Thursday, May 17, 2012

BREAKING NYUZZZZZ........ Mchezaji wa Timu ya Simba,Patrick Mafisango afariki Dunia kwa ajali ya Gari jijini Dar

KWA HISANI YA MICUZI BLOG: Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaeleza kuwa Mchezaji wa Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam na Timu ya Taifa ya Rwanda, Patrick Mafisango (pichani) amefariki Dunia kwa ajali ya Gari alfajiri ya leo majira ya saa kumi hivi wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake.

Globu ya Jamii inaendelea kuwatafuta viongozi wa timu ya Simba ya Jijini Dar ili kupata taarifa zaidi juu ya Kifo cha Mchezaji huyo. Hivyo tuvute subira mpaka hapo Globu ya Jamii itakapo kuja na taarifa kamili.

No comments: