Na Haruni Sanchawa
MCHUNGAJI Ambilikile Masapile (pichani) wa Kijiji cha Samunge, Loliondo amebadili upepo na sasa yupo ‘bize’ kujenga nyumba yake.
Chanzo chetu cha habari kijijini hapo, kilisema Babu amekuwa akijenga nyumba yake baada ya wateja kupungua.
“Wateja wa Babu wamepungua sana wengi wanaokuja wanatoka nje ya nchi. Hivi sasa siyo yule ambaye alikuwa akifanya kazi mpaka usiku. Muda mwingi anakuwa akijenga, ni mtaalamu wa ujenzi,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilipoulizwa kwa wastani Babu anatibu watu wangapi, kilisema si wengi sana. “Siyo vizuri kusema idadi, lakini ukiona mtu anaacha tiba na kwenda kujenga elewa kwamba wateja ni wachache sana,” kilisema.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wanaomzunguka Babu wanamshukuru kwa sababu kawaletea maendeleo.
“Hivi sasa tuna minara ya mitandao, barabara kutoka Arusha imetengenezwa kwa ajili ya Babu, tunamshukuru sana. Hata akibadili upepo na kuamua kuendelea na fani ya ujenzi, sisi hatumlaumu.
Sasa afanye nini na wateja hawaji kwa maelfu?” alisema mwanakijiji mmoja aliyeomba jina lake kuhifadhiwa.
Mchungaji Masapile amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kudai kuoteshwa dawa na Mungu ambayo alisema inatibu magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi
This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Tuesday, July 26, 2011
Waliokunya Vikombe vya TIBA Wamejisumbua BUREEEE!!!!
Elvan Stambuli na Makongoro Oging'
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (pichani) amepasua jipu na kusema hakuna utafiti wowote wa kisayansi uliothibitisha kuwa dawa za asili zina uwezo wa kutibu Ukimwi.
Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo wakati anazindua Kituo cha Matibabu ya Wagonjwa wa Ukimwi na Mafunzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waziri Mponda ameyasema hayo huku maelfu ya watu wakiwa tayari wamekunywa tiba ya mitishamba ya vikombe inayotolewa na watu mbalimbali akiwemo mwanzilishi wake, Mchungaji Ambilikile Masapile, maarufu ‘Babu’ wa Kijiji cha Samunge, Loliondo aliyedai kuoteshwa na Mungu kutibu magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.
Magonjwa mengine aliyotaja kuwa yanatibika kwa mitishamba kwa dozi ya kikombe kimoja ni kisukari, shinikizo la damu, kifafa pamoja na magonjwa mengine yanayosumbua katika tiba za kisayansi.
DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA
Dk. Mponda alisema wagonjwa wa Ukimwi wanatakiwa kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV) na akawataka waende kwenye vituo vya afya kupewa.
Aliongeza kuwa vituo vyote vya afya vinatoa dawa za ARV lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania mwenye tatizo la Ukimwi anapata dawa hizo mahali alipo.
Alisema kuna vituo 50 vya afya ambapo 30 ni vya serikali na 20 ni vya watu binafsi ambavyo vinatoa msaada kutoka kwa wadau wa maendeleo.
“Wagonjwa wanaokwenda kupata tiba asili waache kwa kuwa bado zinafanyiwa utafiti,” alisisitiza waziri na kuzua minong’ono kutoka kwa watu waliokuwa wakimsikiliza wakisema ina maana waliokunywa wamejisumbua.
Akifafanua zaidi, Waziri Mponda alisema dawa hizo za mitishamba zinafanyiwa utafiti katika Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Aliongeza kuwa kuna waathirika 110,000 wanaoishi na virusi vya Ukimwi na kati yao 72,000, wanaendelea kutumia dawa za ARV na kwamba hayo ni maendeleo katika kupambana na ugonjwa huo.
