Balozi wa ZindukaProfesa J akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu Tamasha la Tuzo za wasanii wa mziki wa Injili linalotarajiwa kufanyika februali 27 Kulia ni Mratibu wa Tamasha hilo, Haris Kapiga.
********************************
TANZANIA Gospel Promoters (TGMP) kwa mara nyingine tena baada ya miaka mitano kupita wameandaa tamasha la Tunzo za Muziki wa Injili (Gospel Music Awards) lililopangwa kufanyika Februari 27 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari Mratibu wa Tamsha hilo Haris Kapinga kutoka Kampuni ya Clouds Media Haris Kapinga alisema tamasha hilo litatumika kuwapongeza na kufanya tathmini ya jumla kwa wasanii binafsi na tasnia nzima huku Tunzo mbalimbali zitatolewa.
Tunzo hizo ni wimbo bora wa mwaka, mwandishi bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kike wa mwaka, mwimbaji bora wa mwaka wa kiume, kundi bora, msanii bora wa muiziki wa Injili wa mwaka na mwimbaji anayechipukia katika uimbaji wa nyimbo za Injili. Wimbo wa mwaka, video bora, Mtayarishishaji bora wa mziki wa video wa mwaka , Mtayarishaji bora wa muziki, Tunzo ya Jumuiya, Kwaya bora ya Akapela,Kwaya bora inayotumia ala, bendi bora ya muziki wa Injili, Kwaya bora inayotumia ala ya Piano.
“Jinsi watu watakavyoweza kupiga kura, kura zitaanza kupigwa Januari 29 mwaka huu na kufikia kilele cha February 12 huku fomu zote zilizopigiwa kura zitatakusanywa Februari 13” alisema Kapinga. Anaendelea kwa kusema kuwa mdhamini mkuu wa tamasha hilo ni Mradi wa kutokomeza Malaria , Zinduka ambao zaidi ya lengo kuu la kupambana na Malaria inatumia tamasha hili kuwaunganisha viongozi wa dini mbalimbali kwa kuanza na madhehebu ya dini ya Kikristo ili kupeleka ujumbe kuhusiana na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
Tangu Mradi huo ulipoasisiwa nchini mwaka 2010 umekuwamradi wa kwanza unaofanya kazi kwa kushirikiana na sekta mbalimbali katika jamii ili kusimamia pamoja na kumaliza ugonjwa wa Malaria nchini kote.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa dini ambao ni Sister Mariana Francis kutoka Roman Catholic, Mchungaji David Mwasota ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste, Mchungaji Solomon na John Gao wa Makanisa ya Anglican, ambao wote kwa pamoja wamewakumbusha wana jamii na kuwahimiza Watanzania katika kujilinda, kuepukana na vifo vinavyoweza kuzuilika.
“Tunaimani kwamba kwa kutumia nguvu ya muziki wa Injili , mwamko na ufahamu kwenye jamii vitaongezeka sana huku jamii na waumini wakiunganisha nguvu ya kupambana na Malaria” alisema Mwasota.
Soucre: Bongo Weekend – 28/1/2011
No comments:
Post a Comment