani ilioongoza utekelezaji wa shambulizi hilo.
Habari hizo za kipelelezi zinaeleza kuwa Aprili 13, helikopta aina ya Black Hawks na makomandoo hao walikwenda hadi kituo cha anga Tarbela Ghazi, Kaskazini Mashariki mwa Pakistani ambacho CIA inaruhusiwa kutumia.
Siku ya shambulizi hilo, makomandoo hao waliruka kutoka katika helikopta hizo na kutua juu ya jumba la Osama wakiwa gizani baada kuzima taa za helikopta zote walizotumia.
Walinzi wa Osama walishtuka na kufyatua risasi kutoka katika paa la nyumba hiyo na walifanikiwa kuitungua helikopta moja kwa kutumia roketi.Maofisa wa Marekani walisema tukio hilo lilimshtua Rais Obama na kumkubusha tukio la mwaka 1993 la Somalia ambalo Black Hawk ilitunguliwa na kuua Wamarekani 18.
Makomandoo 24 waliruka uzio mrefu wa nyumba ya Osama wakaanza kutambaa na kuingia chumba hadi chumba wakimsaka. Walifanikiwa kumkuta akiwa katika chumba kimoja akiwa na watu wengine watatu akiwamo mmoja wa watoto wake wa kiume na mwanamke anayeelezwa kuwa ni mkewe.
Hata hivyo, Osama alikataa kujisalimisha huku mkewe huyo kwa kushirikiana na mtoto wa kiume wa Osama na watu hao watatu walijaribu kumuokoa kiongozi huyo wa mtandao wa ugaidi duniani kwa kukaa mbele yake. Wote waliuawa.
Baada ya kuuawa, mwili wake ulichukuliwa kwa helikopta ukiwa umening'inizwa na dakika 40 baadaye, ulizikwa baharini. Ikulu ya Marekani ulidai kwamba alizikwa kwa kufuata taratibu zote za Kiislamu.
Habari zinasema kuwa taarifa zilizofanikisha shambulizi hilo zilianza kupatika miaka minne iliyopita kutoka kwa wafungwa wa ugaidi katika Gereza la Guantanamo Bay baada ya kuteswa.
Wafungwa hao walimtaja, Khalid Sheik Mohammed kuwa ni mmoja kati ya watu wachache walioaminiwa kwa dhati na Bin Laden akisadikiwa kuwa ndiye aliyeandaa mashambulizi ya Septemba 11, 2001 Marekani na kuwa hakuwahi kutumia mawasiliano ya simu kwa miaka saba.
Mamia ya watuhumiwa ambao wengi wao ni kutoka Afghanistani na Pakistani wamewahi kuripotiwa kupata mateso makali, ikiwamo kulala ndani ya maji, kukoseshwa usingizi na kuwekwa katika vyumba vya kiza vyenye kelele.
Mwanzoni mwa mwaka huu, mtandao wa Wikileaks ulifichua mawasiliano ya siri yaliyoonyesha kwamba watuhumiwa wanaoshikiliwa katika gereza hilo walitoa taarifa kuhusu mmoja wa wasaidizi ambaye hupeleka taarifa na vifurushi kwa Bin Laden katika mji huo wa Abbottabad.
Maofisa wa CIA wanasema, awali Septemba mwaka uliopita, walipata taarifa nzito za uwezekano wa kuwapo Osama katika mapango huko Pakistani, lakini Februari mwaka huu maofisa upelelezi walipata uhakika wa makazi ya Osama na familia yake yalipo.
Wanaeleza kuwa mawakala wa CIA wa Pakistani walibainisha makazi hayo na kupachika kamera katika jengo hilo zilizowezesha kufuatilia mwenendo wa nyumba hiyo na kugundua kuwa familia inayoishi humo ni ya Osama Bin Laden.
Kwa mujibu wa CIA, ushahidi wa kwanza kwa kuwapo kwa Osama katika nyumba aliyokutwa ni wa sauti iliyorekodiwa akizungumza ambayo ilinaswa na mawakala hao wa CIA ambayo ilichunguzwa na kugundulika kufanana na sauti zake nyingine zilizorekodiwa siku za nyuma.
Baada ya hapo kamera zilizotegwa zilifanikiwa kupata picha ya Osama akiwa ndani ya nyumba hiyo na kupelekwa kwa Rais Obama Machi, 14 ambaye aliitisha mkutano wa kwanza wa siri kati ya mitano na washauri wa masuala ya ulinzi.
Uhusiano wa Pakistani, Marekani shakani
Kukamatwa kwa Bin Laden akiwa katika ardhi ya Pakistani kumeibua wasiwasi kuhusu mtazamo wa mataifa ya Magharibi na nchi hiyo, huku Serikali ya Pakistani ikisisitiza kwamba haikujua lolote kuhusu uwapo wa kiongozi huyo wa kigaidi katika eneo hilo.
Wanasiasa na wanataaluma walieleza kuwa ni vigumu kuaminika kwamba vyombo vyote vya upelelezi na vya usalama vya Pakistani havikuwa na taarifa yoyote kuwa kiongozi huyo wa kigaidi ambaye alikuwa akiishi umbali wa yadi 800 tu kutoka katika chuo maalumu cha kijeshi. Wachambuzi wanasema ushahidi wa kimazingira unaweza kuthibitisha kwamba Bin Laden alikuwa akiishi chini ya uangalizi wa Serikali ya Pakistani.
Rais Asif Ali Zardari alitoa utetezi kwa serikali yake jana akisema kuuawa kwa Bin Laden katika ardhi ya nchi yake si kigezo cha kushindwa katika mapambano ya serikali yake dhidi ya ugaidi. Katika safu ya maoni aliyoitoa kupitia Gazeti la Washington Post, Zardari alisema nchi yake “Ni moja wa waathirika wakubwa wa ugaidi duniani.”
Kwa mara ya kwanza, Zardari alieleza kwamba vikosi vyake vya usalama havikushirikishwa katika oparesheni hiyo lakini hakutoa maelezo ya kina kuhusu namna kiongozi huyo alivyoishi kwa amani jirani kabisa na Islamabad.
“Hakuwahi kutarajia kuwa atakuwapo katika eneo lolote, lakini sasa ameondoka.
Japokuwa matukio ya Jumapili hayakuwa ya ushirikiano wa pamoja, ushirikiano wa miongo kadhaa baina ya Marekani na Pakistani umechangia kummaliza Osama Bin Laden ambaye alikuwa tishio kwa ulimwengu wa wastaarabu,” alisema.
Maziko yaibua maswali mengi
Japokuwa sehemu kubwa ya dunia imekuwa katika shamrashamra za kifo cha kiongozi huyo wa al-Qaeda, maswali mengi yamekuwa yakiibuliwa kuhusu hatua hiyo, huku kukiwa hakuna taarifa zozote za kutolewa kwa picha zake baada ya kuuawa.
Hatua hiyo inaibua maswali mengi hasa kwa wapinzani wa Rais Obama, iwapo kweli Bin Laden ndiye aliyeuawa au ni hadaa.Hata hivyo, maofisa wa Marekani wamedai kwamba wana uhakika wa asilimia 99.9 kwamba waliyemuua ni kiongozi huyo wa al-Qaeda huku Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon yakieleza kwamba mwili wake ulizikwa kwa kufuata taratibu zote za Kiislamu ikiwamo kuoshwa kabla ya kupelekwa kwenye maji ya bahari ya Kaskazini mwa Uarabuni.
Maofisa wa Marekani walisema wamechukua hatua ya kuutupa baharini ili kuzuia kuwapo kwa kumbukumbu ya sehemu ya kaburi la kiongozi huyo wa al-Qaeda ambayo inaweza kutumika kama sehemu ya kumbukumbu kwa wafuasi wake.
Walisema pia ingekuwa vigumu kupata nchi yoyote ambayo ingekubali kupokea mwili wake kwa kipindi hicho kifupi wakisema sheria za Kiislamu zinaagiza mwili wa aliyeuawa uzikwe ndani ya saa 24 tangu kifo chake.
Rais Barack Obama na maofisa wa ngazi za juu wa Ikulu ya Marekani, jana kutwa nzima walikuwa wakijadili juu ya kuuonyesha hadharani mkanda wa picha za video zinazoonyesha maziko hayo.Maofisa hao hawakudhihirisha eneo halisi la bahari hiyo ambako wanajeshi waliubeba na kisha kuutumbukiza.
Lakini maofisa wa makao makuu ya jeshi la Marekani walisema kuwa mazishi hayo yalirekodiwa katika picha za video na zile za kawaida na pengine yataonyesha hadharani hivi karibuni.
Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Ugaidi cha Ikulu ya Marekani, John Brennan aliwaeleza waandishi wa habari kuwa utawala wa nchi hiyo bado uko katika mjadala mkali juu ya kuzionyesha au kutozionyesha picha za tukio zima la Osama ili kuwaridhisha wenye shaka juu ya ukweli wake.
Masheikh wametabiri kisasi dhidi ya maeneo muhimu ya Marekani kutokana na namna Serikali ya Marekani ilivyoamua kuuzika mwili wa Osama.

Monday, May 2, 2011
WASIFU WA OSAMA BIN LADEN
Osama Bin Laden
Osama bin Laden alizawa mwaka wa 1957, katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia. Ana zaidi ya mandugu na dada 50. Babake Osama alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi. Katika baadhi ya picha zake za utotoni, Osama ameonyeshwa akiwa na mavazi ya kifahari na ghali, akiwa likizoni katika miji mbali mbali barani Uropa.
Hata hivyo mwanzoni mwa miaka ya themaninialiyupia mgongo maisha haya ya starehe na kitajiri, ana kujiunga na vugu vugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan.
Na hapo akipigana pamoja na waarabu wenzake, ndipo alizindua kundi la kigaidi la Al qaeda. Mnamo mwaka wa 1998, alitangaza fatwa yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani. Kufuatia ghadhabu aliyokuwa nayo na Marekani, kwa kuweka majeshi yake katika ardhi ya kiislamu, katika nchi mbali mbali mashariki ya kati.
Alioa mke wake wa kwanza akiwa na miaka 17, na baadaye akawaoa ya wake wengine wanne. Osama Bin Laden naaminiwa kuwa na watoto 17.

Breaking News:::Osama bin Laden Auwawa Pakistan
Marehemu Obama bin Laden
Rais Barak Obama wa Marekani ametangaza sasa hivi kwamba adui namba moja wa nchi hiyo ameuwawa Jumapili hii (Usiku wa kuamkia leo Jumatatu)huko Islamabad, Pakistan, katika operesheni maalumu ya majeshi ya nchi yake iliyofanikiwa baada ya miaka kumi ya kumwinda mtu huyo mzaliwa wa Saudi Arabia. Marekani yote imelipuka kwa nderemo na furaha kwa habari hizi na hivi sasa nchi nzima inasherehekea.

Subscribe to:
Posts (Atom)