| Jumatano June 6, 2012 saa 7:32 mchana KAKA yangu mzaliwa wa kwanza aitwaye ABRAHAM JOHN MLAULE (Kulia mwenye tai na miwani) alifariki dunia katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Vipimo vya madaktari vinaonyesha alikuwa na malaria kali iliyoambatana na maumivu ya tumbo kiasi cha kusababisha ashindwe kula kwa muda mrefu. NATOA SHUKRANI ZANGU KWENU nyote mlionisaidia kwa namna yoyote ile katika kufanikisha safari yangu toka Arusha hadi Dodoma kuhudhuria mazishi. Tulimzika Jumamosi June 9, 2012 katika makaburi ya Msalato Mnadani. MUNGU AWABARIKI SANA. |
|
No comments:
Post a Comment