Na Mwandishi Wetu
ILIKUWA ni kama mchezo wa kuigiza wakati Padri, Ambros Mkenda wa Kanisa la Katoliki la Mpendae lililopo Zanzibar alivyopigwa risasi nyumbani kwake Kitomondo mjini Unguja Desemba 25, mwaka huu na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, lilitokea saa 12 za jioni maaeneo ya Kitomondo nyumbani kwa padri huyo lilikuwa kama mchezo wa kuigiza na kusababisha mshtuko mkubwa kwa watu mbalimbali.
“Lilikuwa ni tukio la haraka sana, padri alikuwa akitokea kanisani, alisimama getini kungoja kufunguliwa mlango, ghafla watu wawili waliokuwa katika pikipiki walifika na kumpiga risasi dhamira yao ilikuwa ni kumuua, akaanguka chini na watu wale kuondoka kwa kasi,” alisema shuhuda mmoja.
Shuhuda mwingine alisema kuwa tukio hilo lilizua hofu kwa walioshuhudia na kuamini kuwa padri alikuwa amekufa baada ya kufyatuliwa risasi mbili lakini moja ilimkosa na nyingine kumpata kidevuni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hakuna mtu anayeshikiliwa lakini uchunguzi unaendelea.
Father Mkenda hivi sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo Askofu wa Anglikan, Michael Hafidh amesema bado ni mapema mno kuelezea kama ataendelea kuwepo hospitalini hapo au atasafirishwa huku akilaani vitendo vinavyoendelea vya kuwavamia viongozi wa dini.
No comments:
Post a Comment