Thursday, February 21, 2013


Diamond:Simu Yangu Iliyoibiwa Ndio Imesababisha Wimbo Wangu wa Ukimuona Kuvuja


Ngoma mpya kutoka kwa Diamond iliyovuja kupitia kwenye mitandao mbali mbali "ukimuona" ambayo pia inasikika kupitia Club mbali mbali, inasemekana kuwa ni demo, haikua imekamilika, lakini baada ya kupoteza sim yake aina ya Blackberry  iliyokua kwenye moja ya gari zake, ndio imesababisha kuvuja kwa wimbo huo..

"kweli kabisa siku release na hiyo nyimbo hapo ilipo haijaisha kabisa, hap katikati nilikua na sim yangu blackberry bold 4 niliipoteza bahati mbaya ikaibiwa, nilikua natoka nyumbani naenda magomeni, nafika kariakoo nakuta siioni sim. hasa katika sim mara nyingi nakuwa sometimes naweka nyimbo, kwasababu moja ya gari yangu haina cd, nilikua sijaweka sound, nikawa nasikiliza kupitia sim yangu nachomeka katika gari.ila kila kitu kinachotokea kwangu sometimes namshukuru mungu kwasababu yeye ndio anaandika, watu wanaipeda sana napoenda kwenye show zangu watu wanataka niimbe..namshukuru sana mungu".

No comments: