Monday, February 11, 2013

AUWAWA WAKIGOMBANIA MWANAMKE MTAA WA ITIJI NONDE MBEYA HII NDIYO HABARI KAMILI TOKA POLISI


MNAMO TAREHE 08.02.2013 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA ITIJI KATA YA ITIJI JIJI NA MKOA WA MBEYA. DANIEL S/O MWASALEMBA,MIAKA 18,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA ITIJI ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA  KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI UPANDE WA KUSHOTO NA  PETER S/O BOSCO,MIAKA 25,MFIPA,MPIGA DEBE,MKAZI WA ITIJI. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA  UKIWA UCHI KANDO YA BARABARA. CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA KUMGOMBEA MWANAMKE ELIZABETH D/O MICHAEL, MIAKA 18,KYUSA,MUUZA POMBE ZA KIENYEJI KATIKA KILABU KIITWACHO MUSOMA MKAZI WA ITIJI. KABLA YA TUKIO MAREHEMU NA MTUHUMIWA AMBAO WOTE WALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA ELIZABETH D/O MICHAEL WALIPIGANA KILABUNI HAPO TAREHE 07.02.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS WAKIMGOMBEA MWANAMKE HUYO KISHA KUAMULIWA NA WATEJA WENGINE NA MTUHUMIWA ALIONDOKA NA MWANAMKE HUYO HADI NYUMBANI KWA MWANAMKE NA KUANZA KUMPIGA.  

 HATA HIVYO ELIZABETH D/O MICHAEL  ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA KURUDI KILABUNI AMBAPO ALIKUTANA NA MAREHEMU NA KUMWELEZA TUKIO HILO  AMBAYE WALIKUBALIANA  KURUDI WOTE NYUMBANI KWA MWANAMKE HUYO. MAJIRA YA SAA 01:30HRS MTUHUMIWA PETER S/O BOSCO ALIRUDI NYUMBANI KWA ELIZABETH D/O MICHAEL NA KUMKUTA MWANAMKE HUYO  AKIWA NA MAREHEMU CHUMBANI HIVYO ALIWAFUNGIA  MLANGO KWA NJE NA KWENDA KUTAFUTA KISU NA ALIPORUDI ALIVUNJA MLANGO KISHA UGOMVI BAINA YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA ULIANZA UPYA NA MTUHUMIWA ALIMCHOMA MAREHEMU KISU KIFUANI  UPANDE WA KUSHOTO  NA KUSABABISHA MAREHEMU KUDONDOKA CHINI HUKU DAMU NYINGI ZIKIMTOKA NA  MTUHUMIWA KUTOWEKA.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI ZAIDI. MTUHUMIWA PETER S/O BOSCO AMEKAMATWA KWA USHIRIKIANO BAINA YA POLISI NA WANANCHI WA ENEO HILO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI KWA KOSA LA MAUAJI. AIDHA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUGOMBEWA  ELIZABETH D/O MICHAEL  ANAENDELEA  KUHOJIWA  POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. AIDHA ANATOA RAI KWA WENYE  NDOA/MAHUSIANO  YA KIMAPENZI KUWA WAAMINIFU KWA WENZI WAO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA NA PINDI WANAPOKUWA NA MIGOGORO/MATATIZO WATUMIE NJIA YA MAZUNGUMZO KUMALIZA/TATUA MATATIZO/MIGOGORO  YAO.



[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: