Saturday, July 14, 2012

RAIA WA CUBA AJARIBU KUVUNJA REKODI YA KUENDESHA BAISKELI KUBWA ZAIDI DUNIANIFelix Guirola akisaidiwa na marafiki kuendesha baiskeli yake.Akichomeka gurudumu kwenye baiskeli yake.

Akichagua spea kwa ajili ya baiskeli hiyo.

FELIX GUIROLA, mpanda baiskeli wa Cuba anajaribu kuvunja ‘rekodi’ yake ya kuendesha baiskeli kubwa zaidi duniani ambayo inatambuliwa katika Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness.
Mtu huyo amekuwa akifanya jaribio hilo la kuendesha baiskeli hiyo yenye urefu wa mita 5.5 kwenda juu akipita katika mitaa ya Havana ya Zamani akisaidiwa na watu watatu. Hata hivyo, madai ya jamaa huyo ambaye ni fundi wa kuchomelea hayajathibitishwa na wahusika, na sasa Terry Goertzen, raia wa Canada ndiye anashikilia rekodi hiyo.
Guirola alitengeneza baiskeli yake kubwa ya kwanza yenye urefu wa mita mbili mnamo 1983 kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya dada yake mlemavu ambaye alifariki mwaka 1994.

No comments: