Friday, January 11, 2013

Haruna Boban kivutio kwa Waarabu

Haruna Moshi Shabani ‘Boban’ wakati akishuka kwenye ndege nchini Oman.
Na Saleh Ally, Oman
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi Shabani ‘Boban’, amekuwa kivutio kwa mashabiki wengi wa soka mjini hapa, hasa wale waliokuja kuipokea timu hiyo.
 
Boban amekuwa kivutio kutokana na mashabiki wengi kumuulizia kama alikuwa amekuja, mashabiki hao ambao wanazungumza Kiswahili fasaha walikuwa wakimuulizia Boban kila mara.
 
Asilimia kubwa ya mashabiki waliokuja kuipokea Simba walitaka kujua Boban yuko wapi, walipoonyeshwa walitumia dakika kadhaa wakimuangalia au kuonyeshana.
 
Boban alikuwa kati ya wachezaji wachache wa Simba waliowasili mjini hapa kwa ajili ya kuanza kambi ya wiki mbili kujiandaa na ngwe ya lala salama ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.
 
Baadhi walisema Boban alikuwa anawavutia wengi kwa kuwa aliwahi kucheza soka nchini hapa, hivyo wengi wanakijua kiwango chake.

No comments: