Bendi hii ni ya ‘watoto wa hapahapa nyumbani’, huu ndio msingi wa bandi hii kubandikwa jina la “Wahapahapa”.
Bendi hii ndio nguzo kuu katika shughuli nzima ya utayarishaji na kurekodi nyimbo zote unazozisikia katika mchezo wa radio wa “Wahapahapa”.
Tanzania, imethibitishwa kisayansi, kuwa ndio mama wa binadamu wote alizaliwa hapa, basi ukweli huu una kila sababu ya kututhibitishia kwamba hata mirindimo ya miziki yote duniani imezaliwa hapa, na hapa ndipo ilipo bendi ya “Wahapahapa”.
Bendi ya Wahapahapa inapiga muziki wake kuenzi utamaduni, si tu ule wa mtanzania, bali wa wanadamu wote. Wahapahapa pia inatumia muziki wake kusaidia wasikilizaji katika harakati zao za kujiletea maendeleo, na bila kusahau suala zima la kuienzi lugha tamu ya Kiswahili.
Aina ya muziki unaopigwa na bendi hii umebatizwa jina la “TanzRock”, na hili ndilo jina pia la albamu ya kwanza.
No comments:
Post a Comment