Wednesday, November 14, 2012

Hamida Hassan na Imelda Mtema
MSANII Baby Joseph Madaha hivi karibuni amenaswa nyumbani kwa mwanamuziki Juma Kassim ‘Nature’ maeneo ya Temeke jijini Dar.

 
Baby Madaha.
Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitutonya kuwa, Baby Madaha alinaswa juzikati geto kwa Nature akipika msosi, mazingira yaliyoashiria kuwa, kuna kitu kati yao.
“Mbona siyo habari huku Temeke, yaani juzi nilimuoona kwa macho yangu akipika msosi pale nyumbani kwa Nature ila mkifuatilia mnaweza kuupata ukweli zaidi,” alidai mtoa habari huyo na kuongeza:
“Unajua mkeo akiwa hayupo kisha wewe ukaingiza mwanamke mwingine ndani kwako ambaye si ndugu yako kisha ukamruhusu aingie jikoni ni lazima watu watafikiria tofauti na hata mkeo akisikia hawezi kukuelewa.”

 
Juma Kassim ‘Nature’.
Baada ya kuinasa habari hiyo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwatafuta wawili hao na wa kwanza kupatikana alikuwa Baby Madaha ambaye alikiri kupika na kupakua kwa Nature.
“Ni kweli huwa nakwenda pale na kupika na kupakua, si unajua nafanya kazi na TMK Wanaume Halisi. Kwa hiyo nikienda pale kwa Nature na ukafika muda wa chakula, itakuwa si busara kuwaacha wanaume waingie jikoni wakati mimi nipo,” alisema Baby Madaha.
Akilizungumzia hilo, Nature alisema: “Mke wangu (Mama Happy) Mwanza kikazi. Baby Madaha kweli nipo naye karibu lakini ni kwa sababu za kisanii, hakuna kingine.”


No comments: