Thursday, December 29, 2011

TID - Hanitaki (Official Video)

Upepo mkali wapeperusha vitu na watu huko Blackpool Uingereza

Waves whipped up by high winds crash against Blackpool promenade on Dec. 28, in Blackpool, England. Most of the North West is bracing itself against high winds but the brunt of the gusts are hitting Scotland with road closures and sporting events being postponed

Muone huyu mdada utadhani kaweka style ya Nwele kumbe ni kazi upepo hadi anaonekana hivyo, uso wote umefichwa na nywele wima, Duh si mchezo ati!

Ndege yaanguka na kushika moto wakati ikitua

Waokoaji wakiwa karibu na ndege ya abiria aina ya Tupolev 134 (juu na chini) iliyotengenezwa Urusi (Russia) ambayo ilianguka nje kidogo ya mji wwa Osh huko Kyrgyzstan jana Jumatano Desemba 28, 2011. Iliwaka moto mara baada ya kuanguka wakati ikitua. Mashuhuda walisema walijeruhiwa watu sita, hakuna aliekufa.


Wednesday, December 28, 2011

Kampuni ya Honda yaanza kuzisaga/kuziharibu gari zilizoharibiwa na mafuriko huko Thailand

Jionee mwenyewe zilivyoharibika kwa mafuriko

hapa zione kwa karibu zaidi

Gari limebebwa juu juu kupelekwa katika mtambo wa kusagia magari

Hapa gari likisagwa na mtambo maalum kiwandani

Nimependa alivyo simpo-Barrack Obama

Rais wa Marekani Barrack Obama akiwa amemshika binti yake Milia (kulia) na Sasha (kushoto) wakati akitoka Sea Life Park ambayo ni mbuga ya wanyama wa baharini jana Desemba 27, 2011huko Waimanalo Hawaii

Treni ya mizigo yasombwa na mafuriko huko Australia

Treni ya mizigo ikiwa imesombwa na mafuriko karibu na kijito cha Edith katika mji wa Katherine jana Desemba 27, 2011 nchini Australia

Tuesday, December 27, 2011

Ngazi za umeme zaboresha usafiri katika jiji nchini Colombia

Natamani zingekuja na hapa Tanzania haswa maeneo ya Usambaani na Upareni kwenye milima
Msichana akipanda ngazi za umeme huko Comuna 13 karibu na Medellin nchini Colombia jana Desemba 26, siku ambayo zilizinduliwa.Ngazi hizi ni za kwanza za aina yake katika mji huo wenye visa vingi vya ubabe na kutumia nguvu. Na zimekuja kuwa mbadala wa zile za zege 350 zilizokuwepo awali.

Mama huyu naye anazitama ngazi hizo kwa mbele chini, zinapamba mji pia kusema ukweli

Luis Holguin (Kushoto) na binti yake Refsa wakipandishwa na ngazi hizo. Ni raha sana

Watoto nao wakijinafasi katika ngazi hizo

Muonekano mpana zaidi wa ngazi hizo. Jueni kwamba huduma hii ni BURE. Hulipii chochote.

Jengo lalipuka huko China-Ila sio kwa Bomu bali limetitia/poromoka

Jengo kongwe la ofisi lenye urefu wa mita 80 kwenda juu, likiporomoka siku ya X-Mass December 25, 2011 huko Kunming katika jimbo la Yunnan nchini China

Vumbi kubwa likitimuka mara baada ya jengo hilo kuanguka

Wananchi wakipita kando ya mabaki ya jengo hilo

CCTV-9 report: Solar bottle lights in the Philippines

Tuesday, December 20, 2011

Babu Ambilikile hatarini!!



CHAKULA NDIYO CHANZO CHA MARADHI YANAYOTUSUMBUA


CHAKULA ni dawa, lakini chaweza kuwa sumu pia. Katika makala yetu ya leo tunazungumzia namna ambavyo chakula kimekuwa chanzo cha maradhi mengi sugu yanayotusumbua binadamu hivi sasa.
Vijana wengi wanapoteza uhai wakiwa bado vijana, maradhi kama shinikizo la damu (presha), saratani, kiharusi, kisukari, magonjwa ya miguu na migongo, yamekuwa sawa na ni wimbo wa taifa.

Asilimia kubwa ya magonjwa yanayotusumbua, kama vile shinikizo la damu (Low and High Blood Pressure), Magonjwa ya moyo (Cardiovascular diseases), saratani (cancer), ambayo ndiyo mengi, yanatokana na vyakula tunavyokula kila siku au tunavyoacha kula kama inayotakiwa.

Ukiangalia katika muongozo wa vyakula (Food Guide Pyramid) ambao unatuonesha kundi lipi la vyakula tunatakiwa kula kwa wingi na kundi lipi tunatakiwa kula kidogo, katika maisha halisi tuliyonayo, utaona muongozo huo umegeuzwa, miguu juu, kichwa chini.

Hii ina maana kwamba vyakula ambavyo tunapaswa kula kwa wingi tunakula kidogo au kwa nadra sana na vyakula ambavyo tunapaswa kula kidogo na kwa nadra ndiyo tunakula kwa wingi na karibu kila siku.

VYAKULA TUNAVYOTAKIWA KUVILA KWA WINGI
Katika muongozo huo wa vyakula, ambao unatambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), unaorodhesha vyakula vitokanavyo na nafaka kama vile mchele, ngano, mahindi, uwele, mtama, n.k, kama vyakula tunavyotakiwa kuvipa kipaumbele katika milo yetu ya kila siku kwa kuvila kwa wingi.

Tukizungumzia maisha ya Kitanzania, vyakula maarufu vitokanavyo na nafaka hizo, ambavyo vinatumiwa na familia nyingi ni ugali, wali, mikate, tambi, makande, uji, n.k. Uzoefu unaonesha kuwa familia nyingi za Kitanzania zinatumia ugali, wali na mikate, uji karibu kila siku katika milo yao, lakini tambi, kande na vingine vya jamii hiyo, huliwa mara moja moja.

TATIZO LIKO WAPI?
Ikiwa familia nyingi zinakula ugali, wali, mikate na maharage kila siku kama muongozo wa vyakula unavyotukata, tatizo liko wapi? Tatizo lipo, tena kubwa na familia nyingi zinaathirika nalo kwa kukosa elimu ya kutosha kuhusu vyakula wanavyokula. Kweli wanakula ugali, mikate, lakini VIMECHAKACHULIWA!

UGALI
Familia nyingi zinapopika ugali zinatumia unga mweupe, wenyewe wanaita sembe safi nyeupe, wakiamini kwamba huo ndiyo unga bora wakati siyo kweli.
Ili upate faida ya nafaka kwa kula ugali, ni lazima iwe nafaka ambayo haijaondolewa viini lishe vyake na ili vipatikane viini lishe hivyo, mahindi hayatakiwi kukobolewa bali yanatakiwa kusafishwa na kusagwa hivyohivyo.
Halikadhalika mtama na uwele.

Mahindi yaliyosagwa bila kukobolewa ndiyo yanayotoa unga safi na bora kiafya, unga huo ndiyo unaojulikana kama dona.
Kwa kutumia unga huo, iwe kwa kupika ugali au uji, utakuwa umepata faida ya kula vyakula vitokanavyo na nafaka kama inavyoagizwa kwenye muongozo wa vyakula. Ulaji wa ugali ama uji uliotokana na sembe nyeupe ni sawa na kula chakula kilichochakachuliwa!

MIKATE
Kama ilivyo kwenye ugali, tatizo hilo lipo pia kwenye mikate inayotumiwa na familia nyingi mijini karibu kila siku. Mikate inayoliwa na watu wengi ni hii inayotengenezwa kutokana na nafaka ya ngano, lakini kwa bahati mbaya nayo huwa imechakachuliwa na kukosa faida ya ngano kiafya.

Mkate unaopendwa na kuliwa sana ni mkate mweupe, huu hutengenezawa kutokana na ngano iliyokobolewa na kwa maana hiyo kiafya hauna ubora, kwa sababu viini lishe vyake vimeondolewa na mbaya zaidi hutiwa sukari kunogesha ladha.
Licha ya kasoro hiyo, mkate mweupe umeendelea kuwa chaguo la kwanza na mlo wa kwanza katika familia nyingi duniani.

Ingawa kuna aina mbili ya mikate, lakini aina moja ndiyo inayopendwa na watu wengi zaidi kuliko aina nyingine ambayo hutengenezwa kutokana na ngano isiyokobolewa, aina hii huitwa mkate mweusi au ‘brown bread’

Waranti kumkamata makamu wa rais wa Iraq


Iraq's Sunni Arab vice president Tariq al-Hashemi speaks during a Press conference about the upcoming elections in Baghdad, Iraq, on Wednesday, Nov. 18, 2009.  al-Hashemi vetoed part of a key election law, throwing national polls slated for January and a planned U.S. troop draw-down into question. (AP Photo/Karim Kadim)
Makamu wa rais wa Iraq, Tareq al-Hashemi 

 

 Iraq imetoa waranti ya kumkamata makamu wa rais wa nchi hiyo Tareq al-Hashemi, kwa madai ya kuhusika na ugaidi.

 
Kwa mujibu wa duru za usalama na sheria, waranti hiyo imetolewa na kamati ya mahakama kuambatana na sheria za kupiga vita ugaidi. Wakati huo huo, wizara ya mambo ya ndani mjini Baghdad imesema, walinzi wa Hashemi wamekiri kupanga na kufanya mashambulio. Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya Iraq, watu hao walipewa fedha na walihakikishiwa kuungwa mkono na al-Hashemi. Makamu huyo wa rais wa madhehebu ya Kisunni, ni mpinzani na mkosoaji mkali wa Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ambae ni wa madhehebu ya Kishia.

Monday, December 19, 2011

"Hhmm...- CPwaa.VOB-Video ina ubora wa hali ya juu

BARCELONA YATWAA KOMBE LA KLABU BINGWA DUNIANI

Lionel Messi akishangilia na mchezaji mwenzake, Daniel Alves (2) baada ya kuifungia timu yake bao dhidi ya Santos katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Duniani iliyopigwa Yokohama, Japan leo. Barcelona imeshinda bao 4-0

GLOBAL

Cesc Fabregas akiifungia Barcelona bao la tatu dhidi ya Santos katika fainali ya Klabu Bingwa Duniani iliyopigwa Yokohama, Japan leo. Barcelona imeshinda bao 4-0.

Baada ya David Kafulila kuvuliwa Uanacha NCCR-Mageuzi, Zito atoa kauli;


Kwanini FUNGATE/HONEY-MOON ukafanyie kitanda cha GEST badala ya CHAKO nyumbani kwenu????



WAUMINI wa Kikristo wametakiwa kulala kwenye vitanda vya nyumbani kwao na si vya nyumba za wageni (gesti) wakati wa FUNGATE/HONEY MOON, mara baada ya sherehe za harusi ili kuepuka tabia ya kufanya ngono hovyo hovyo na kuzizoea Gesti kupaona pa kawaida sana.
Haya yalisemwa na Mchungaji Elieza Masoud kutoka Mbeya ambaye alihudhuria harusi ya rafiki yake Mchungaji Thomas Paul wa Usharika wa Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) Mji Mpya katika Manispaa ya Morogoro ambaye amefunga pingu leo (Jumapili).


"Nashangaa sana, utaona mkazi wa maeneo ya Mji Mpya anaacha kitanda chake kizuri anakwenda kulala kwenye nyumba ya wageni inayopaswa kulala mimi mgeni kutoka Mbeya.  Hii yote ni watu kukosa uelewa katika somo hili la harusi.  Wanalichukulia kama maigizo  ya Kanumba (mcheza sinema Steven)," alisema mchugaji huyo ambaye  baada ya kumtaja Kanumba waumini wote waliofurika kwenye ibada hiyo waliangua vicheko

Akifafanua zaidi, mtumishi huyo wa Mungu alisema hali hiyo inatokana na watu kushindwa kuzidhibiti nafsi zao
zilijojaa tamaa nyingi na kukosa hofu ya
Mungu.
Maoni ya Mhariri/Mwenye Blogu:
Hii ni kweli tena ni muhimu sana. Ndoa yangu niliyofunga Juni 14, 2003 nilifanyia FUNGATE/HONEY-MOON kwenye kitanda changu nyumbani. Sikuona HESHIMA kumpeleka mke wangu mpendwa na kufanya nae TENDO LA NDOA katika KITANDA CHA WOTE huko Gesti, Hoteli, Lodge au vyovyote utakavyoita. 

Kuanzia Maigizo ya ITV hadi Degree Marekani

 Mdau na mpiganaji machachari Idd Ligongo,aliewahi kuwa muigizaji ktika michezo ya ITV hapa Tanzania hivi juzi kati alikula Nondozzz  ya "master of arts in communication," kutoka chuo kikuu cha Wichita State University, kilichopo Jimboni Kansas, nchini Marekani.

Mpiganaji Ligongo  baada ya kuchukua cheti chake

Mdau akiwa na mai waifu wake Mary-Mzubwa Ndaro, hii inakuwa kama vile mdau karudisha bao baada ya mai-waifu wake kula nondo toka chuo hicho hicho hivi karibuni

Thursday, December 15, 2011

MAKALA YA MAISHA YA MR EBBO!

MAKALA YA MAISHA YA MR EBBO!

MGOMO WA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM


Wanafunzi hao waliokuwa wanaendeleza mgomo wao ulioanza Jumatatu wiki hii wakidai taarifa za kwa nini pesa zao zinachelewa wakati bodi ya mikopo, ilishasema wamezileta chuoni hapo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu na uvunjifu wa amani chuoni hapo tangu mwanzo wa juma hili.


“Desemba 13 (Jumanne) Kamati ya Wakuu wa Chuo na Shule Kuu zilizoko kampasi kuu ya Mlimani walifanya kikao cha dharura na kufanya mapendekezo kuhusu hatua za kuchukuliwa ili kusitisha uhalifu chuoni,”alisema Mukandala na kuongeza:

“Siku hiyo hiyo Baraza la Chuo nalo lilifanya kikao cha dharura na kutathimi mwelekeo wa chuo na kupitia mapendekezo yaliyoletwa na Kamati ya Wakuu wa chuo na shule kuu na kutoa maamuzi.”. Profesa Mukandala alisema, maamuzi yaliyotolewa na vikao hivyo ni pamoja na kuwafukuza wanafunzi hao 43 na kuchukua hatua za kuongeza ulinzi kwa muda katika maeneo muhimu ya chuo ili wanafunzi walio wengi waendelee kusoma bila kusumbuliwa.

Alisema kati ya wanafunzi hao 43, wanafunzi wanane ni wale ambao walisimamishwa masomo kwa muda wa miezi tisa, lakini waliendelea kuonekana maeneo mbalimbali ya chuo hicho huku wakilazimisha kuonana na uongozi. “Kuna hawa 35 ambao ni kati ya wale wanafunzi 51 waliokuwa na kesi mahakamani nao wamefukuzwa, kati ya hao 51 ilibainika kwamba watatu hawakuwa wanafunzi wa UDSM, hivyo wanafunzi walikuwa 48 tu,” alisema Profesa Mukandala.

Alisema kuwa kuna wanafunzi tisa ambao mpaka sasa uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili, unaendelea na kufafanua kuwa kati yao, wanne wanatuhumiwa kuwa vinara wa kuongoza vurugu zilizotokea Jumatatu na Jumanne wiki hii na watano ni wale wanaokabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani.

“Kati ya hao wanafunzi wanne ambao wako katika uchunguzi, mmoja alivunja vioo vya mabasi ya kubebea wanafunzi na mwingine alimchapa fimbo tumboni mwanafunzi mjamzito na kumsababishia maumivu makali.

Pia yupo aliyemmwagia profesa maji akiwa darasani. Yeye ni miongoni mwa wale 43 waliotimuliwa,” alisema Profesa Mukandala. Vurugu Akizungumzia vurugu, uharibifu na uvunjifu wa amani uliofanywa na wanafunzi hao, Profesa Mukandala alisema walikimwagia chakula vumbi, kuwapiga wafanyakazi wa mgahawa, kuharibu majokofu na kushambulia mabasi yaliyopita eneo la chuo yakiwemo yanayobeba wanafunzi, hali iliyosababisha huduma hizo kukosekana kwa siku mbili.

“Wanaotoa huduma ya mabasi kutoka Hosteli ya Mabibo waligoma kutoa huduma hiyo, hata wanaoendesha mgahawa nao waligoma kutoa huduma ya chakula jambo ambalo lilileta usumbufu kwa wanafunzi, ila kwa sasa hali ni shwari,” alisema Profesa Mukandala.
Kwa mujibu wa Profesa Mukandala, matukio hayo ni mwendelezo wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyoanza kutokea mwanzoni mwa Septemba mwaka huu na kwamba vurugu hizo zilianzishwa na kikundi kidogo cha wanafunzi ambao walipata wafuasi wachache na kuvuruga shughuli za chuo hicho.

Madai ya Wanafunzi Profesa Mukandala alisema awali madai ya wanafunzi hao yalikuwa ni kuondolewa adhabu za kinidhamu walizopewa wenzao wachache kwa mujibu wa kanuni na sheria za chuo, lakini baadaye wakageukia suala la kupatiwa fedha zao za malazi na chakula kwa kipindi cha kuanzia Desemba 10 mwaka huu. Alifafanua kuwa fedha hizo hutolewa kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza ilikuwa Sh 4.2 bilioni ambayo ilitolewa kwa wanafunzi wa Kampasi ya Mlimani na kwamba ziliingizwa katika akaunti tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Awamu ya pili ilikuwa ni Sh 700Milioni kwa wanafunzi wa Uhandisi, fedha hizo ziliingizwa jana (juzi) katika akaunti za wanafunzi na awamu ya tatu ilikuwa Sh 200Milioni kwa wanafunzi wanaosoma Uandishi wa Habari ambazo ziliingizwa katika akaunti Desemba 12,” alisema Profesa Mukandala.

Alisema katika kipindi hicho chote, Baraza la Chuo lilikutana kujadili hali hiyo na kuwataka wanafunzi hao kutoendelea na mgomo na kuvunja taratibu za chuo na kuwaonya kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, lakini baadhi yao hawakuonyesha kujali.

Profesa Mukandala alitumia fursa hiyo kuonya kuwa mwanafunzi yoyote atakayefanya tendo la kihalifu ikiwa ni pamoja na kujaribu kuwatisha wenzake au kuendesha mkutano nje ya taratibu za chuo, atafukuzwa. “Pia yanafanyika mawasiliano na Bodi ya Mikopo (TCU) ili wanafunzi waliofukuzwa chuo kutokana na uhalifu wasipate tena mkopo wa Serikali wala kuruhusiwa kusoma katika chuo chochote cha umma,” alisema Mukandala.

 Wakati huohuo, polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wameweka kambi katika eneo la Chuo Kikuu cha Ardhi kilichoko jirani na Chuo Kikuu hicho cha Dar es Salaam, ili kukabiliana na vurugu za wanafunzi. Mwananchi lilishuhudia magari manne ya FFU yakiwa yameegeshwa eneo hilo sambamba na gari linalobeba maji ya kuwasha.


Tanzania 50th Independence Concert and Profesa Jay Interview

Tuesday, December 13, 2011

MAKOMANDOO WA TANZANIA


Baadhi ya  Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania wakionesha ukakamavu na mbinu za mapigano bila silaha wakati wa kilele cha sherehe za Miaka 50 ya Uhuru uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

WASHINDI WA AIRTEL MZUKA WAENDELEA KUJIZOLEA ZAWADI ZAO

Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki (kushoto) akimkabidhi moja kati ya washindi wa promosheni ya Mzuka wa Airtel bwana Yusuf Semi Samsung Tablet baada kuibuka mshindi wa wiki ya kwanza ya promosheni hiyo ambapo wateja mbalimbali wa Airtel wanapata nafasi ya kujishindia zawadi kabambe ikiwemo simu,ipad, muda wa maongezi na pesa tasilimu.

Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki (kushoto) akimkabidhi moja kati ya washindi wa promosheni ya Mzuka wa Airtel bwana Murtaza Aliraza Samsung Tablet baada kuibuka mshindi wa wiki ya kwanza ya promosheni hiyo ambapo wateja mbalimbali wa Airtel wanapata nafasi ya kujishindia zawadi kabambe ikiwemo simu,ipad, muda wa maongezi na pesa tathilimu.

 Baadhi ya washindi wa promosheni ya Mzuka wa Airtel wakiwa na zawadi zao aina ya Sumsung Tablets mara baada ya kuibuka washindi na kukabidhiwa zawadi hizo katika makao makuu ya Airtel Tanzania,pamoja nao pichani ni mwakilishi wa Airtel (wa pili kushoto) Afisa uhusiano Dangio Kaniki akifurahia kwa pamoja ushindi kwa wateja hao







RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA WOTE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Matunda na bidhaa aina mbalimbali za shambani

Nyanya, Vitunguu na Maembe
Maembe na Vitunguu

Vitunguu na Nyanya

Thursday, December 8, 2011

Mafuriko huko Bogota-Colombia

Firefighters evacuate residents from a flooded neighborhood in Patio Bonito, southwest of Bogota on Dec. 7. At least 96 people have died as a result of heavy rains, authorities said. Colombia's weather office expects La Nina-related downpours to continue at least until the end of the first quarter of next year

Two men wait on their car in a flooded street of the Bella Vista neighborhood, following the overflowing of the Bogota River, on Dec 7 in Bogota, Colombia. Bogota's mayor Clara Lopez on Wednesday declared a state of emergency because of the floods and mudslides caused by heavy rains

Firefighters evacuate residents from a flooded neighborhood in Patio Bonito, southwest of Bogota on Dec. 7.

A woman carries her daughter on her shoulders as she wades through a flooded area of a residential complex in the Bella Vista neighborhood, following the overflowing of the Bogota River, on Dec. 7., in Bogota

WWF film of NZ penguin release post oil-spill.mov

Miti ya X-Mass yaanzisha maandalizi ya sikukuu hiyo huko Marekani

Askari wa jeshi la Marekani Sgt Evan Kirouak ambaye amerejea hivi karibuni toka Iraq akipoea zawadi ya mti wa X-Mass jana Jumatano huko Fort Carson Colorado Spring-Marekani

Hapa Sgt Evan Kirouak akisimama na mchumba wake Aeryn Dahl mara baada ya kuchagua mti wa X-Mass

Sgt Patricia Foust wa jeshi la Marekani nae akiwa na mti wake wa X-Mass

Mke wa askari wa jeshi la Marekani Candace Jones akiwa amembeba binti yake Abighail (mwenye miaka 2) huku akielekea kwenye gari mara baada ya naye kupata mti wake