Majeshi ya serikali nchini Syria yameanza mashambulizi mapya
usiku wa kuamkia Alhamis, dhidi ya mkoa wenye upinzani mkubwa wa Homs
ambayo yamelenga zaidi mji wa Al-Rastan ulioko mikononi mwa waasi.
Shirika la haki za binadamu la Syria lenye makao yake mjini London
limesema majeshi ya serikali yanataka kuuharibu kabisa mji huo ambao ni
kitovu cha harakati dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Assad.
Mkuu wa Shirika hilo, Rami Abdul Rahman, alisema makombora yasiyopungua
30 yaliangushwa katika mji huo katika kipindi cha dakika 10. Mji wa
Al-Rastan umeshuhudia mfululizo wa mashambulizi kwa miezi kadhaa kutoka
kwa majeshi ya serikali yanayotaka kuurejesha kutoka mikononi mwa waasi.
Askari wa jeshi la Syria Huru akifurahia mbele ya kifaru
kichoharibiwa wakati wa mapigano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.
Abdul Rahman amewataka waagalizi wa amani wa Umoja wa Mataifa kufika
haraka katika Mji huo uliozingirwa na majeshi ya serikali. Siku ya
Jumatatu, timu ya waagalizi hao iliripoti kuwepo mapigano makali karibu
na al Rastan ambapo wanaharakati walisema wanajeshi wasiopungua 23 na
raia 7 waliuawa katika makabiliano kati ya wasi na wanajeshi wa
serikali.
Milipuko mingine imeripotiwa kutikisa vijiji vya Al-Jamila na Al-Furqan
katika mkoa wa Aleppo na mingine imesikika sehemu mbalimbali za mji huo
uliopo kaskazini mwa Syria. Hakukuwa na taarifa za maafa
yaliyosababishwa na milipuko hiyo lakini katika mji wa Al-Qatifa,
mapigano yalizuka usiku baada ya wanajeshi kadhaa kutoroka jeshi na
kujiunga na waasi.
Umoja wa Mataifa walia na pande zote
Umoja wa Mataifa umezilaumu pande zote katika mgogoro huu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo ni sehemu ya mpango wa amani uliopendekezwa na mjumbe maalumu wa umoja huo na umoja wa nchi za jumuiya ya kiarabu, Koffi Annan.

Katika mahojiano yake ya kwanza na chombo cha habari tangu Desemba
mwaka jana, rais wa Syria Bashar Al-Assad alisisitza kuwa utawala wake
unapambana na mamluki kutoka mataifa ya kigeni wanaotaka kumpindua, na
si raia wasio na hatia wanaotaka demokrasia.
Licha ya kunyooshewa kidole na jamii ya kimataifa kuwa ndiyo chanzo cha
mgogoro huu uliodumu kwa muda wa miezi 14 na kuua watu zaidi ya 12,000,
Assad aliiambia Televisheni ya Urusi ya Channel Rossiya24 kuwa majeshi
yake yamewateka mamluki kadhaa na kwamba watawaweka hadharani ulimwengu
upate kuwaona.
Hivi ndivyo hali inavyokuwa Mkoani Homs.
Azionya Uturuki na Lubnan
Assad pia aliyaonya mataifa jirani ambayo anayashtumu kwa kuwapatia silaha waasi na kusema kuwa ukipanda mbegu za vurugu ndani ya Syria, zinaweza kukuathiri na wewe baadaye. Ingawa hakufafanua zaidi, lakini waasi na wanaharakati wanasema majeshi ya Syria yameweka mabomu ya ardhini katika njia zinazotumiwa kupitisha silaha hasa kutoka nchi za Uturuki na Lubnan.

Assad ambaye alirithi uongozi kutoka kwa baba yake, anaonekana
kuendelea kujizatiti licha miezi 14 ya harakati za kumuondoa kutokana na
mgawanyiko katika jamii ya kimataifa, hasa mataifa makubwa wanachama wa
kudumu wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa, akiungwa mkono na
Urusi na China.
Lubnan nako hali inazidi kuchafuka
Wakati huo huo mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine saba kujeruhiwa siku ya Alhamis katika makabiliano mapya kati ya watu wa kabila la Alawite wanaomuunga mkono rais Bashar Assad na waumini wa madhehebu ya Sunni wanaounga mkono waasi.

Wanajeshi wa Lubnan wakijianda kukabiliana na vurugu mjini Tripoli ambako machafuko ya Syria yanaonekana kuhamia.
Makabiliano ya hapa na pale yakihusisha pia mashambulizi ya roketi na
silaha za rasharasha yalianza majira ya saa 10 usiku katika vijiji vya
Bab al-Tebanneh na Jabal Mohsen kwa mujibu wa afisa moja aliyetaka jina
lake lihifadhiwe.
Jabal Mohsen inakaliwa na watu wa kabila la Alawite na Bab al-Tebbaneh
inakaliwa na watu wanaounga mkono waasi. Mapigano kati ya watu hao
mwanzoni mwa wiki hii yalisababisha vifo vya watu 9 na kujeruhi 50 na
kuzua hofu ya mgogoro wa Syria kusambaa katika mataifa jirani. Vurugu
hizi zilisababishwa na kukamatwa kwa sheikh moja wa kisunni kwa madai
kuwa alikuwa mwanachama wa genge la magaidi.
No comments:
Post a Comment