TAHARUKI
Tamko hilo la Waziri Mponda limesababisha taharuki kubwa kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakipiga simu katika ofizi za gazeti hili wakidai kuwa serikali imechelewa mno kutoa tamko hilo.
“Watu wengi wameuza mali zao ili waweze kutibiwa kwa mitishamba inayotolewa kwa kikombe sehemu mbalimbali nchini, serikali inapojitokeza sasa na kusema haitibu, inatushangaza, wengi wameumia tayari,” alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la John, mkazi wa Arusha.
Mara baada ya tiba hiyo ya Babu kutangazwa, mawaziri, baadhi ya wakuu wa mikoa, makamanda wa jeshi na wananchi walifurika kwa mzee huyo na watoa tiba wengine wa vikombe huko Tabora, Morogoro, Mbeya na Iringa kupata dawa.
Baadhi ya mawaziri, waliokunywa dawa hiyo ya mitishamba ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira na wabunge Nimrodi Mkono (Musoma Vijijini) na Augustine Mrema (Vunjo), Rose Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yohana Balele na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro.
ASILI YA DAWA YA BABU
Mchungaji Masapile aliwahi kuulizwa kuhusu asili ya tiba yake, akasema : “Asili ya dawa hii ni Mungu mwenyewe, mti ni wa kawaida kama miti mingine ila Mungu ameweka neno lake ndani ya mti, hivyo neno ndilo linaloponya.”
Hakuishia hapo, alisisitiza kuwa Mungu akitoa neno lake ndani ya mti huo, basi mti hautakuwa na nguvu hiyo ya uponyaji. Hata hivyo, hadi sasa Babu hajatoa tamko kuueleza umma kuwa Mungu ametoa neno lake ndani ya mti huo au la na wananchi wachache wanaendelea kwenda kupata kikombe licha ya vifo kuongezeka kila kukicha.
WAZEE WA SAMUNGE
Aidha, baadhi ya wazee wa Samunge waliowahi kuzungumza na wanahabari kwa nyakati tofauti walidai kuwa mti huo anaotumia Babu kutibu watu una majina mawili ambayo ni Mgamryaga na Mbaghayo na walisema unapatikana kwa wingi katika Mlima Mwegari kijijini hapo.
Walidai kuwa mti huo ulikuwa ukitumika kama kinga ya kansa kwa kuuchemsha na kunywa supu yake na pia ulikuwa ukitibu baadhi ya magonjwa ya wanyama.
Lakini walitoa angalizo kuwa hapo kwao hakuna waganga wa kienyeji pengine katika jitihada ya kusititiza kwamba yanayotokea huko siyo masuala ya kishirikina kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodai.
Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakipinga tiba hiyo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe alimuambia mwandishi wa habari hii kuwa dawa za vikombe vyote inayotolewa sasa kama tiba ni mambo ya shetani.
Alinukuu aya ya Biblia Wakorintho 1;10 msitari wa 14-22 ambayo inasema Wakristo wanaoshiriki meza ya Bwana na kukinywea kikombe cha Bwana kamwe wasishiriki kikombe cha mashetani.
“Kwa hiyo kinachofanyika Loliondo ni ushirikina na ni kazi ya pepo wa uaguzi,” alisisitiza Askofu Kakobe

Monday, July 25, 2011
KWANINI MIAKA SABINI Je umejipangaaje?
Hapo mwanzo Mungu aliumba ulimwengu na wanyama wake. Kila mnyama alipewa
miaka ya kuishi 30. Kati ya wanyama walioumbwa walikuwa Punda, Mbwa na
binadamu. Mungu akawauliza wanyama hao Je! unadhani miaka hiyo thelathini
inakutosha? Kila mmoja akajibu hivi:
Punda: Mimi nikae nikitumikishwa miaka 30, niwe kihongo miaka yote hiyo?
Loh! kazi hiyo ni kubwa sana . Mimi nipunguzie iwe miaka 10 tu inanitosha
bwana.
Mungu: Sawa wewe utaishi miaka kumi tu.
Mbwa: Mimi nikae nikilala nje miaka thelathini! Kula majalalani, kubweka
usiku kucha. Naomba unipunguzie niishi miaka kumi tu inanitosha.
Nitajitahidi kwa kipindi hicho kulala nje, kubweka na kulinda usiku kucha.
Watanitumia wapendavyo kunusa madawa ya kulevya, kukamata wanyama nk.
Mungu: Sawa, umri wako utakuwa miaka kumi.
Binadamu: Ha! Miaka 30 tu, nita enjoy nini mimi? Niongezee bwana.
Mungu: Sawa, niliyoipunguza kwa punda na mbwa utaongezewa wewe. Nawe
utaishi miaka sabini (30 + 20 + 20 = 70). Kipindi chako cha miaka 30
utaishi maisha yafaayo binadamu, miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na
maisha ya punda, na miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na maisha kama ya
mbwa.
Binadamu: Ahsante sana bwana na iwe kama ulivyosema.
Miaka 0 – 30+: Maisha mazuri sana (hayo ndiyo maisha ya binadamu). Maisha
ya kutafuta marafiki, maisha ya kulishwa, maisha ya kuwaandikia barua girl
friends na boy friends, kutafuta pen pal. Maisha ya kuangalia mtindo mzuri
wa nguo, nywele, kutembea kwa mikogo, kutuma message kila dakika,
kupigiana simu kila saa, ugomvi usio na kichwa wala miguu, kujifunza
kuvuta bangi, kunywa pombe, kuhudhuria madisco n.k.
Miaka 35 – 50: (Maisha ya punda). Wengi wanajitegemea wameoa au kuolewa.
Maisha magumu, unapanga chumba lakini mhh kodi sasa watoto watano na mke
chumba kimoja, kibarua wa kubeba zege, kimbiza shilingi, huna muda wa
kwenda disco tena au kuangalia mitindo mipya, hakuna kulala hapa. Watoto
wanasumbua shule, wanaumwa, kadi nyingi za harusi, madeni hadi unawakimbia
marafiki zako. Hii itaendelea hadi upite umri wa miaka hamsini.
50+ tuseme 60: Mstaafu. Unakaa nyumbani, unalinda boma (maisha ya mbwa),
nyumba imebomoka huna pesa ya kurepair, nyumba inavuja, watoto wote
wameondoka wanahangaikia maisha yao na wake/waume zao. Huna jinsi wewe ni
kama mlinzi wa eneo ulilochagua.
Je! Katika maisha haya upo kundi gani? Jiandae hatua unayoendea ni ngumu
zaidi. Jipange, wakati ni huu.
JIPANGE SAWASAWA!!

Tuesday, July 19, 2011
Monday, July 18, 2011
He! Wake watano! Hii imezidi kawaida!!!
MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Nurdin Mohammed ‘Chekbudi’ (29), katikati ya wiki hii amefunga ndoa yake ya tano na mwanamke anayejulikana kwa jina la Mariam, ikidaiwa kuwa ni mke wake wa tano.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Chekbudi alifunga ndoa hiyo saa 2:00 usiku wa Julai 6, mwaka huu katika Msikiti wa Magomeni Kichangani, Dar es Salaam, siku chache baada ya kutifuana na mkewe, Leila Juma (pichani)2.
Habari zinasema kuwa Chekbudi akiwa katika harakati za kufunga ndoa alimfuata Leila anayeishi Ilala kwa ajili ya kumpa taarifa za kuoa mke wa pili lakini wakashindwa kuelewana na Chekbudi kuishia kumpiga mkewe huyo na kumjeruhi jichoni.
Inadaiwa kuwa, chanzo cha msanii huyo kumpiga mkewe ni pale mwanamke huyo alipotaka wagawane mali walizochuma ikiwemo gari analoliendesha msanii huyo ambalo linadaiwa kuwa ni mali ya Leila.
Baada ya kichapo hicho, Leila alikwenda kufungua jalada katika Kituo cha Polisi cha Mango Garden Kinondoni, shitaka likisomeka SHAMBULIO LA MWILI namba RB/ GARD/RB/504/2011.
Jitihada za Chekbudi kuomba suluhu ya kesi hiyo zilishindikana na kumfanya mke huyo kumsaka msanii huyo na polisi baada ya ndoa yake na kuwa ‘honeymoon’.
Kwa mujibu wa rekodi za uoaji za msanii huyo, mwanamke aliyemuoa juzi ni wa tano. Wa kwanza alikuwa Mwanaidi ambaye alishiriki Miss Kurasini mwaka 2001, hata hivyo, hakudumu naye.
Mwingine ni Zamzam aliyetemana naye na kumfanya kuangukia kwa mama mmoja wa Kiarabu anayeishi Tabata, Dar, ambaye inadaiwa bado wako pamoja.
Siku ya sita ndani ya Mwezi wa Ramadhani mwaka 2010, Chekbud alifunga ndoa nyingine kwa siri na Leila.
Mwandishi wetu alipozungumza na Leila alikiri kuwa ni mke wa Chekbudi na kusema kuwa ni kweli anamsaka na RB baada ya kumjeruhi.
Mwandishi wetu alimtafuta msanii huyo siku ya pili baada ya kuoa ili kuweka wazi suala hilo lakini simu yake ya kiganjani haikupatikana.
Vituko vya Mastaa wa KIbongo
STAA wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba ‘The Great’ (pichani), amezua mjadala vichwani mwa wadau wa burudani ndani ya Ukumbi wa Bilicanas Posta, Dar es Salaam baada ya kunaswa usiku wa manane akiwa na mrembo aliyedai kuwa ni mchumba wa mtu ambaye jina halikupatikana.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu, Kanumba alikuwa ‘bize’ na kimwana huyo kiasi cha kuonekana walikuwa na uhusiano zaidi ya kuwa mtu na shemejiye wakati Bendi ya African Stars international ‘Twanga Pepeta’ ikiporomosha burudani ukumbini humo.
Wawili hao walikuwa wakichombezana kwa utundu huku vicheko na tabasamu vikichukua nafasi kiasi cha wadau wa burudani kuhisi kuwa wawili hao wana la ziada.
Awali, paparazi wetu alimshuhudia Kanumba akifika ukumbini humo saa 7:09 usiku, akiwa ameongozana na baadhi ya rafiki zake na kwenda kuketi kwenye kona moja iliyopachikwa jina la Bongo Movie.
Akiwa pande hizo, staa huyo aliagiza vinywaji na baadaye kucheza muziki na marafiki zake. Baada ya muda akatokea dada huyo na kuwa naye sambamba.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mapozi ya wawili hao yalizidi kuzua utata hasa kwa kimwana huyo kujisahau kama wako mbele ya kadamnasi na kupitisha mikono yake katika maungo ya Kanumba.
Baada ya kuona mapozi yamezidi, paparazi wetu alimfuata Kanumba na kumuuliza kuhusiana na ukaribu wake na msichana huyo.
“Aaah! Huyu ni rafiki yangu lakini tena ni mchumba wa mtu, sioni ubaya kufurahia naye hapa ukumbini na mapozi yote haya ni kuonesha furaha tuliyonayo,” alisema Kanumba.
Hata hivyo, paparazi wetu alimtaka Kanumba afunguke kama kimwana huyo ni mbadala wa mchumba’ke waliyemwagana, Miss Ilala 2009, Sylvia Shally.
“Mmmh! Siwezi kuweka wazi sana lakini kama unavyoona, tunapeana kampani tu,” alichezesha taya huku akipiga hatua kumpotezea ‘vuvuzela’ wetu.
Baadaye kila mmoaja alichukua hamsini zake
TR 6 Session 3
Unamfahamu huyu?
Kulwa Laurent akifanya vitu vyake!
Yupo Biiiiiizeeeh!
Mr. Mbise akifanya mamboz!
Huyu nae anapenda sana mgongo mgongo, si unamuona?
Mkono shavuni!!
Miss Photogenic. Pose No.1
Miss Photogenic. Pose No.2

Friday, July 8, 2011
Bei za Mastaa wa Kibongo
Na Mwandishi Wetu
Kwa jicho la juu, warembo mastaa muonekano wao ni bei mbaya a.k.a expensive, wapo wanaovunja benki ili kuwanasa bila kujua siri nzito iliyopo, kumbe asilimia 90 ni bei chee.
Ingawa wapo wenye misimamo yao na wasiozuzuka na ‘usistaduu wa kideoni’, idadi kubwa ya mastaa wanaotibua ‘kitaani’ na kwenye vyombo vya habari ni sababu ya tasnia nzima kuingia doa.
Ijumaa ‘The Udaku Master’, kupitia uchunguzi wake limebaini makundi matatu ambayo warembo hao wameyatengeneza, mosi likiwa la wale wanaojiheshimu (watulivu, wenye msimamo), pili ni la wale bei mbaya ‘expensive’ (kuwapata inabidi ujipinde), tatu lenye memba wengi ni la bei chee.
Ripoti ya Ijumaa pia ina kundi la warembo ambao pamoja na kwamba hawakuwekwa kwenye kundi lolote kati ya hayo matatu lakini tabia na vitendo vyao vimekuwa vikitia ‘kinyaa’ na kusababisha jamii iwashushe hadhi.
WANAOJIHESHIMU
Mastaa ambao mpaka sasa wameonesha msimamo na wanajiheshimu ni Malkia wa Afro Pop Bongo, Judith Wabura ‘Lady Jaydee’, (aliyepakatwa na mumewe pichani) mtangazaji nyota aliye pia mwanamuziki, Fina Mango ‘Ndege Mnana’ na staa wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’.
Wengine wenye msimamo ambao hawajanaswa na skendo ya aina yoyote mpaka sasa ni mtangazaji Zamaradi Mketema, mrembo aliyetisha kwenye Hip Hop, Zainab Lipangile ‘Zay B’, Miss Tanzania 2007/08, Richa Adhia na Miss Tanzania namba mbili 2006/07, Jokate Mwegelo.
Wapo wengine wanaoonekana wanajiheshimu lakini Ijumaa limewaondoa baada ya kubaini kasoro zao za chini chini, huku baadhi likitaka kujiridhisha zaidi.
BEI MBAYA
Kundi hili, linaundwa na mastaa wenye msimamo kwa wanaume ‘makapuku’ lakini ni wepesi mbele ya wafanyabiashara na wanasiasa wanaojua ‘kukata mpunga’.
Ingawa majina yao yanahifadhiwa kwa sasa, Ijumaa lina orodha ya mastaa 13 ambao wamekuwa wakigawa mapenzi kwa wanaume matajiri kwa matarajio ya kupata malipo makubwa.
Hata hivyo, baadhi yao wamejikuta wakiaibika baada ya kunyang’anywa magari ambayo walihongwa na wanaume kama malipo ya kuwapa mapenzi ya ‘nipe nikupe’.
BEI CHEE
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, mastaa wengi wanaounda kundi kubwa ni bei chee kwa sababu hutoa penzi ama kwa gharama nafuu au bure ili kutimiza matakwa yao ya kuwa maarufu.
Ijumaa limebaini kwamba, warembo wengi hasa waigizaji, hujirahisi kwa maprodyuza mastaa ili wapate kuonekana kwenye filamu zinazotengenezwa.
Prodyuza mmoja aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa warembo wengi kabla ya ‘kuuza’ sura kwenye filamu mbalimbali, huwapa ofa ya unyumba baadhi ya maprodyuza.
“Hii ipo wazi kabisa, tasnia inaundwa na watu wengine hatari kabisa. Baadhi yao walikuwa hawajatulia huko mtaani na wengine wameshindwa maisha, kwa hiyo kutoa unyumba kwa prodyuza ili watoke hawaoni kazi.
“Ni wengi sana wanajirahisi. Unaweza kuwaona ni mastaa kwenye filamu lakini nje wanatongoza wanaume ovyo,” alisema prodyuza huyo (jina tunalo).
Ukiachana na prodyuza huyo, hivi karibuni gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda liliandika habari ya staa mmoja wa filamu kumpigia simu mbunge wa jimbo moja la Morogoro na kumuomba wawe pamoja.
Mbunge huyo aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mrembo huyo alikuwa anamheshimu lakini alimshusha thamani baada ya kumtongoza bila aibu.
Aidha, Ijumaa inaifanyia kazi orodha ya mastaa 22 ambao wanatajwa kuwa kimeo kuliko wengine kwa kuwa na tabia ya kutongoza au kujitongozesha kwa wanaume.
KUNDI LINALOCHAFUA TASNIA
Uchunguzi umebaini kuwa, mastaa wanaoongoza kwa skendo, wamekuwa wakichafua hali ya hewa na kusababisha hata wengine wanaojiheshimu waonekane hawana maana.
Staa wa filamu, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ anatibua hali ya hewa kutokana na skendo zake za waume za watu pamoja na ile ya kufumwa chumbani akiwa na mchumba wa mtu mwaka juzi.
Aunt alifumwa akiwa na brazameni, Mwilu Mwilola ‘Silvanus’ ambaye alikuwa mchumba wa msanii, Sara Mwakapala. Hivi sasa Aunt na Silva ni wapenzi wa kudumu.
Skendo za Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu kubadili wanaume mara kwa mara na ‘kashkash’ za kukamatwa na polisi, ni baadhi ya vitu vinavyochafua ‘statas’ ya ustaa ndani ya ‘Bongoland’.
Mastaa Jacqueline Pentzel, Jacqueline Patrick, Blandina Chagula ‘Johari’, Sylvia Shally, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na wengineo wengi pia wanatajwa kuwa sehemu ya ‘uchafuzi’ wa hali hewa katika tasnia kutokana na skendo zao za hapa na pale.

Mambo ya Kuchimba Dawa!!!
Na Issa Mnally
Mrembo mmoja ambaye alikataa kutaja jina lake, hivi karibuni alitoa kali ya mwaka baada ya kunaswa ‘akichimba dawa’ hadharani.
Tukio hilo lisilo la kawaida lilitokea Bungoni, Ilala jijini Dar es Salaam saa 9.30 usiku karibu na Baa ya Max kulikokuwa na onesho la kundi moja ya taarab.
Awali, mrembo huyo alikuwa akiburudika na miondoko ya rusha roho iliyokuwa ikiporomoshwa ukumbini humo ambapo onesho hilo lilipoisha alitoka nje.
Muda mfupi baadaye, paparazi wetu aliyekuwa eneo hilo alimuona mrembo huyo akielekea kwenye mlango wa choo wa baa hiyo na kutaka kuufungua lakini akakuta umefungwa ndipo alijongea kwenye lori lililokuwa karibu, akamaliza shida zake.
Alipomaliza kufanya zoezi hilo, paparazi wetu alimfuata na kumhoji kwa nini alifanya vile sehemu isiyohusika, akajitetea kwa kusema kuwa alizidiwa na kumwomba asimtoe gazetini kwani ataaibika.
“Chonde chonde kaka yangu, sikuwa na jinsi, nilizidiwa,” mrembo huyo alijitetea.
Subscribe to:
Posts (Atom)