Wednesday, January 9, 2013

HUYU NDIO MWIZI ANAEDAIWA KUJICHOMA MOTO NYUMBANI MWIMBAJI JOSE CHAMELEONE.

Nyumbani kwa Jose Chameleone.
Gazeti la Sunday Mail la Uganda limeripoti kwamba Polisi wa nchi hiyo wanaendesha uchunguzi ambapo huenda wakamfungulia mashitaka ya mauaji mwanamuziki Joseph Mayanja, mke wake Daniella na kundi la muziki la Leon Island.
Ni kutokana na kifo cha Robert Karamagi (27) aliyefariki katika Hospitali ya Mulago baada ya majeraha aliyoyapata nyumbani  kwa mwanamuziki huyo huko Seguku Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kajjansi Ibrahim Saiga alisema wamechukua ushahidi mbalimbali kutoka kwa majirani na mashuhuda walioona, ushahidi ambao unapingana na ule uliotolewa na familia ya Mayanja.
Huyu ndio mwizi mwenyewe ambae anadai hakujichoma mwenyewe bali kina Chameleone ndio walimchoma.
Pamoja na kusema faili la uchunguzi huo litapelekwa kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP) kwa ushauri,  Saiga alisema pia baba wa Karamagi alikana kwamba mwanaye alijimwagia mafuta na kujiwasha moto, pia alisema mwanaye alipomwita hospitalini alimwambia aliteswa, akafungwa kamba, akamwagiwa mafuta na kuchomwa moto na mwanamuziki huyo pamoja na wenzake wa kundi lake.
Jose Chameleone akihojiwa na NTV Uganda na kusema kwamba hilo swala wameliacha kwenye mikono ya polisi, gazeti la sunday mail limeripoti pia kwamba alhamisi iliyopita Jose Chameleone alihojiwa na wapelelezi kwa muda mrefu lakini aliachiwa kwa dhamana.

No comments: