Ni watu wengi wamehitaji
kufahamu kuhusu kauli ya familia ya Marehemu mwigizaji/msanii Sharo
Milionea baada ya tangazo la Airtel lenye sauti yake kuendelea kutumiwa
na kampuni hiyo wiki kadhaa baada ya Sharo kufariki kwa ajali ya gari
iliyotokea novemba 26 2012 Tanga.
Mjomba wa Marehemu ambae ndio
msemaji wa familia Shaban Mkiete amethibitisha kwamba wamezungumza na
kukubaliana na kampuni ya Airtel na hapa namkariri akisema “ni kweli
tumekubaliana, kwa mujibu wa makataba wao lilikua linaisha terehe 31
mwezi huu tumekubaliana kwamba liendelee kwa makubaliano ambayo
tumekubaliana nayo sisi kati ya mzee Majuto ambae bado yupo na familia
ya Marehemu, mama mzazi wa Sharo Milionea ameridhia hilo hakuna tatizo”
Siku ya msiba millardayo.com
ilipopata nafasi ya kuongea na mwakilishi wa Airtel alisema Marehemu
Sharo Milionea alifariki ndani ya kipindi cha miezi 6 tu toka asaini
dili la kuwa balozi wa Airtel na kufanya matangazo mbalimbali yeye na
mzee Majuto.
Sio tu dili la Airtel,
imefahamika tayari Sharo Milionea alikua amesaini mikataba mizuri na
makampuni mbalimbali wakiwemo Wamarekani waliotengeneza filamu maarufu
Afrika kama Yellow Card, Neria na nyingine ambapo kwa sasa Wamarekani
hao wako hapa Tanzania na wametengeneza series kadhaa ikiwemo Wahapahapa
na Siri ya Mtungi ambayo ndio Sharo Milionea kashiriki ndani na mpaka
anafariki tayari alikua ameshaanza kucheza igizo hilo.
Unaweza kumsikiliza mjomba wa Marehemu akiongea hapo chini.
No comments:
Post a Comment