Kwa nini niliomba muongozo-Sakata la Mgomo wa Madaktari
Leo nilitaka kuomba muongozo wa Spika kwa mujibu wa Kanuni 49 (2) baada ya Waziri wa Afya kutoa kauli juu ya utekelezaji wa madai ya madaktari. Kanuni hiyo inataka kauli isiwe ya kuzua mjadala lakini aliyoyaeleza waziri juu ya uboreshaji wa maslahi ya madaktari yanazua mjadala kwa kuwa yanatofautiana na majibu ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoyatoa bungeni jana, (Juni 21, 2012) na pia hayana uhalisi.

Mathalani,
wakati serikali ikidai imeongeza posho ya kuitwa kazini (on call
allowance) toka Februari, 2012 na kutumia bilioni 7.9 kwa miezi
michache, imetenga kwa watumishi wa Afya bilioni 18.9 tu kwa mwaka mzima
wa 2012/2013 kiwango ambacho hakitoshi.
Hivyo
nilitaka kuomba muongozo Spika awezeshe kauli hiyo ijadiliwe kama
ilivyokuwa kwa kauli juu ya fedha za rada. Nakusudia kumuandikia barua
Spika kushauri aelekeze kamati ya bunge ya huduma za jamii kauli hiyo ya
waziri.
Pia bunge
halipaswi kunyimwa fursa ya kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa ibara ya
63 ya kuishauri na kuisimamia serikali kusuluhisha mgogoro na madaktari
ili kuepusha mgomo wenye athari kwa nchi na wananchi kwa kisingizio cha
kusudio la serikali kupeleka mgogoro mahakama kuu kwa kuwa mpaka leo
taarifa iliyotolewa bungeni bado hakuna shauri katika kitengo cha kazi.
Hivyo, Spika anapaswa kutoa jukumu kwa kamati husika ya bunge kuendelea
na usuluhishi kabla ya serikali kukimbilia mahakamani.
Wabunge tupewe nakala ya taarifa ya majadiliano ya pande mbili yaliyochukua zaidi ya siku 90 badala ya kupewa hotuba ya nusu saa ya upande mmoja wa serikali pekee.
Hata serikali ikizuia mgomo wa wazi kwa zuio la kimahakama ieleweke kuwa mgomo wa chinichini kwa watumishi wa afya ambao una athari ya muda mrefu kwa maisha ya wananchi nchini.
Mwisho, serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima na ipanue wigo wa mapato.

John John Mnyika.
Mbunge Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
22 Juni, 2012
No comments:
Post a Comment