Thursday, June 28, 2012

HUYU NDIYE MCHEZAJI WA UGANDA ALIYEFIA UWANJANI.

Hapa ilikua ni muda mfupi kabla ya kukimbizwa hospitali kabla hajafariki.
Mashabiki wa mpira wa miguu huko Sironko Uganda wamepata mshituko baada ya mchezaji kuzimia kwenye uwanja wa mpira na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali.
Simon Musika ana umri wa miaka 30 na alicheza kwenye hiyo mechi ya timu za mitaani kwa dakika 15 kabla ya kuzimia na kufariki dunia ambapo baada ya taarifa za kifo chake ilibidi mechi isimamishwe.
Ndugu wa marehemu walikusanyika kwenye uwanja wa mpira muda mfupi tu baada ya kifo cha mchezaji huyo.

No comments: