Monday, September 27, 2010

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Jamii


ICT ni mojawapo ya kazi ambayo kama utaiendekeza bila kuwa makini basi inaweza kukupelekea kupoteza au kuharibu mahusiano,marafiki na hata kutengwa na wanafamilia.Leo hii tutaangalia mustakabari wa wana ICT ndani ya jamii,mwisho kabisa tutapenda kupata maoni yako ni jinsi gani jamii na wana ICT wanavyoweza kushirikiana ili kuondokana kero zilizomo ndani yake.

Kazi za manane
Kwenye ulimwengu wa ICT kufanya kazi hadi usiku wa manane au kutolala usiku mzima ni jambo la kawaida kabisa,je ni mara ngapi mitambo imegoma kufanya kazi na ukakesha ofisini ukitatua matatizo? Ni mara ngapi upo katikati ya mapumziko nyumbani mara ukapokea simu ukiambiwa kila kitu site kipo down ukatakiwa kuacha mambo yako binafsi na kukimbilia site kurekebisha mambo?

Kuna siku niliwahi kuongea na mmoja wa wana ICT ambaye ni tegemezi kwenye kampuni moja ya mawasiliano mujini,yeye alilalamikia kuhusu kutoelewana na mchumba wake kwakuwa muda mwingi yupo ofisini na hata akirudi nyumbani kila wakati simu haziishi hivyo wanakosa muda wa kujadili mambo yao binafsi ukizingatia ndio kamaliza chuo hivyo bado kijanaa,kwetu sisi wana ICT hili linafahamika lakini je kwa walio nje ya ICT wanaweza kulifahamu na kulikubali??

Kwenda na wakati
Mtafaruku hauishii hapo,kumbuka kuwa ICT ni teknolojia inayoishi,hapa nina maana kila kukicha kuna mambo mengi yanagunduliwa au yakihitajika na wanajamii ambao kwao wao ni kila anachofikiria anajua ni lazima wana ICT atakuja na suluhisho,hivyo ni kazi yetu kuja na suluhisho la mahitaji ya wanajamii vilevile kuwa tayari kujifunza maarifa mapya pindi wenzetu wanapogundua,hivyo basi ukiwa mwana ICT wewe upo shuleni.

Kuna rafiki yangu aliwahi kutembelea nyumbani ninapoishi,maswali la kwanza aliloniuliza,Hivi lini utamaliza kusoma? Hivi vitabu vyote umesoma wewe au? Jibu linakuja ili kuwa mwana ICT bora ni lazima uwe na uwigo mkubwa mno wa idara kadha wa kadha huku ukijiupdate na teknolojia mpya,Hivyo muda kwetu ni kama almasi,ila jamii inaweza kutuelewa?

Wanawake na ICT
Hizi ndio sababu zinazopelekea wanawake kuikimbia hii fani ya ICT,kwani wao wakifikiria msongo uliopo kwenye ICT wanaogopa kuna uwezekano wakapoteza au kukosa wenza wao kwakuwa hawatakuwa na muda wa kuitunza familia kwani kama wengi ujuavyo mila zetu nyingi ni kuwa mama ndiye mtunzaji wa familia.Hili sio tu kwa Afrika,bali dunia nzima,iwe Marekani,iwe Uchina na hata Burundi,wanawake kwenye ulimwengu wa ICT ni wachache mno.

Ushauri
Hivyo basi leo hii,tungependa kujua wewe kama mwana ICT unapambana vipi na hii hali,Je unatumia njia gani kuweza kuielimisha familia yako na kukuelewa,Kwa wale ambao sio wana ICT je wewe kama mwana jamii una ushauri gani juu ya hili kwa wana ICT? Je wakinamama walio ndani ya ICT wanamaoni gani?

Kwa kuchangia maoni yako hapa unaweza kusaidia wana jamii na kuokoa ndoa na mahusiano kibao ambayo hadi sasa yapo kwenye mkimki mkimki na pia tukajenga jamii imara.

No comments: