Monday, October 10, 2011

Kazi yangu ni Ngumu ila Naipenda!

Kazi yangu ni kukamata Nyoka( Chatu). Kwanza najifunga ngozi mkononi!

Kisha nazama katika shimo anakoishi huyo Chatu

Natumia taa za asili (Kijinga cha moto)

Mara ghafla nishawasili anapoishi Chatu huyo

Sasa kazi inaanza, kwa hasira za kujilinda na kulinda mayai yake Chatu anakuja kwa kasi kunimeza, lakini nampa mkono niliofunga ngozi aumeze

Natumia fursa hio kumshika shingoni (unaifahamu shingo ya chatu?)

Najivuta kinyumenyume taratibu nikikaribia mdomo wa shimo nampa ishara jamaa yangu wa kule nje anivute

kazi imekamilika naondoka na Mzigo wangu (inataka Ujasiri usio wa kawaida kwa sababu mwingine kutazama tu hizi picha hawezi, sembuse kumkamata?)

Hapa kijijini kwetu huyu ni kitoweo cha siku zaidi ya tatu. Karibu chakula ewe msomaji

Hii ndio KAZI YANGU!!

No comments: