Sheria ya kudhibiti umiliki wa bunduki New York
Jimbo la New York
limeidhnisha sheria za kudhibiti matumizi ya bunduki Marekani. Mswaada
huo unapunguza kiwango cha risasi na bunduki na kuanzisha kuchunguza
afya za watu wanaotaka kununua bunduki.
Tangazo hilo limetolewa siku moja kabla ya Rais Barack Obama kutangaza mipango yake ya kudhibiti matumizi ya bunduki kitaifa.
Vile vile sheria hiyo inadhibiti
ununuzi wa bunduki , ukubwa au udogo wa risasi ambazo mtu anaweza
kununua hata kuifanya vigumu kwa mtu mwenye matatizo ya kiakili kununua
bunduki.
Hii ndiyo sheria ya kwanza ya kudhibiti bunduki
tangu mauaji ya kiholela ya watoto 26 na walimu katika eneo la
Connecticut mwezi uliopita.
Jimbo la New York sasa lina sheria kali zaidi ya kudhibiti bunduki nchini Marekani.
Wabunge wa Democrats na wengi wa chama cha
Republican waliunga mkono sheria hiyo ya kuruhusu tu risasi saba na
kuongoza shughuli za kuwakagua watu wanaonunua silaha za kibinafsi.
Kadhalika watu wanaotaka kununua bunduki wanachunguzwa akili yao kwanza.
Akitia saini mswada huo kuwa sheria Gavana wa
New York Andrew Cuomo amesema ikiwa watu watatumia busara, mauaji ya
kiholela ya bunduki yatakwisha.
Shirika la kitaifa linalotetea umiliki wa bunduki limesema kuwa sheria hiyo imepitwa na wakati.
No comments:
Post a Comment