Tuesday, January 22, 2013

MH PINDA AFUNGUA MASHINDANO YA KIKAPU KANDA YA TANO, TANZANIA YAANZA NA VICHAPO WAKAKA NA WADADA ZAO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiingia Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo kwa ajili ya ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu, iliyoanza leo kwenye Uwanja huo. Wengine kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Magessa.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijiandaa kutupa mpira kwenye kikapu kuashiria ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu, iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha Mmarekani wa Tanzania, Jay Scannier akitoa maelekezo kwa wachezaji wake, wakati wa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Uganda ilishinda kwa vikapu 80-66. Timu ya wanawake nayo ilifungwa na Kenya.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mchezaji mwenye urefu wa futi 7.2 wa Uganda, Gombya Sam wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu, iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Uganda iliifunga Tanzania 80-66.

Mchezaji wa Tanzania, Abdallah Ramadhan 'Dullah' akidanki

Mohamed Ally 'Dibo' wa Tanzania akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Uganda

Wachezaji wa Tanzania wakijaribu kumdhibiti mchezaji wa Uganda

Mchezaji wa Tanzania, Maige Civillian Yunzu akiruka juu kuifungia timu yake  

Soud Mlanga wa Tanzania (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Uganda

Mchezaji wa Tanzania (7) akifunga

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mchezaji wa Tanzania, Juma Kisoky wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu, iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezaji wa Kenya, Desmond Owiri akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Burundi, Ntagunduka Jean De Dieu katika mechi ya kwanza ya Wanaume ya michuano ya Kikapu Kanda ya Tano Afrika, leo Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Kenya ilishinda 71-63.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mchezaji wa Tanzania, Abdallah Ramadhan 'Dullah' katika ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu, iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Dullah akimdhibiti mchezaji wa Uganda

Wachezaji wa timu ya wanawake ya Misri wakiwa wamelala wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatoa hotuba ya ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika, iliyoanza leo Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu, iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kanda ya Tano Afrika ya Mpira wa Kikapu, iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Soud Mlanga wa Tanzania (kushoto) akikimbilia mpira dhidi ya mchezaji wa Uganda

No comments: