This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Wednesday, May 14, 2008
Kumbe KAduguda Mkorofi Sana!!!
KATIBU Mkuu wa Simba, Mwina Kaduguda amesimamishwa uongozi wa klabu hiyo kwa muda usiojulikana.
Habari zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa Kaduguda amesimamishwa kutokana na tuhuma 11 zilizokuwa zikimkabili.
Tuhuma hizo ziliwasilishwa mbele ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo na kushirikisha watu tisa, baraza la wazee wajumbe watatu na uongozi wote wa Simba.
Kikao hicho ambacho kilifanyika jana jijini Dar es Salaam, maamuzi yake ndiyo yaliyoafiki kusimamishwa kwake (Kaduguda) hadi mkutano mkuu wa klabu hiyo ambao utafanyika baada ya zoezi la uhakiki wa wanachama na kutolewa kwa kadi mpya.
Habari za awali ziliorodhesha tuhuma hizo dhidi ya katibu huyo kuwa ni pamoja na kuwapiga makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Omar Gumbo na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Mohamed Mjenga mwaka jana katika mashindano ya kombe la Hija Salehe, visiwani Zanzibar.
Nyingine ni pamoja na kumtukana mwanachama wa klabu hiyo, Dioniz Malinzi mwaka 2007. Malinzi, pia alikuwa mdhamini wa klabu na kumsababisha ajitoe katika udhamini huo.
Pia, anadaiwa kuwatukana makocha wawili wa kigeni ambao waliwahi kuifundisha timu hiyo, ambao ni Nielsen Elias na Neider Do Santos, raia wa Brazil na kusababisha waondoke na kurudi kwao.
Kilieleza kuwa Kaduguda alishawai kuchukua jezi na mipira ya klabu hiyo na mpaka leo hajarudisha klabuni hapo.
Pia, inadaiwa kuwa alitumwa na klabu hiyo kwenda katika kikao cha rufaa ya mchezaji wao ambaye walimchezesha wakati hana adhabu, Juma Said Nyosso katika Shirikisho la Soka la Tanzania, TFF lakinhakwenda na kusababisha kupokonywa pointi tatu.
Katika mechi ya watani Simba na Yanga iliyochezwa Morogoro, kiongozi huyo anadaiwa kuwa aligombana na mtunza fedha wao, Idd akitaka fedha za mapato.
Tuhuma nyingine zinazomkabili ni pamoja na kumpiga mkewe katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kitu ambacho kiliidhalilisha klabu hiyo ikizingatiwa kwamba yeye ni kiongozi wa klabu hiyo.
Pia, anadaiwa kupigana na mke wake wakiwa Msamvu, Morogoro wakati wakitokea Bukoba kwenye mechi ya Simba na Kagera iliyofanyika Katika Uwanja wa Kaitaba. Pia, wakati wa kurudi aligombana na dereva pamoja na wachezaji baada ya mkewe kutaka gari lisimame kila mara achimbe dawa na inadaiwa kuwa alikuwa amelewa.
Katika kukao cha Jumapili cha uongozi wa Simba na kundi la Friends of Simba, kiongozi huyo anadaiwa kuwa aliwatukana wanachama wa kundi hilo na mdhamini ambaye alikuwa anamlipa kocha Milovan Cirkovic dola 5,000 kwa mwezi na kusababisha asusie kikao na kuondoka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment