MShiriki
wa Miss Tanzania 2012, Babylove Kalala akijaribu kumuuma nyoka wakati
mrembo huyo pamoja na wenzake wanaowania taji hilo walipotembelea eneo
la Snake Park mjini Arusha. Habari na picha kwa hisani ya Father Kidevu
Blog.
********
Warembo
wanaowania taji la Miss Tanzania 2012 jana walitembelea eneo la Utalii
la ufugaji nyoka la mjini Arusha maarufu ARUSHA SNAKE PARK na kujionea
nyoka wa aina mbalimbali, Mamba, Kenge, ndege aina ya Bundi, Tai na
Tumbiri.
Warembo
hao wapo Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwaajili ya kutembelea vivutio
mbalimbali vya Utalii nchini na kujifunza mambo tofauti tofauti.
Pamopja
na kujionea Nyoka hao na kucheza nao kwa kuwa vaa shingoni pia warembo
hao walipata fursa ya kujifunza juu ya tamaduni za Mila ya Wamaasai na
kutembelea vibanda vya urembo wa Kimasai.
Mrembo wa Kilimanjaro, Anande Raphael (kushoto) akipozi na Mrembo wa Lindi, Irine Veda huku wakiwa na nyoka.
Mrembo Diana Hussein nae aliweka mapozi yake na nyoka
Warembo wakimwangalia Catherine Masumbigana aliyemzungusha nyoka shingoni
Hapa ni Mrembo wa Kitongoji cha Ukonga jijini Dar es Salaam, Mary Chizi akila pozi.
Jesca Haule mrembo kutoka Kitongoji cha Chang'ombe jijini Dar es Salaam nae alionesha ujasiri wake wa kumvaa nyoka.
Wapo walio ogopa kama Miss Photogenic 2012, Lucy Stephano
Mrembo wa Mbeya Caren Elias nae aliogopa sana. Kulia ni Noela Michael kutoka Tabata nae akiogopa hata nyoka hajamshika.
Lightness Michael nae aliweka pozi na Nyoka
Fina Revocatus kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha akipozi na wenzake.
Warembo wakiwa katika eneo la Historia ya Jamii ya wamaasai ambayo nayo ipo Meserani mjini Arusha.
Mrembo wa Pwani, Rose Lucas akipita katika sehemu ya Historia ya Wamasai.
Miss Tanzania 2011, Salha Izrael nae akitoka katika vibanda vya biashara
Elizabeth Diamond mrembo kutoka Singida akiangalia shanga na urembo za aina mbalimbali kwaajili ya kununua.
Mrembo wa Kahama Mkoani Shinyanga, Happiness Rweyemamu nae alikuwa akitafuta cha kununua.
Mkuu wa
Itifaki ya Miss Tanzania, Albert Makoye akipiga picha na warembo wa Miss
Tanzania akiwa amevalia vazi rasmi la Kabila la Kimasai.
Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye na Mrembo Joyce Baluhi wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya jamii ya Wamaasai.
No comments:
Post a Comment