Club ya Yanga imeandika kwenye
club yake kwamba Katibu wa Baraza la wazee wa klabu hiyo Mzee Ibrahim
Akilimali ametoa ufafanuzi juu ya timu ya Yanga kutovaa jezi zenye nembo
nyekundu ya mdhamini wa ligi kuu Tanzaniza bara kampuni ya simu ya
Vodacom.
Akiongea na wandishi wa habari
makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga/Jangwani, Mzee Akilimali
amesema kamwe hawatakubali matakwa ya vodacom na TFF ya kuweka nembo
yenye doa jekundu katika jezi za Yanga.
Ni afadhali hao TFF watufute
katika ligi yao kama wataendelea kutulazimisha kuvaa jezi zenye nembo
nyekundu, kwani tupo radhi kubaki kucheza michezo isiyodhaminiwa na
Vodacom kama bao, ngumi, na mingineyo au hata kuhamia ligi ya visiwani
Zanzibar ambako tutacheza bila vikwazo.
Labda kwa wasiofahamhu
historia, Yanga mwaka 1953 mbele ya aliyekua Gavana wa Tanganyika, Sir
Edward Twinning ilikataa kuvaa jezi zenye madoa ya rangi nyekundu
ilizoletewa na timu pinzani ya mabaharia kutoka Uingereza, na kusema ni
bora tucheze vifua wazi kuliko kuvaa jezi hizo alisema ‘Mzee Akilimali’.
Mzee Akilimali aliongeza pia
kuwa hata chama cha TANU kiliwahi kuiomba Yanga ibadilishe rangi zake za
kijani na njano, lakini Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa
Julius Nyerere aliwambia wajumbe wa TANU kwamba waacheni Yanga na rangi
zao, rangi hizo wanazotumia zinawatambulisha wao, madini, na maliasili
ya nchi hii.
Aidha pia Mzee Akilimali
alisema mnamo mwaka 1963, aliyekuwa mkuu wa mkoa Dar es salaam mh
Mustapha Songambele aliziita timu zote zilizokuwa na majina ya kigeni
kwamba zibadilsihe majina hayo na kujiita majina ya kitanzania, timu
zote zilibadilisha majina lakini Young Africans ilipotafsiriwa ilileta
maana ya Vijana wa Afrika hali iliypolekea Yanga kuendelea kutumia jina
lake, na timu zingine kubadilisha majina yao.
Kaimu katibu mkuu wa Yanga,
Lawrence Mwalusako amesema wanashindwa kuelewa kwa nini vodacom mwaka
huu wanalazimisha Yanga ivae jezi zenye rangi jekundu, ili hali mwaka
jana walikubali kutoa jezi zenye rangi nyeusi ya doa la vodacom.
Mkataba kati ya TFF na Vodacom
sisi hatujauona, sasa inakuwa vigumu kujua kipi kimeandikwa ndani ya huo
mkataba na kinapaswa kutekelezwa, ilipaswa vilabu tuepewe nakala ya
mkataba tuusome kabla ya kusainiwa, ili na sisi tupate nafasi ya kutoa
hoja katika mkataba huo, lakini wao wamefanya kinyume kisha
wanatulazimisha tuvae hiyo nembo, ikiwa hatujui maslahi ya mkataba
wenyewe alisema ‘Mwalusako’.
Yanga itashuka dimbani siku ya
jumamosi kucheza na timu ya Ruvu Shooting katika muendelezo wa michezo
ya Ligi ya Kuu ya Vodaco nchini raundi ya 8.
Naye Mzee Mwika aliongezea kwa
kutoa mfano kwamba “haiwezekani Mnyamwezi aje zake Pwani toka Tabora
atukataze wazaramo kucheza mdundiko au dogoli”, alichokikuta anapaswa
kukifuata na kukiheshimu na sio kuja na kutaka kubadillisha tamaduni za
watu, Yanga ina rangi kuu tatu (3) Kijani, Njano na Nyeusi.
No comments:
Post a Comment