Wednesday, February 29, 2012

Tamasha la PASAKA ni April 8-UWANJA WA TAIFA -DAR ES SALAAM

WADAU wa muziki wa Injili wa Dar es Salaam, wameipongeza Kampuni ya Msama Promotions kwa kuamua tamasha la Pasaka kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa badala ya Diamond Jubilee. 

Maoni hayo yametolewa na baadhi ya wadau wa muziki wa Injili waishio Dar es Salaam baada ya kutangazwa kuwa tamasha la Pasaka litafanyika Aprili 8 mwaka huu Uwanja wa Taifa. "Nikiwa Mkristo mwenye kupenda kusikia ujumbe wa neno la Mungu pia kwa njia ya uimbaji, nimefurahi sana kusikia tamasha la Pasaka litafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam," alisema Jimmy Bukuku wa Mbagala.

Bukuku anayeabudu Kanisa la Pentekoste Church of Holiness Mission (PCHM) la Tandika, alisema kwa namna fulani tamasha hilo litawakuza watu kiroho. Alisema, mbali ya kuburudisha na kufariji, ujumbe wa neno la Mungu ambao hupatikana kupitia nyimbo, huweza kuwabadili wengi.

Bukuku alisema kutokana na ujumbe wa neno la Mungu kumgusa kila mwanadamu, ndio maana muziki wa Injili umekuwa ukiwagusa wengi bila kujali ni Mkristo au Muislamu. Alisema kwa upande wake analiombea tamasha hilo ili lifanikiwe kwa sababu limekuwa likiwabadili na kuwajenga wengi kiroho.

Alisema analisubiri kwa shauku tamasha hilo la Pasaka akiamini litakuwa lenye upako kama yaliyowahi kufanyika chini ya Msama Promotions. Mdau mwingine aliyegusia tamasha hilo, ni Furaha Masinga wa Kanisa la Mchungaji David Mwasota ambaye kwa upande wake, alisema litasaidia wengi kuimarika kiroho.


No comments: