Monday, October 15, 2012

WALIPOTEMBELEA NCHI JIRANI YA DRC...



Stori:Sifael Paul
Mastaa wawili wakubwa wa Gospo Bongo, Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, wamejikuta wakipigwa na butwaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuwekewa ulinzi wa kutisha, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika Mji wa Goma nchini humo ambapo waimbaji hao walikuwa na mwaliko kati ya Septemba 14 hadi 17, mwaka huu, uliolenga kueneza neno Mungu kupitia nyimbo zao zinazopendwa na wengi.
Ilifahamika kuwa katika ziara hiyo akina Mbasha walialikwa na kanisa lililotajwa kwa jina la Mji wa Makimbilio lililopo Goma.

KAZI YAANZA
Mara baada ya kukanyaga ardhi ya mji huo, akina Mbasha walikuta wamewekewa ulinzi mkali kutoka kwa wanajeshi wa nchi hiyo wa Kundi la Makomandoo hali iliyowafanya washindwe kuamini kwani haijawahi kutokea kulindwa kiasi hicho maishani mwao.

NI KILA SEHEMU
Shuhuda wetu alitonya kuwa kuanzia walipofia, kila sehemu waliyokwenda walikuwa wakisindikizwa na msafara wa wanajeshi hao na siyo polisi kama ilivyo Bongo.
“Unaambiwa muda pekee ambao walikuwa wakikaa peke yao ni wakati wa kulala. Hata kanisani walipelekwa kwa ulinzi mkali. Wakati wa kuimba ndiyo kabisa askari walikuwa wametanda kila kona kwani kulikuwa na umati mkubwa sana uliokuwa ukifurahia huduma yao,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:
“Yaani waliondoka mikononi mwa Wanajeshi wa Makomandoo baada ya kumaliza ziara yao na kutolewa kwa ulinzi katika mji huo.”

Shuhuda huyo alisema, mwanzoni mastaa hao wanandoa walikuwa wakihofia na kuhisi labda wametekwa lakini ulifika muda wakawa wamewazoea wale wanajeshi ambapo tayari walishajenga nao urafiki.
BOFYA HAPA KUMSIKIA FLORA
“Kwa kweli nchi ya watu ni ya watu tu, tulienda kwa ajili ya shoo lakini tukashangaa kupewa ulinzi wa ajabu kiasi kile. Sisi wenyewe tulishindwa kuamini, awali tulidhani tumefanya makosa ndiyo maana tukaletewa wanajeshi lakini walipojitambulisha na nia yao tukawa na amani.”

MBASHA
“Mh! Ule ulinzi hatujawahi kuupata kokote, hatukuamini kilichotokea, tulishangaa tu, kwani silaha walizokuwa nazo zilikuwa za moto na hatari. Unajua kuna wakati tulihisi tunatekwa lakini baadaye wakawa marafiki zetu, kwa kweli tulilindwa sana, tena wale ni makomandoo.”

KWA NINI ULINZI MKALI?
Pamoja na kushangazwa na hali hiyo lakini ukweli ni kwamba walikutana na ulinzi huo kutokana na sifa ya eneo la Goma ambalo linadaiwa kugubikwa na vita kati ya serikali na waasi nchini humo, hivyo kuwaacha akina Mbasha bila ulinzi wangeweza kuuawa au kufanyiwa vurugu.

No comments: