Hafla hiyo iliongozwa na Baba
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mbeya Evaristo Chengula, ambapo mgeni
rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ambaye katika sherehe
hiyo aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Rungwe ndugu Crispin Meela.
Katika hotuba yake Baba Askofu
ameiomba Serikali kufanya haraka kutoa eneo la ardhi ili hospitali hiyo iweze
kupanua shughuli zake ikiwa ni pamoja kuanzisha Chuo cha Wauguzi ili kuisaidia
Serikali katika uboreshaji wa sekta ya Afya nchini.
Askofu Chengula amesema Kanisa la
Kikatoliki lina nia ya kuleta maendeleo zaidi katika hospitali hiyo licha ya
wananchi 9 kugoma kuachia maeneo yao ili kupisha ujenzi wa majengo ya hospitali
kwa ajili ya chuo na mahabara ya kisasa.
Aidha uongozi wa hospitali hiyo
ulimweleza mgeni rasmi kuwa zaidi ya watu 150,000 hupatiwa huduma ya malazi kwa
mwezi na kwamba zaidi ya wagonjwa 400,000 hutibiwa na kurejea makwao.
Vilevile hospitali hiyo imelenga
kutoa ajira kwa watumishi 120 wa kada mbalimbali wakiwemo madaktari, wauguzi,
mafamasia na kada nyingine na kwamba kila mmoja waweze kuifikisha hospitali
hiyo ambapo kwa mwaka imeweza kuhudumia zaidi ya wagonjwa 5600 na huduma ya
upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya 503.
Hata hivyo hospitali hiyo
inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi wa kada mbalimbali na uongozi umeitaka
Serikali kuongeza watumishi, kwani hospitali hiyo imekuwa ikitoza kiasi kidogo
cha fedha, hali iliyopelekea kuwa kimbilio kwa wananchi wengi kutoka mikoa ya
Rukwa, Iringa na Ruvuma pia nchi za Zambia na Malawi kutokana na ubora wa
huduma unaotolewa na hospitali hito.
Wakati huohuo hospitali inakabiliwa
na changamoto za upungufu wa vitanda, ambapo hivi sasa kuna vitanda 140 za
kulaza wagonjwa katika wadi tano zilizopo, ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa,
ulipaji wa mishahara kwa wakati, pesa za kulea watoto wanaokaa katika mazingira
hatarishi na hawajiwezi, ukatikanaji wa umeme na barabara mbovu ambayo huweka
adha kwa wagonjwa pindi wanapokimbizwa katika hospitali hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Abbas Kandoro ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bwana
Crispin Meela amesema ombi la ardhi litaanza kufanyiwa kazi Oktoba 22 mwaka huu
na suala la barabara atawasiliana na wakala wa barabara nchini(TANROADs), ili
baada ya hiyo iingia katika mpango wa mkoa ili kuboresha miundombinu katika
hospitali hiyo na kwamba barabara hiyo yenye urefu wa Kilimita 4 iwe lami.
Askofu Chengula amewashukuru
wafadhili waliolazwa katika Hospitali hiyo na pia anaomba ruzuku ya madawa
katika bohari ya serikali(MSD) huku huduma za watu wanaoishi na VVU, pia huduma
ya mama na mtoto ambayo ilipaswa kutolewa na serikali.
Mbali na sherehe ya Jubilee Askofu
Chengula alizindua mnara rasmi wa Jubilee hiyo na kuwapa daraja la kipaimara
vijana na wazee wapatao 200 katika sherehe iliyofana na kuwataka waeende katika
maadili yatakayompendeza Mungu na wanadamu pia nao kuleta amani na upendo kwa
waumini na wasiokuwa waumini kwani kumekuwa na matukio ya uhalifu ambao wengi
hufanya na watu waliopata kipaimara hivyo vijana wasifurahie tendo hilo tu bali
wafuate Mema kwa kristo.
No comments:
Post a Comment