Wednesday, June 27, 2012

KIONGOZI WA MADAKTARI ATEKWA, AOKOTWA AKIWA KATIKA HALI MBAYA



Taarifa zilizotufikia ni kwamba Kiongozi wa Mgomo wa Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka ametekwa na ameokotwa akiwa katika hali mbaya sana.
Kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forums, Dk Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye 'face to face' kwa ajili ya mazungumzo.
Tukio hilo limetokea wakati kumekuwepo na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao hata hivyo wameonekana kusalitiana kwa kutokuwa na msimamo wa pamoja, kwani maeneo mengine huduma zimeendelea kama kawaida.

No comments: