Friday, November 2, 2012

MHARIRI BUSINESS TIME ASHAMBULIWA KWA RISASI

Mnaku Mbani Lukanga (Mhariri wa gazeti la Business Times ) akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi alipohamishwa kutoka hospitali ya Temeke alikolazwa jana mara baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi hapo jana usiku katika mtaa wa Lugoda akiwa anaelekea nyumbani kwake Mbagala usiku wa saa mbili jioni na watu wasiojulikana.

Katika tukio hilo, alikuwa na abiria wenzake 6 ambao nao walipigwa risasi.Baadhi yao walitolewa risasi na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Mnaku alipigwa risasi juu yo mdomo na risasi hiyo kutokea kwenye shavu lake la kushoto. Bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari.

FATHER KIDEVU BLOG na wadau wake inatoa pole kwa Mnaku, ndugu jamaa na marafiki na inaungana na jamii kwa ujumla kumuombea aweze kupona haraka na kurudi katika hali yake ya kawaida na kuendelea na majukumu yake.SOURCE LEMUTUZ BLOG.

No comments: