This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Friday, March 4, 2011
Binadamu wengine wana ROHO MBAYA ya UKATILI-Soma hii
Kiukweli kutoka moyoni nimesikitika sana!!!hivi kwa nini jamani umfanye hivi mtoto wa mwenzako? mtoto yupo darasa la tatu tu.Kisa chenyewe hana daftari!
Mtoto unayemuona katika picha ni mwanafunzi wa shule ya msingi Buguruni jijini Dar es Salaam anasoma darasa la tatu, siku yanamkuta haya alikuwa na kosa la kutokuwa na daftari mwalimu anaeitwa Ms.Haule ambaye ni mdada alimpiga na kumfinya kwa kumvuta ngozi ya macho.Mtoto nyama ya macho ikamtoka nje,macho yakawa mekundu yanatoa tu machozi mtoto akawa kama kapoteza fahamu hata kusikia akawa hasikii.Jamani nimesikitika sana kila nikiangalia picha hii ni huzuni kubwa.Mtoto anaendelea na matibabu katika hospital ya CCBRT ambako baba yake amempeleka.Baba wa mtoto anasikitika sana hana hakika kama mtoto wake atakuwa sawa!!
Hivi sasa mwalimu husika kakimbia haijulikani alipo na polisi wanamtafuta.Kwa nini lakini mwalimu umefanya hivyo haukuwa na kitu kingine cha kumuadhibu huyo mtoto mpaka macho yake uyavute? Poor kid nahisi anasikia maumivu makali sana na huyu mtoto lazima hata kisaikolojia hayupo sawa.Wewe mwalimu huko uliko hata kama umejificha ila hutajificha milele hata kama si mkono wa sheria kukuangukia ila mwenyewezi Mungu atakuonyesha nguvu yake!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment