Saturday, March 23, 2013


Na Imelda Mtema

‘VIDEO Queen’ maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye muda mwingi amekuwa akiishi Afrika Kusini ameelezea jinsi maisha ya Bongo yalivyomchosha huku usumbufu anaopata kutokana na makalio yake makubwa ikiwa moja ya sababu.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
Akipiga stori na Ijumaa juzikati, Masogange alisema umbile lake hilo limekuwa likimfanya akose amani anapokatiza mitaani, tofauti na Sauzi ambako wanawake wengi wamefungashia huku yeye akionekana ‘cha mtoto’.
“Muda mwingi niko Sauzi, Bongo miyeyusho na hili umbo langu nimekuwa nikisumbuliwa sana na wanaume lakini Sauzi hili langu la kawaida, wengi wamefungashia ile mbaya, kwa hiyo muda mwingi nitakuwa huko, huku nitakuwa nakuja na kuondoka,” alisema Masogange.

No comments: