Tuesday, April 29, 2008

TIGO YAMWAGA TIKETI ZA ONESHO LA 50 CENT




Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya Mwana G Unit anayetesa katika anga la Muziki wa Hip Hop 50 Cent kutua nchini, Kampuni ya Simu za mikononi ya TIGO, imemwaga tiketi za bure kwa wateja wake kwa ajili ya kuhudhuria onesho hilo, Mwana ShowBiz Richard Bukos anaporomoka nayo.

Tiketi hizo zimetolewa kwa washindi wa Bahati Nasibu ya TIGO Muziki, inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo katika droo ya pili iliyofanyika jana katika Makao Makuu ya Kampuni hiyo iliyopo Mtaa wa Lugoda jijini Dar es Salaam, walipatikana washindi 200 hivyo kufikisha jumla ya washindi 400 baada ya wiki iliyopita kupatikana washindi wengine wenye idadi sawa na ya jana.

“Leo tena wamepatikana washindi 200 na wale wa wiki jana wanakuwa 400 hivyo bado tuna tiketi 300 zinashindaniwa. Tunawaomba wananchi wajiunge na Mtandao wa TIGO na waendelee kushiriki shindano hili kwa kutuma neno MUZIKI au MUSIC kwenda namba 15315 ili waweze kujishindia zawadi hiyo ya tiketi ya kumshuhudia live 50 Cent,” alisema Meneja Masoko wa TIGO Kelvin Twissa.

Twissa alidakisha kuwa pamoja na shindano hilo la tiketi, Mtandao wa TIGO ni wa gharama nafuu na hivi sasa wanaendelea na Longer Longa II na XTREME ili kila mwananchi aweze kumudu gharama za huduma zao.

No comments: