Tuesday, January 8, 2013

LIONEL MESSI ATWAA TUZO YA BALLON D'OR


Lionel Messi akiwa na tuzo yake ya Ballon d'Or.
 Fabio Cannavaro, akionyesha jina la mshindi wa Ballon d'Or, Lionel Messi.
MSHAMBULIAJI wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa nne mfululizo.
Messi (25) alifunga jumla ya mabao 91 mwaka jana na aliwashinda wachezaji wengine Andres Iniesta wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real Madrid.
Vicente del Bosque, akituzwa kuwa kocha bora na Abby Wambach, alishinda tuzo kwa upande wa akina dada.
Messi alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya the Ballon d'Or, tuzo ambayo hukabidhiwa mchezaji bora wa mwaka katika sherehe iliyofanyika mjini Zurich.
Mesi sasa ni mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo ya Ballons d'Or kwa miaka minne mfululizo na kuvunja rekodi ya aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa na rais wa UEFA kwa sasa, Michel Platini, ambaye alitwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo mwaka 1983, 1984 na 1985.

No comments: