Tuesday, February 12, 2013


KILICHOSEMWA NA VIONGOZI MBALIMBALI BAADA YA PAPA KUTANGAZA KUJIUZULU


Msemaji wa serikali Ujerumani amesema anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria ndani ya nchi hiyo, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha uhusiano wa Vatican na Uingereza.
Askofu mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa Benedict wa XVI kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake, kiongozi wa Ujeremani Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala wa makanisa, waislamu na wayahudi.
Kasema uamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI  kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane kuliongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo, ni sahihi
Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu na sherehe za Pasaka ambapo kama hufahamu, tabia ya kujiuzulu kwa Papa si ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi karibuni.
.
Mwandishi wa BBC Roma Alan Johnston anasema habari hizi zimetokea kama radi, hakukua natetesi yoyote juu ya uwezekano kama huu na hata msemaji wa Vatican Father Federico Lombardi amesema  hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu juu ya tukio hili.
Kaka yake Papa akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Regensburg Ujerumani, Georg Ratzinger amesema Papa alikuwa ameanza kupata shida kutembea.
Wakati wa kutawazwa kama Papa, Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa mwenye na umri mkubwa wa miaka 78 na alitangazwa kuwa Papa Aprili 2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana ambapo Papa amekaririwa akisema “baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa, ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki”
Kwa mujibu wa BBC Swahili walioiandaa hii ripoti, Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki
.

No comments: