Monday, July 23, 2012

TAMKO LA CHADEMA KWA MADIWANI WA VYAMA VINGINE ARUSHA Kwa muda mrefu kumekuwa na mgogoro wa Uchaguzi wa MEYA wa manispaa ya Arusha, ambayo ilitokana na ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uchaguzi wa Meya ambayo akidi yake ilikuwa haijatimia. Ikumbukwe kuwa Mhe. Kivuyo ambaye katika sakata hilo alijikuta akichaguliwa kwa hila kuwa NAIBU MEYA, alifikia hatua ya kujizulu nafasi hiyi na kukiri mbele ya waandishi wa habari na wananchi wa Arusha kuwa uchaguzi uliofanyika haukuwa wa haki na yeye alipewa nafasi hiyo kwa hila, kitu ambacho baada ya tafakari ya kina aliamua kujiuzulu ili asiwe sehemu ya dhambi hiyo na kujikuta anakalia KITI CHA DAMU. Jambo hili pia limekuwa likisemwa na baadhi ya madiwani wa CHAMA CHA MAPINDUZI pindi tunapokutana nao kuwa mfumo wa chama cha CCM unazuia kuyatamka haya lakini ukweli ni kuwa huo uchaguzi wa meya uliofanyika na Mhe Gaudence Lyimo kupata nafasi hiyo ulikuwa batili kwa mujibu wa kanuni, lakini mbaya zaidi, umepelekea damu kumwagika, jambo ambalo ndio baya.

No comments: