Tuesday, April 16, 2013

ABIRIA WANUSURIKA KUFA BAADA YA NDEGE KUTUMBUKIA UFUKWE WA BALI (BALI BEACH), INDONESIA


ndege 859b3
Zaidi ya abiria 100 wamenusurika kimiujiza jana baada ya ndege kuvuka njia ya kutua/kuruka na kwenda hadi ufukwe wa Bali na kujikita kwenye bahari.

Mashuhuda walisema abiria waliokuwa wakihofia maisha yao walipiga makelele kutokana na kuchanganyikiwa huku ndege hiyo ya Lion Air ilipovuka njia ya kutua/kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa Ngurah Rai, karibu na Denparsar.
Ndege hiyo, ilikuwa imebeba abiria 101 na wafanyakazi saba - kisha ikatumbukia baharini kutoka urefu wa karibu mita 50 juu.

Abiria waliojawa na hofu walipigwa picha wakitoka kwenye ndege hiyo iliyovunjika vipande, huku wengi wakisubiri juu ya mabawa yake wakati waokoaji wakifanya juhudi za aina yake za ukoaji.



Uwanja huo wa ndege unafahamika zaidi kutokana na njia yake ya kuruka/kutua kurefushwa hadi baharini.Wengi wa abiria waliokoka kupitia milango ya dharura ambayo ilifunguliwa nusu sambamba na kiunzi hicho cha ndege na kufanya njia yao kuelekea ufukweni.

Baada ya kuwa wameokolewa kutoka kwenye ndege, walipelekwa kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Maofisa wa Uwanja wa Ndege walisema kwamba watu kadhaa walijeruhiwa kwenye ajali hiyo, lakini ukubwa wa majeraha yao haukuweza kufahamika.
Lion Air kwa sasa imefungiwa kusafiri katika Umoja wa Ulaya sababu ya hofu kuhusu viwango vya usalama wake.
Mkuu wa Polisi Bali, Arif Wahyunadi alisema: "Abiria wote na wafanyakazi wameondolewa kwenye ndege hiyo huku ikiwa imelala kwenye maji.
"Wamepokelewa na kuhudumiwa kwenye uwanja wa ndege."
Abiria wote na wafanyakazi wameokolewa salama na kwamba watu 22 wamepelekwa kwenye hospitali tatu tofauti kutokana na majeraha mbalimbali.
Taarifa za awali zinaonesha kwamba kulikuwa na abiria 101 na wafanyakazi saba ndani ya ndege hiyo.
Wahyunadi alisema ndege hiyo asili yake ni mji wa Bandung, mji wa tatu kwa ukubwa nchini Indonesia - kivutio cha utalii sababu ya ujenzi wake.
KUHUSU SHIRIKA LA NDEGE LA LION AIR:
Ndege ilikuwa ikimilikiwa na Lion Air, ambalo kaulimbiu yake ni: Tunawezesha Watu Kuruka.Ni shirika la ndege binafsi la pili kwa ukubwa nchini Indonesia, likishikilia sehemu kubwa ya soko la ndani.

Shirika hilo linafanya safari zake kwenda miji mikuu ya Indonesia, na pia safari nyingine Kusini Mashariki mwa Asia, ikichukua abiria kwenda Vietnam, Singapore, Malaysia na hata Saudi Arabia. Likianzishwa mwaka 1999, shirika hilo lilianza kutumia ndege moja aina ya Boeing 737-200.

Lion Air ni ndege zinazotoza viwango vya chini vya nauli ambalo linashikilia asilimia 45 ya soko nchini Indonesia.

No comments: