Tuesday, March 20, 2012

Wa-Afganistan washerehekea mwaka mpya "Nowruz" wa Kiajemi

Mwanamuziki wa Ki-Afghanistan akipiga muziki huku amezingirwa na mashuhuda kibao kwa kutumia kifaa kiitwacho Dombura katika kusherehekea mwaka mpya wa Waajemi, hayo yametokea leo Jumanne Machi 20,2012 huko Kabul

Wanaume wakinyanyua bendera ya kuongezea raha katika sherehe hiyo

Askari Polisi wakiwa wamezuia barabara ili watu wasijazane huko Sakhi kulikofanyika sherehe hizo. Kiusalama uamuzi huu ni mzuri sana

Mke na mume wameketi kilimani wakishudia sherehe hizo (Tazama mbele chini kwa mbali) hapa ni Karti-El-Shakhi mjini Kabul

Kijana mdogo akionyesha madoido yake katika kucheza wakati wa sherehe hizo za mwaka mpya wa Kiajemi

No comments: