Friday, April 13, 2012

SHAIRI LA KUMUENZI KANUMBA

Naanza kwa jina lake, Mtukufu MaulanaAtupe rehema zake, Atuongoze bayanaKila mtu ana yake, Sikuye hawezi kanaKwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Shairi naliandika, Kalamu wino machoziNajikaza kuishika, Nilibuni kwa majonziMaini yanikatika, Katutoka kiongoziKwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Majonzi yametukumba, Afrika masharikiAmetutoka Kanumba, Kifo hakitabirikiKarudi kwake Muumba, Alotaka afarikiKwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Huzuni umenitanda, Moyo ukinenda mbioNikiitazama sanda, Kifwatacho ni kilioTutaenzi zako kanda, Filamu ndo masalioKwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Safari imewadia, Pasi watu kubainiKaka ukafwata njia, Jongomeo kwa mananiSanaa itafifia, Bila we’ si burudaniKwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Msanii ulo bora, Nakusifu hadharaniSio Tanga si Tabora, Wewe ndio namba waniFilamu zitadorora, Umetutoka rubani

No comments: