Tuesday, February 19, 2013

WASHINDI WA KITABU CHA ERICK SHIGONGO WAANZA KUCHUKUA ZAWADI ZAO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers ambaye pia ni mtunzi mahiri hapa nchini, Eric Shigongo (kushoto) akimkabidhi kitabu Tatu Majliwa ambaye ni mmoja wa washindi wa zawadi za kitabu chake.
Eric Shigongo akisaini kitabu chake kabla ya kumkabidhi mshindi, Tatu Majaliwa (kulia).…

Mmoja wa washindi wa kitabu cha Eric Shingongo kiitwacho 'KIFO NI HAKI YANGU', Tatu Majaliwa akifurahia zawadi yake.
Tatu akipata maelekezo ya jinsi ya kusoma magazeti ya Global kwa njia ya mtandao kutoka kwa mtaalamu wa kompyuta wa Global Publishers, Clarence Mulisa (kulia).
MMOJA wa washindi 50 wa kitabu cha Eric Shigongo kiitwacho 'KIFO NI HAKI YANGU', Tatu Majaliwa, leo amekabidhiwa zawadi yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho katika ofisi za kampuni hizo zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar. Tatu baada ya kupokea zawadi hiyo alifurahi sana na kuahidi kuwa mwanachama bora wa tovuti ya Global Publishers.

No comments: