Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Paul Mtowe wakihutubia jumuiya iliyofika katika hafla hiyo, Mheshimiwa Lema aliwahakikishia watoto hao watasoma na kupata matibabu bure na Mwenyekiti wa ArDF aliwahakikishiwa licha ya kupatiwa Ada na Matibabu pia watapatiwa Chakula kufuatia kampuni ya Arusha Mambo kuazima shamba lake lenye Ukubwa wa ekari 30 lilimwe na chakula kitakachopatikana kigawanywe katika shule za Kata na Vituo vya watoto yatima, hata hivyo aliomba jamii, mashirika na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia Taasisi yao ili imudu kuwasomesha watoto hawa na kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Paul Mtowe wakimpatia mmoja wa wazazi Cheti cha kuthibitisha kupatiwa msaada wa Ada na Matibabu kwa watoto wake kwa kipindi cha miaka minne.
Kati ya watoto wenye kuishi katika mazingira ya kati waliojitokeza kuwahamasisha watoto wenzao wenye kuishi katika mazingira magumu kuwa watashinda na siku moja wataishi katika Nchi yenye neema wakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini na mmoja wa mzazi aliyejitokeza kusaidia watoto wenye uhitaji baada ya kununua tshirt za ArDF kama mchango wao kwa watoto wenzao.
Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakiwasajili na kugawa Tshirt na Bendera za Taifa kwa Watoto waliofika katika hafya hiyo kabla hawajaimba wimbo wa Tanzania Nakupenda na baadae wimbo wa Taifa.
Baadhi ya Wazazi na Walezi waliojitokeza wakiwa katika picha ya Pamoja na Mbunge Pamoja na Mwenyekiti wa ArDF baada ya watoto wao kupatiwa Ada, Kadi za Matibabu, Daftari na Kalama Ili kuendelea na kutimiza ndoto zao.Baadhi ya Watoto kati ya watoto 400 watakaopatiwa msaada wa Ada na Kadi za Afya na Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini kwa kupitia Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo, watoto hao waliojitokeza kwenye Ofisi ya Mbunge wa JImbo la Arusha Mjini kupokea Msaada huo wa Ada wenye thamani ya Shilingi Milioni 60 na kadi za bima ya Afya zilizopata udhamini kutoka Shirika lisilo la Kiserekali la Green Hope linalopata msaada kutoka Serekali ya Canada.
Baadhi ya watoto na Madiwani waliojitokeza katika picha ya Pamoja na Mbunge Pamoja na Mwenyekiti wa ArDF baada ya kupatiwa Ada, Kadi za Matibabu, Daftari na Kalama Ili kumudu mahitaji ya masomo yao.
No comments:
Post a Comment