Monday, January 30, 2012

Waliopigana vita Iraq wakaribishwa Marekani

Washiriki wa gwaride/maandamano ya heshima ya kuwapokea/kuwakumbuka waliopigana vita vya Iraq. Sherehe hio ilifanyika huko ST. Louis Marekani, wapo waliouawa na wapo waliorudi salama.

Mwanamama Stephanie King akiwa amebeba picha ya mjomba wake Kanali Stephen Scott alieuawa Iraq mwaka 2008. Stephanie alikua miongoni mwa walioandamana kuwapokea na kuwakumbuka maveterani wa vita vya Iraq.

Larry Connor, askari wa Marekani aliepigana vita vya VIETNAM akipiga salute kutoa heshima kwa askari wanaorejea toka Iraq. Kwa TANZANIA askari hatakiwi kupiga saluti kama hiyo hadi avae sare/uniform kamili ya jeshi. Huyu kavaa kiraia na amepiga. Jeshi letu TANZANIA lina NIDHAMU kubwa katika swala hili.

No comments: