Friday, September 17, 2010

Mashindano ya Uimbaji "Tusker Project Fame" yazinduliwa Dar


Pichani kushoto ni Meneja matukio, Bahati Sigh akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu mchakato mzima wa ushiriki wa shindano la Tusker Project Fame mbele ya Waandishi wa Habari, ambalo limezindua kampeni yake ya 4 ndani ya hoteli ya Movernpick, mapema leo mchana jijini Dar, katikati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii Dada Teddy Mapunda na mwisho kabisa ni Mshauri wa Masoko Dada Caroline wote kutoka kampuni ya bia ya Serengeti a.k.a SBL.

Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii wa SBL,Teddy Mapunda amewaeleza Waandishi wa habari kuwa nia na madhumuni ya kufanya shindano hili kwa Tanzania ni kutaka kuinua vipaji vya Watanzania hapa Tanzania.

Tusker Project Fame kwa mwaka huu itakuwa inashirikisha nchi tano ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania pamoja na Sudani ya Kusini.

Aidha Teddy amesema kuwa usahili kwa ajili ya shindano hilo utafanyika katika hoteli ya Peacock-Mnazi Mmoja siku ya jumamosi kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 11 jioni.

Amesema kuwa washiriki wa shindano hilo ni lazima wawe na umri wa miaka 23 na kuendelea na wawe na vitambulisho vyao kuhakiki umri wao,"fomu za kujiunga zinapatikana Mlimani City, Benjamin William Mkapa Towers, IPS Building pamoja na sehemu ya usahili wenyenyewe pale Peacock Hotel", amesema

No comments: