Friday, September 17, 2010

Irene Uwoya nae atembea na kichupi huko Dubai, haya jionee mwenyewe!


Issa Mnally Na Richard Bukos
Nyota wa Bongo Movies, ambaye pia ni Miss Tanzania Nambari 5, 2006/07, Irene Uwoya, anadaiwa kuliaibisha Taifa kufuatia kitendo chake cha kutembea nusu utupu kwenye Uwanja wa Ndege wa Mji wa Dubai uliopo Muungano wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Amani lina data za kumwaga.


Kwa mujibu wa mtu mmoja (jina tunalo) aliyekuwa kwenye mji huo, tukio hilo lenye sura ya aibu lilijiri Jumatatu Septemba 6, 2010, saa nne asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Dubai ambapo msanii huyo alikuwa njiani kuelekea Tanzania.


Staa huyo anayeishi na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ nchini Cyprus (jirani na Uarabuni), alivaa kaptula ya ‘jinsi’ fupi kiasi cha kuwafanya watu uwanjani hapo ambao wengi wapo katika Mfungo wa Ramadhan, kumtumbulia macho ya ‘kulaani’ vazi hilo lenye majaribu makubwa.

MWANZO WA MKASA
Baada ya kuona wananchi wengi wakimtazama Irene katika nyuso za ‘kuhamasika’ kufuatia kivazi hicho ambacho juu alikivalia jezi Namba 3 yenye jina la Ndikumana mgongoni, ndipo mtu huyo alipoamua kuwasiliana na Mpiga Picha Wetu, Issa Mnally na kummegea ishu nzima.


Ilikuwa majira ya saa 4:04 asubuhi ya Jumatatu, ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu ya mkononi (sms) ukaingia kwenye simu ya mpiga picha huyo ukisomeka hivi:

“Haloo… (likiandikwa jina la mpiga picha huyo) mambo vipi? Kama unaweza majira ya saa tisa mchana (alasiri) leo nenda Uwanja wa Ndege wa Dar umpige picha Irene Uwoya, yaani kakaa uchi mpaka siye huku Dubai tumeona aibu sana kaka... ni noma, yule demu siyo kabisa.”


Baada ya kupata ujumbe huo, mpiga picha huyo alimwendea hewani mtuma ujumbe huo ambapo alijitambulisha kwa jina na kusema kwamba, yeye alikuwa Uwanja wa Ndege wa Dubai akimsindikiza jamaa yake na alimwona Irene, lakini kwa jinsi alivyovaa hakutaka kumsalimia (huenda wanafahamiana) kwani aliona aibu.

“Mimi nilikuwepo pale Uwanja wa Ndege wa Dubai, nilimwona Irene lakini sikutaka kabisa tusalimiane kwani ni aibu sana,” alisema mtu huyo.



KAULI YA CHANZO INAFANYIWA KAZI
Saa 8: 45 Wapiga Picha Wetu, Issa Mnally na Richard Bukos walitia timu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar na kutegesha kamera tayari kwa kusubiri ndege aliyopanda msanii huyo, Fly Emirates.

Ilikuwa saa 10:08 ndugu, jamaa na marafiki waliofika uwanjani hapo kupokea wageni wao walionekana wakipigwa butwaa huku wakiangalia upande wanaotokea wageni, kumbe Irene alishafika na sasa alikuwa akitoka ili kukutana na nduguze.


Ndipo Mapaparazi Wetu walipoanza kuwajibika kwa kumfotoa picha mbalimbali, lakini na yeye (Irene) alishtukia ishu na kuanza kukimbilia maeneo mbalimbali ya Uwanja huo kwa lengo la kukwepa kamera.

Hata hivyo, Wapiga Picha Wetu walimfukuza kwa nyuma huku nyota huyo akiwa anajiziba uso kwa mkoba mdogo wa mkononi.

WAPIGA PICHA WAKUMBANA NA KIMBEMBE
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmoja wa ndugu waliokuja kumpokea msanii huyo alimkamata mmoja wa Mapaparazi Wetu na kufanya jaribio la kupora kamera hali iliyozua tafrani kubwa iliyosababisha Mpiga Picha Wetu kujeruhiwa mkono wa kuume, lensi ya kamera kuharibika na simu ya mkononi kupotea.


Baadhi ya watu waliokuwa wakushuhudia tukio hilo walisikika wakimpa vijembe ndugu huyo kwa kumwambia kuwa, alichotakiwa kufanya ni kumwonya Irene kuachana na mavazi yasiyo na maadili na si kupambana na Wapiga Picha.

Hata hivyo, kamera hiyo ilidhibitiwa vilivyo na Wapiga Picha Wetu na picha zilizokwishapigwa kuwa salama (angalia ukurasa wa mbele).

Tukio la ndugu huyo liliripotiwa muda huo huo kwenye Kituo cha Polisi Uwanja wa Ndege kwa kuandikishwa kwa jalada namba JNA/IR/174/010 ambapo Irene na familia yake wanasakwa na polisi wa kituo hicho ili kujibu shitaka la shambulizi na kuharibu mal

1 comment:

Unknown said...

Dada Irene, Mke wa mtu lazima ujiheshimu kwa ukivaa vazi la heshima tena unapendeza sana kuliko hivyo vichupi unavyovipenda unamdhalilisha mume wako pamoja na familia yako jumla. Muogope Mungu kumbuka wewe ni kiumbe tu, siku moja utakuja acha mambo yote ghafla tengeneza maisha yako. jua kesho pia kuna hukumu usijisahau.