Monday, October 22, 2012

AVUNJA REKODI YAKE MWENYEWE KWA KUPATA MTOTO AKIWA NA UMRI WA MIAKA 96

 
Kikongwe Ramjit Raghav aliyevunja rekodi yake kwa kupata mtoto akiwa na umri wa miaka 96.
MZEE Ramjit Raghav, kutoka nchini India amevunja rekodi yake mwenyewe baada ya kupata mtoto wa pili wa kiume katika kipindi cha miaka miwili akiwa na umri wa miaka 96.
Randy Ramjit na mkewe Shakuntala Devi (52) walipata mtoto wa kiume mwenye afya njema mapema mwezi huu.
Kikongwe huyo na mpenzi wake wanafurahia sana tendo la ndoa. Shakuntala anadai mumewe akiwa kitandani ni sawa na kijana wa miaka 25.

 
Kikongwe Ramajit Raghav (kushoto) akiwa pamoja na familia yake.
'Naweza kufanya mapenzi mara tatu au nne kwa usiku mzima,' alieleza bwana Randy nje kidogo ya nyumba yake huko Haryana, India. 'Majirani zetu wanakuwa na wivu kwa kuniuliza mara kwa mara juu ya siri yangu hii, ila mimi nawajibu kuwa ni mapenzi ya Mungu.
'Nina afya njema na ninafurahia mapenzi na mke wangu. Nadhani ni muhimu kwa wanandoa kufanya mapenzi mara kwa mara. Mke wangu akinihitaji namkubalia na tunaweza kufanya usiku mzima ila kwa sasa tumeweka mambo yetu pembeni kwa ajili ya mtoto wetu.

 
Mtoto wa Mzee Ramjit Raghav.
'Namjali sana mke wangu na nampatia kila kitu anachohitaji . Ni mwananmke mwenye furaha.'
Randy, ambaye enzi zake alikuwa mwana mieleka alitengeneza vichwa vya habari mwaka 2010 baada ya kuvunja rekodi ya kuwa baba mzee kuliko wote duniani baada ya kupata mtoto wake wa kwanza aitwaye Vikramjeet akiwa na umri wa miaka 94, na kumpiku aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo, Mkulima kutoka India, Nanu Ram Jogi aliyepata mtoto akiwa na umri wa miaka 90 mwaka 2007.

 
Mke wa Ramjit, Shakuntala Devi.
Chanzo: www.metro.co.uk

No comments: